Huwa kila siku natafakari umuhimu wa Baba katika maisha ya kila Familia

Pole Sana mkuu
 
Kadhalika wapo wanawake wanawajaza sumu watoto wao kutichukia sisi mababa.
 
Ila sisi wengine Mola wetu ametupa mapenzi na familia zetu sana,hasa watoto,nawapenda sana watoto wangu,mpaka wake zangu wanajua.

Ila wapo baba wengine mtihani sana,mpaka unajiuliza inakuwaje akawa baba...?!
 
Nna shangaa Sana Sasa hivi sifa zote anapewa mwanamke, Baba kasahaulika! Mama yangu mzazi alifariki nikiwa km na 3yrs unfortunately siijui hata saiti yake na Sina kumbukumbu yoyote na Mama yangu mpenzi lkn nnaona picha zake na sisi tulipokuwa wadogo! MUNGU ailaze roho yake mahala pema peponi Amina! Baba alioa tena Mama yetu mlezi alitulea vizuri tuu hakuwa shida maana tayari tulikuwa watano na yeye akapata watoto wawili.

Baba alikuwa akifanya kazi serikalini na alikuwa na wadhifa kimkoa. Ukisikia Baba wale wa enzi za mwalimu Sasa yeye ndo alikuwa mmoja wao. Yaani strict to the rules hakupindisha maneno, akisema A ni A. Kwa kweli baba alikuwa ndio nguzo yangu! Rip baba alijitoa zaidi ya 100% tusome na kuhakikisha tunakuwa na maadili na nidhamu. Hakubagua Mtoto! Alinifundisha kufanya kazi kwa bidii kujituma na ucha MUNGU! alikuwa kila jpili hakosi kanisani na nyumbani habaki mtu, wote church!

Alihimiza Sana kupendana na kuwa kitu kimoja. Nikiwa na 5yrs Kuna siku walipishana maneno na huyu Mama yetu mlezi, walizozana kidogo siku ikaisha, kesho yake kukawa shwari. Mpaka wote wamefariki sikuwasikia Tena wakigombana, wala mmoja kanuna sijui haongei na mwenzie.

Yaani wakitoka room km hakuna kitu, maneno nayakuja kuyapata kwa dad's yangu mkubwa, atakwambia unajua kwa Nini shangazi alikuja mwezi wa tatu? Sijui utasikia ohooo alikuja suluhisha ugomvi Mama anataka mwanae wa kike wa kwanza apatiwe ile nyumba yetu kubwa! Khaaaa ndo naajua kumbe Kuna issue hahahaa. Baba will always be my hero! Ingawa ma mlezi kwa kweli ametulea Kama watoto wake, alifariki bado nipo chuo lkn Kama angekuwepo leo hii ningemzawadia nyumba mpyaa.

Alikaa na sisi tukiwa wadogo, nakumbuka Kuna siku nilibanwa na asthma usiku saa nane alinibeba mpaka zahanati nikatibiwa alikuwa akinipendanoo. Akipika mie ndo mwonja chumvi, chumbani kwa baba na Mama mie peke yangu ndo nilikuwa naweza tumwa hukoo! Sasa hivi nnatamani angekuwepo nimwoneshe appreciation yangu kwake!
 
Wote wana thamani sawa shida baba ndio huanza kufa
Thamani ya baba na mama,haijwahi kuwa sawa. Mama ana thamani kubwa yaani mara tatu zaidi ya baba. Mimi ni baba,ila sitashangaa kuja kuona watoto wangu wakimthamini sana mama yao na kumfanyia mema.

Suala la kufa yoyote ana kufa tu,ni muda tu ukifika.
 

Mara nyingi watoto wanawathamini mama zao lakini hawajuwi mchango wa baba ni mkubwa kiasi gani
 

Wa mama wengi huwachochea watoto kuhusu baba na kusema vibaya na kujenga chuki mtoto kumchukia baba mamawengi wabaya
 
Tatizo wanaume wengi huwa tunadhani kwamba mke wako anakuhitaji sana wewe kuliko we we unavyomuhitaji dear friends tunakosea angalia familia nyingi akifa baba mama anaishi mingi mbele lakini angalia akifa mama baba hachukui round naye anafuata.
 
Serikali pia inachangia kuwasema vibaya wakina baba . hawana mchango serikalini mfano utakuta siku ya kina mama mara haki za kina mama mara dawati la uonevu la kina mama mara tv na radio zoote kuna vipindi vya kina mama.
 
Mimi na mshua wangu tunaishi kisela kinyama. Anaweza kuniita tukagonga vyombo mbaya halafu tuka maindiana nae sana. Kesho yake asubuhi tunaombana msamaha tuenda kutoa "loku".

Mungu amuweke miaka mingi dingi yangu msela msela.
Hahahaha Kama nakufahamu vile maana hii story ya kuishi kisela mtu na dingi yako niliwahi kusimuliwa na bwanamdogo mmoja hivi
 
Ikitokea hivyo bora hata uhame mji, uwe mbali nae, kuliko kupigana vita na mzazi wako.
 
Tatizo wanaume wengi huwa tunadhani kwamba mke wako anakuhitaji sana wewe kuliko we we unavyomuhitaji dear friends tunakosea angalia familia nyingi akifa baba mama anaishi mingi mbele lakini angalia akifa mama baba hachukui round naye anafuata.
Hiyo research umeifanya kwenye mikoa mingapi??[emoji15][emoji15][emoji15]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…