Huwa kila siku natafakari umuhimu wa Baba katika maisha ya kila Familia

Huwa kila siku natafakari umuhimu wa Baba katika maisha ya kila Familia

Angekuwa baba yangu hapo nisingekuwa shule muda huo. Kuna watu wengi wenye umuhimu kwangu kumzidi yeye, mtu anayekwambia mbona unanipigia sana kwani sijui kama upo unategemea maajabu gani kwake. Hapo ushamtafuta mwaka mzima hapokei sasa jichanganye umpigie kwa namba nyingine apokee atabadili gia angani kama hivi;

Mimi: Inaita
Yeye: Anapokea
Mimi: (Salamu na maelezo kwa mkupuo maana najua hatoongea sana, hela hazihusiki kabisa)
Yeye: Kumbe ni wewe, mbona namba nyingi. Simu yangu hii ina shida
Mimi: Siku nyingi hatuongei kulikoni
Yeye: Hello! mbona sikusikii
Mimi: Wazima uko
Yeye: Hello! Hello! Naona mtandao una shida, sikusikii ntakupigia nikikaa kwenye network.

Kuna siku usanii wake nikauchoka nikamtukana we mpuuzi nini kila siku mtandao unasumbua. Kesi nikaisikia kwa aunt yangu ikiwa na nyongeza ya mashtaka kwamba simpendi na natamani afe. Kazi yake kwangu ni kunifanya nisiitwe yatima, hafai hata kunipa ushauri.
Huyo atakuwa sio baba yako halisi,itakuwa kambambikiziwa tu.
 
Exactly the same story .
Mshua wangu alitengana na bimkubwa kitambo sana Kabla ya kuzaliwa kwangu. Kusoma kwangu,kula na kuvaa ni mama mpaka nimemaliza chuo.kiukweli huwa najiuliza hata kama walitofautiana na mama basi angenionyesha ule upendo basi kama baba yangu lakini wapi .hali hiyo ya kukosa upendo wa baba imeniathiri kisaikolojia hadi sasa . Najiuliza kwanini asingenionyesha upendo hata basi wa kinafiki. Kwa kweli nikikumbuka maisha haya niliyoyapitia nasema anyway ...
Huyo atakuwa sio baba yako halisi,kabambakiziwa.Huwenda pia huko kutengana baba yako na mama,ni hiyo wewe baba yako ni mwingine.
 
Ndio maana nakwambia kuna mazee mengine akili hakuna kabisa

Yeye mwenyewe kwa utashi wake kakuleta duniani and still anakwepa kua karibu na mwanadamu aliemleta duniani yeye mwenyewe!

So strange kabisa
Ukiona hivyo,ujuwe huyo sio baba yako halisi,amebambakiziwa tu.
 
Wakati fulani nikisoma shule ya Sekondari, baba alikuja kunitembelea shuleni, nikashangaa kwa nini amekuja kwa miguu na ana mavumbi mengi miguuni?

Akanikabidhi TZS 12,000/= yani 10,000/= ya kulipia hostel na 2,000/= ya matumizi. Nikamuuliza mbona leo huna baiskeli? (mara zote alikuwa akiendesha baiskeli 40kms kuja shuleni). Akanijibu "...nimekuja kwa basi", nikaamini ni kweli!
_
Miaka mitano baadaye, nikiwa Chuo Kikuu, wakati nimerudi likizo nyumbani, nikawa nimekaa nje saa za usiku mnene, niko na baba akinipigia stori za vita za Uganda, Msumbiji nk.

Ghafla akanipigia stori iliyomkuta miaka 5 iliyopita, kwamba alikuwa na shilingi 12,000 tu ndani, akapata taarifa kuwa wanafunzi wanarudishwa kwa kutolipa hela za hostel. Akafunga safari ya baiskeli kuja shuleni kwetu (alikuwa anaanza safari zake saa 8 au 9 usiku), ili kuniletea ile pesa, safari ya kilomita 40.

Alipofika kilomita 13 baiskeli ikaharibika, "tyre tube" ya nyuma ikapasuka, ikawa haifai. Akaamua kuacha baiskeli kwa wenyeji na kuanza safari ya saa nyingi kwa mguu hadi shuleni kwetu, zaidi ya kilomita 27.

Akafika ametabasamu ana furaha mno, akanikabidhi zile pesa na akaanza safari nyingine ya kilomita 27 + 13, ananiambia alifika nyumbani kesho yake.

