Huwa kila siku natafakari umuhimu wa Baba katika maisha ya kila Familia

Huwa kila siku natafakari umuhimu wa Baba katika maisha ya kila Familia

Dingi yangu nilikua namuonaga wa maana nilipokua mdogo ila nimekuja kua mtu mzima nikafikiria his life decision skills,ninaona ni wa hovyo sana so far.....

Kupata wazazi au mzazi generally ni vizuri ila wazazi au mzazi mwenye akili ya intelect is something else entirely
Alikuwa akikunyanyasa? Hakukupenda? Hakukuhudumia kama baba?
 
Nna shangaa Sana Sasa hivi sifa zote anapewa mwanamke, Baba kasahaulika! Mama yangu mzazi alifariki nikiwa km na 3yrs unfortunately siijui hata saiti yake na Sina kumbukumbu yoyote na Mama yangu mpenzi lkn nnaona picha zake na sisi tulipokuwa wadogo! MUNGU ailaze roho yake mahala pema peponi Amina! Baba alioa tena Mama yetu mlezi alitulea vizuri tuu hakuwa shida maana tayari tulikuwa watano na yeye akapata watoto wawili.
Baba alikuwa akifanya kazi serikalini na alikuwa na wadhifa kimkoa. Ukisikia Baba wale wa enzi za mwalimu Sasa yeye ndo alikuwa mmoja wao. Yaani strict to the rules hakupindisha maneno, akisema A ni A. Kwa kweli baba alikuwa ndio nguzo yangu! Rip baba alijitoa zaidi ya 100% tusome na kuhakikisha tunakuwa na maadili na nidhamu. Hakubagua Mtoto! Alinifundisha kufanya kazi kwa bidii kujituma na ucha MUNGU! alikuwa kila jpili hakosi kanisani na nyumbani habaki mtu, wote church! Alihimiza Sana kupendana na kuwa kitu kimoja. Nikiwa na 5yrs Kuna siku walipishana maneno na huyu Mama yetu mlezi, walizozana kidogo siku ikaisha, kesho yake kukawa shwari. Mpaka wote wamefariki sikuwasikia Tena wakigombana, wala mmoja kanuna sijui haongei na mwenzie. Yaani wakitoka room km hakuna kitu, maneno nayakuja kuyapata kwa dad's yangu mkubwa, atakwambia unajua kwa Nini shangazi alikuja mwezi wa tatu? Sijui utasikia ohooo alikuja suluhisha ugomvi Mama anataka mwanae wa kike wa kwanza apatiwe ile nyumba yetu kubwa! Khaaaa ndo naajua kumbe Kuna issue hahahaa. Baba will always be my hero! Ingawa ma mlezi kwa kweli ametulea Kama watoto wake, alifariki bado nipo chuo lkn Kama angekuwepo leo hii ningemzawadia nyumba mpyaa. Alikaa na sisi tukiwa wadogo, nakumbuka Kuna siku nilibanwa na asthma usiku saa nane alinibeba mpaka zahanati nikatibiwa alikuwa akinipendanoo. Akipika mie ndo mwonja chumvi, chumbani kwa baba na Mama mie peke yangu ndo nilikuwa naweza tumwa hukoo! Sasa hivi nnatamani angekuwepo nimwoneshe appreciation yangu kwake!
Pole sana, ukipata baba mwenye akili ni zawadi.
 
Thamani ya baba na mama,haijwahi kuwa sawa. Mama ana thamani kubwa yaani mara tatu zaidi ya baba. Mimi ni baba,ila sitashangaa kuja kuona watoto wangu wakimthamini sana mama yao na kumfanyia mema.

Suala la kufa yoyote ana kufa tu,ni muda tu ukifika.
Ni mtazamo wako wewe binafsi, sio akina baba wote. Hongera!
 
Mama zetu wamekuwa na tabia ya kupandikiza chuki na barrier kati ya watoto na baba zao, lakini ukiwa mtu mzima ndio unaweza kuelewa kuwa baba ni kama bulldozer/caterpillar. Kazi yake ni kutengeneza barabara, likishamaliza kutengeneza haliruhusiwi kutumia hiyo barabara.

I loved my dad, I still do coz alikuwa sio mtu wa kuyumbishwa, misimamo thabiti na alitimiza majukumu yake ya baba kwa watoto wake. Spent his last days with me, had that privilege to nurse him so I have no regrets.
 
