Huwa kila siku natafakari umuhimu wa Baba katika maisha ya kila Familia

Huwa kila siku natafakari umuhimu wa Baba katika maisha ya kila Familia

Hahahaaaa

Mzee unaishi kwa wasiwasi sana aiseee

Wasiwasi na upendo wa watoto which is very very hard to determine na kutegemea...

Unaishi kwa utegemezi sana hadi wa emotions,jaribu kukata human dependences as minimum as you can

Watoto timiza majukumu yako kadiri inavyotakiwa,upendo mzee ni very subjective,huwezi pangia wanadamu upendo wapende wapi

Treat every human being decently and respect,iwe watoto au watu wazima,upendo ni parameter huna control nayo

Otherwise utakuja kua na dissapointments za ajabu hapa duniani
Tatizo ni malezi yako ila ukiwa mtu mzima utanikumbuka. Sisemi mwanaume unaweza kuwa tegemezi kwa watoto! No ila unahitaji kuwa na watoto karibu uzeeni kama kumtuma aende bank kukuchukulia hela yako. Utakuwa wa ajabu unastaafu bila kujipanga kiuchumi ukategemea misaada.
 
Wanaume hatupendi kutelekeza watoto ila mazingira ya uliyezaa naye yanaweza kukufanya uwe mbali nae..... Mfano kuna demu alizaa na mshkaji afu akamuwekea sumu mshkaji ikamdhuru baadae akabainika akamfukuza demu akaondoka na mtoto hawajaonana hadi leo mwaka wa 7. Sasa hapo utakuta hilo demu anamjaza ujinga mtoto
 
Kina baba huwa wanapambana sana muda mwngine kuhatarisha maisha yao bila kujijali wao isipokua ni kwaajili ya familia na wanayafanya hayo bila kuongeaongea au kutaka kujulikana umuhimu wao ,, muda mwngne hata wale anao watafutia huwa hawauoni umuhimu wake
 
Uko sahihi mm ninawatoto wakubwa wanne,mkubwa kabisa wa kiume ana 29 yrs huyo hana time na Mimi ila anaemfuatia wakike ana 26yrs huyo ananipenda Sana baba yake
Faza shikamoo
 
Baba ame'hustle hadi kutufikisha ukubwani
Na tunashukuru kwa hilo

shida za Baba:Mkali sana hadi leo.,hata kama unamtendea jema ukikosea kidogo ni shida kubwa

wababa msiwe wakali sana.,
 
Sisi alitufukuza usiku wa mbaramwezi nakumbuka kulikuwa na umande tukapitia uwanja wa michezo ulikuwa nyuma kidogo ya nyumba. Mama alikuwa anaogopa mbwa hivo hatukupitia kwa nyumba za majirani, mzee ana kacheo flani hakuna jirani angeweza tuhifadhi. Sikumbuki tulilala wapi nilikuwa mdogo bado.

Kumbukumbu yangu nyingine na mzee ni pale amekutana na mimi bila kutarajia wilaya nyingine giza linaanza ingia hivi amelewa anaongea lugha na sauti tofauti kidogo, aisee sikumtambua. Alinishikashika na kuniongelesha nilikuwa na binamu, nilipofika kwa mama nikamshtaki mzee kwamba kuna mwanaume nimekutana naye kanishikashika. Kipindi utotoni tunapigwa marufuku kuongea na strangers.
Una bahati dingi angekula tunda kimasihara
Lakn pia kama ilivyo kuna baba wabaya pia wapo wamama wabaya vle vle
 
Kuna wakati Mungu anatuepusha wanaume na mengi kutokana na watu wanaotutegemea.
 
Point.
Shukuru Mungu kama Ulizaliwa na baba wa aina hiyo! Siyo watoto wote wana historia kama hizo na baba zao!

Sidhani kama kuna mtu anayemchukia baba yake bila sababu! Ukikuta mtu anamchukia baba yake tafuta kujua chanzo!

Na mara nyingi mtoto akimchukia baba yake lawama zote hutupiwa mama! Wamama wengi wana wakati mgumu sana!
 
Wakati fulani nikisoma shule ya Sekondari, baba alikuja kunitembelea shuleni, nikashangaa kwa nini amekuja kwa miguu na ana mavumbi mengi miguuni?

Akanikabidhi TZS 12,000/= yani 10,000/= ya kulipia hostel na 2,000/= ya matumizi. Nikamuuliza mbona leo huna baiskeli? (mara zote alikuwa akiendesha baiskeli 40kms kuja shuleni). Akanijibu "...nimekuja kwa basi", nikaamini ni kweli!
_
Miaka mitano baadaye, nikiwa Chuo Kikuu, wakati nimerudi likizo nyumbani, nikawa nimekaa nje saa za usiku mnene, niko na baba akinipigia stori za vita za Uganda, Msumbiji nk.

Ghafla akanipigia stori iliyomkuta miaka 5 iliyopita, kwamba alikuwa na shilingi 12,000 tu ndani, akapata taarifa kuwa wanafunzi wanarudishwa kwa kutolipa hela za hostel. Akafunga safari ya baiskeli kuja shuleni kwetu (alikuwa anaanza safari zake saa 8 au 9 usiku), ili kuniletea ile pesa, safari ya kilomita 40.