Usiku nilipojua safari ile ya Mzee wangu nililia sana, sikulala, ilinipasa nijitafakari juu ya huyu mtu anayeitwa BABA, ambaye yuko tayari kufa na kutokwa jasho la damu kwa ajili ya familia yake.
_
Kila mwanaume 1 anaporudi nyumbani, anaenda kuipa matumaini, familia yake, hata kama hana senti tano! Uwepo wake na tabasamu na kurudi kwake, kunainong'oneza familia "IPO KESHO....KUNA MAISHA BADO....TUNA ULINZI WA KUTOSHA. BADO LIPO TUMAINI.."
_
Hadithi ya baba yangu mzazi, inatukumbusha mwanaume anatembea na mengi sana kichwani na moyo wake, na hawezi kuyasema, kama wanaume wangelikuwa wanawaeleza wake zao namna wanavyopambana kwa ajili ya familia zao, wanawake wangelikufa kwa mshtuko.

And you know what? Baba hakuwahi kumpigia mama hii stori, hadi mimi nilipomsimulia mama.

Si ajabu ndiyo maana wanaume tunakufa mapema, maana tunauawa na mengi!
Hii story imenigusa sana, Mungu ambariki baba yako na wababa wote maana bila wababa familia hazijakamilika
 
Mzee wangu alidanja miaka karibia 30 iliyopita sijawahi mfaidi kabisa coz alidanja nikiwa mdogo .

Ila ameacha legacy ninayokula matunda yake Hadi leo

Nawaza tu angekuwepo Leo pengine angekuwa mtu mzito fulani hivi maana alikuwa kwenye radar nzuri ya kutusua msomi mwenye vipaji lukuki.kichwa hasa .

Wadau nikikutana nao wananiambia aisee wewe dogo mshua wako angekuwepo leo ungekula Bata ,kuku,Bata mzinga,Bata bikini[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Yule jamaa alikuwa mtu POA raia walikuwa wanampenda Sana [emoji1]

R.I.P mzee wangu sijawahi kukusahau kamwe
 
Shukuru Mungu kama Ulizaliwa na baba wa aina hiyo! Siyo watoto wote wana historia kama hizo na baba zao!

Sidhani kama kuna mtu anayemchukia baba yake bila sababu! Ukikuta mtu anamchukia baba yake tafuta kujua chanzo!

Na mara nyingi mtoto akimchukia baba yake lawama zote hutupiwa mama! Wamama wengi wana wakati mgumu sana!
 
Huyo atakuwa sio baba yako halisi,itakuwa kambambikiziwa tu.
Unamaanisha ndugu zake na wazazi wake ni wajinga ambao naishi nao. Yani ndugu zake wote nalala kwao wakati yeye kwake sipakumbuki, babu yangu alifia mikononi mwangu, bibi yangu ananipenda kuliko maelezo (naamini huwa anafanya hivi kujaribu kufidia makosa ya mwanae, hadi ada alikuwa ananichangia akidai ni baba katoa kumbe ni mwenyewe). Hawa wote ni wapuuzi?

Babu na bibi wasingenipa sehemu yake ya urithi badala yake wakati wanajua mimi sio mwanae. Nishakuwa main topic kwenye vikao vya familia. Unajua ile familia ya heshima akitokea mmoja akakengeuka, na kila familia yupo mtu huyu.

Mnasemaga hivihivi tukitoboa maishani mnakuja kutia huruma. Tukiwa vibaka mnapeta na kujifanya mlijua hatuwezi lolote ndio maana mkatuacha.
 
Mimi binafsi hunambi kitu kwa Baba yangu asee, Japo sipo naye tena ila namkubali sana hadi nitakapoingia kaburini. Missing you Daddy [emoji41]
 
Exactly the same story .
Mshua wangu alitengana na bimkubwa kitambo sana Kabla ya kuzaliwa kwangu. Kusoma kwangu,kula na kuvaa ni mama mpaka nimemaliza chuo.kiukweli huwa najiuliza hata kama walitofautiana na mama basi angenionyesha ule upendo basi kama baba yangu lakini wapi .hali hiyo ya kukosa upendo wa baba imeniathiri kisaikolojia hadi sasa . Najiuliza kwanini asingenionyesha upendo hata basi wa kinafiki. Kwa kweli nikikumbuka maisha haya niliyoyapitia nasema anyway ...
Unaweza kukuta kutengana kwao kulitokana na mama yako kuuza mechi. Kwa vile ulikuwa mdogo na DNA haikuwepo basi akadhani pengine wewe si zao lako. Akaachia jumla. Ni vyema ukajaribu kuanzisha uhusiano naye!
 
Yaani nikijiangalia Mimi ninavyotegemewa kwa kila kiti harafu watoto wakishakuwa watu wazima watamjali zaidi mama yao
Investment zaidi kwa mabinti, hutajuta uzeeni. Wavulana lazima waegemee upande wa mama zao. Hii laana maana hata sie tulielemea upande wa mama zetu.
 
Yaani unaniita dogo wakati ninaweza kumstarehesha bimkubwa wako[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]Nina watoto unaoweza kutafutiana nao wanawake
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] aise, angetakiwa asemee tu mzee shikamooo
 
Back
Top Bottom