Niliwah lala stendi nyegezi na baba angu ili kesho yake alfajir niende chuo na nilkuwa mkubwa tu lakin alipenda nisindikiza ile usiku nilkuwa namuwazia sana,kwann huyu mzee anateseka hv kwa ajiri yangu.

Niliwah lazwa hospital siku 4,sku zote alilala kwenye kiti pemben mwa kitanda changu,nikawa najiuliza mbona hawabadilishan na yeye akapumzika akalala nyumban,maana nyumban kulkuwa na ndugu wengine ambao wangeweza kuniangalia ili kumsaidia
So nini kilifuata? Hebu andika taarifa kama msomi kaka!
 
Sijawahi kupendwa na mwanaume zaidi baba yangu! Japo amekufa pengo lake ni kubwa mno. Rest easy my father. Na hongera kwa wababa wote wanaotimiza majukumu yao
 
Nah

He was just a serially bad decision maker in his lifetime..

Effects of those bad decisions are on him up to this day
Is He alive or dead? If He serves you as his son, so how does his bad decision making hinder you? Don't you see that it was non of your business, and never interfered your upbringing? Play your part as a son, leave upon him what is non of your business or control.
 
Nitamkumbuka sana kwa "emotions" zipi?

Na uoga wa kumkumbuka sana ndio kunifanye niseme uongo about his life?

No

Listen,kama maisha ulijifelisha kwa kutotumia ubongo wako binafsi sawasawa ,sisi wanadamu tunaokuangalia we will give an actual accounting of your failures,we cant lie!

Huo uoga mwingine uliobeba ni wako ndugu yangu,we are different human beings..that nonsense dont bother me....
Sawa brother

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Natamani huu uzi upate sticky, na wachangiaji wapate kutoa pongezi kwa baba zao.
Pia itasaidia kuwatia moyo wanaume wanaopambana kuhudumia familia zao katika zama hizi za 'politically corrected gender roles ", ili hali hata wake zao hawawashukuru.
 
Hii story sio mpya maskioni mwangu,umeicopy sehemu even so hongera kwa wababa wote wanaoitendea haki nafasi ya Baba
 
Ndiyo kwanini sasa wawajaze sumu
Huweza wakawa na sababu na kadhalika ujinga na chuki za kihayawani. Hakuna sehemu ambayo inahimiza mtu kulipa ubaya kwa ubaya,haya ni matatizo ya akil na hawaa za nafsi bali ni ujinga.

Mathalani hivi wewe leo mzazi mwenzako akikufanyia ubaya,lazima umjaze sumu mwanao ?
 
Vitu kama sherehe ya siku ya kuzaliwa huwagusa sana akina mama. Mimi naiona km inanipotezea muda wa kurafuta pesa. Hata weekend, nawaza kazi ambazo hazijaisha na deadline imekaribia. Naweza kutoa kompyuta ili nizipunguze. Wenyewe wakiona hivyo, wanafikiri siwajali!
Jambo moja ni kuwa wababa hatupendi sifa. Hebu jaribu kuwa uitwe mbele vile waitwavyo wanawake kwenye harusi kisha uvalishwe na mwanao kitambaa cha suruali huwa naona shobo tu ila kwa mwanamke anapenda sana kufanyiwa kitu hata kiwe kidogo ila sisi wababa labda ukitaka kinistua uje na funguo za gari jipya au trekta la kulimia au kitu chochote atakacholia bata aka mapene hufurahi sana.

Mama unaweza kumwimbia mashairi yote akafurahi sana hata usipompa chochote wala baba asione shida kabisa.
 
Thamani ya baba na mama,haijwahi kuwa sawa. Mama ana thamani kubwa yaani mara tatu zaidi ya baba. Mimi ni baba,ila sitashangaa kuja kuona watoto wangu wakimthamini sana mama yao na kumfanyia mema.

Suala la kufa yoyote ana kufa tu,ni muda tu ukifika.
Ulichosema ni sahihi, lakini kwa baadhi ya watu baba anathamani kubwa sana kuliko mama,,,,binafsi leo mama yupo na Baba hayupo alishafariki...lakini nafasi ya baba kwangu ni kubwa mno kuliko hata mama...hii ni kwa sababu ya ni jinsi gani kila mmoja alivyokuwa anatimiza majukumu yake kwangu. Watoto wengi wanawapenda mama zao kwa sababu mama wengi huwajibika sana kwa watoto wao na baba walio wengi hukwepa majukumu.....lakini si wote kwani kuna akina baba wanawajibika ipasavyo
 
Back
Top Bottom