Alipofika kilomita 13 baiskeli ikaharibika, "tyre tube" ya nyuma ikapasuka, ikawa haifai. Akaamua kuacha baiskeli kwa wenyeji na kuanza safari ya saa nyingi kwa mguu hadi shuleni kwetu, zaidi ya kilomita 27.

Akafika ametabasamu ana furaha mno, akanikabidhi zile pesa na akaanza safari nyingine ya kilomita 27 + 13, ananiambia alifika nyumbani kesho yake.

Usiku nilipojua safari ile ya Mzee wangu nililia sana, sikulala, ilinipasa nijitafakari juu ya huyu mtu anayeitwa BABA, ambaye yuko tayari kufa na kutokwa jasho la damu kwa ajili ya familia yake.
_
Kila mwanaume 1 anaporudi nyumbani, anaenda kuipa matumaini, familia yake, hata kama hana senti tano! Uwepo wake na tabasamu na kurudi kwake, kunainong'oneza familia "IPO KESHO....KUNA MAISHA BADO....TUNA ULINZI WA KUTOSHA. BADO LIPO TUMAINI.."
_
Hadithi ya baba yangu mzazi, inatukumbusha mwanaume anatembea na mengi sana kichwani na moyo wake, na hawezi kuyasema, kama wanaume wangelikuwa wanawaeleza wake zao namna wanavyopambana kwa ajili ya familia zao, wanawake wangelikufa kwa mshtuko.

And you know what? Baba hakuwahi kumpigia mama hii stori, hadi mimi nilipomsimulia mama.

Si ajabu ndiyo maana wanaume tunakufa mapema, maana tunauawa na mengi!
Mkuu mkumbuke aliyoitoa hii kisa siku za nyuma hukoooo![emoji16][emoji16][emoji16]
 
Angekuwa baba yangu hapo nisingekuwa shule muda huo. Kuna watu wengi wenye umuhimu kwangu kumzidi yeye, mtu anayekwambia mbona unanipigia sana kwani sijui kama upo unategemea maajabu gani kwake. Hapo ushamtafuta mwaka mzima hapokei sasa jichanganye umpigie kwa namba nyingine apokee atabadili gia angani kama hivi;

Mimi: Inaita
Yeye: Anapokea
Mimi: (Salamu na maelezo kwa mkupuo maana najua hatoongea sana, hela hazihusiki kabisa)
Yeye: Kumbe ni wewe, mbona namba nyingi. Simu yangu hii ina shida
Mimi: Siku nyingi hatuongei kulikoni
Yeye: Hello! mbona sikusikii
Mimi: Wazima uko
Yeye: Hello! Hello! Naona mtandao una shida, sikusikii ntakupigia nikikaa kwenye network.

Kuna siku usanii wake nikauchoka nikamtukana we mpuuzi nini kila siku mtandao unasumbua. Kesi nikaisikia kwa aunt yangu ikiwa na nyongeza ya mashtaka kwamba simpendi na natamani afe. Kazi yake kwangu ni kunifanya nisiitwe yatima, hafai hata kunipa ushauri.
Kwa tabia yako ya kukosa huruma kwa matumizi yako ya hovyo na kutunga!Ulitaka mzee wako akuchekee tu?.
 
Jambo moja ni kuwa wababa hatupendi sifa. Hebu jaribu kuwa uitwe mbele vile waitwavyo wanawake kwenye harusi kisha uvalishwe na mwanao kitambaa cha suruali huwa naona shobo tu ila kwa mwanamke anapenda sana kufanyiwa kitu hata kiwe kidogo ila sisi wababa labda ukitaka kinistua uje na funguo za gari jipya au trekta la kulimia au kitu chochote atakacholia bata aka mapene hufurahi sana.

Mama unaweza kumwimbia mashairi yote akafurahi sana hata usipompa chochote wala baba asione shida kabisa.
 
We jamaa bhna

Tumekua kwenye malezi tofauti

Nini usichoelewa sasa
**** vitu vinashangaza sana hapa haijalishi malezi bali ni ujinga na kukosa maarifa.

Kuna uhusiano gani kati ya malezi na kujua hadhi ya mama kuwa ni ya juu kuzidi ya baba zaidi ya hizo sababu mbili nilizo zitaja hapo juu ?
 
Ushuhuda wangu mwenyewe.
Mwaka huu nilipata ajali nikawa wa ndani tuu hakuna kutoka.
Ila familia haikuwa wah lala njaa.
Wife akija halisi tumizi.
 
Kwa tabia yako ya kukosa huruma kwa matumizi yako ya hovyo na kutunga!Ulitaka mzee wako akuchekee tu?.
Matumizi ya kutunga ndio yakoje? Kutunga mashairi ama kitu gani, mimi sio muimba singeli kama wewe.
 
Niliwah lala stendi nyegezi na baba angu ili kesho yake alfajir niende chuo na nilkuwa mkubwa tu lakin alipenda nisindikiza ile usiku nilkuwa namuwazia sana,kwann huyu mzee anateseka hv kwa ajiri yangu.

Niliwah lazwa hospital siku 4,sku zote alilala kwenye kiti pemben mwa kitanda changu,nikawa najiuliza mbona hawabadilishan na yeye akapumzika akalala nyumban,maana nyumban kulkuwa na ndugu wengine ambao wangeweza kuniangalia ili kumsaidia
 
Back
Top Bottom