Huwa sielewi watu wanatoa wapi Uhalali wa kumfananisha Mwanamuziki Fally Ipupa na Feregola!

Dah mkuu ulikua wapi mda wote? Tulipigiwa sana kelele na hawa wasioijui rhumba vizuri.
 
Unaweza ukawa unamjua ila hufatilii mziki wake, inshort hujui lolote kuhusu ferre gola we endelea kusikiliza bakanja.
Namuwekea hapa live concert ya wenge ya mwaka 1996, ferre gola akiimba mwanzo mwisho wakati huo fally hata hajaingia Quartier Latin yupo zake bendi ya mtaani iliyoitwa Talent Latent , wakati huo huko Quartier Latin kulikuwa na wakali animators akina Bivens Rappason,Suzuki Luzubu,Dolce Parabolique Somono n.k. wakati huo 1999 miaka mitatu mbele Fally ndio anapewa nafasi ya kuimba kidogo sana lakini Ferre anapewa concert aimbe dakika 45+ akiwa Wenge BCBG chini ya Jb na Werrason.

Fally kajiunga Quartier Latin mwaka 1999 wakati huo tayari Ferre ni mwanamuziki mkubwa ambapo mwaka 2005 ndio na yeye akajiunga na QL International ya mwamba Mopao Mokonzi, Ferre alidumu mwaka mmoja tu katika band ya koffi lakini alifanya makubwa sana ndani ya muda huo, ukitaka kuamini kasikilize Skol Longitima au katika album ya Danger de mort, wimbo kama "Silivi"na "Insecticide humo utapata balaa la Ferre.
 

Attachments

Heshima yako mkuu, aisee wewe kweli unaijua rhumba kuna vitu vingi nimejifunza kupitia comments zako, barikiwa.
 
Kwa faida ya wengi hizi ni albums kadhaa alizoshiriki Ferre Gola le padre akiwa solo, akiwa na wenge na akiwa na Quartier Latin.

Akiwa na Wenge
  • Force D’Intervention Rapide (1998)
  • Solola Bien (1999)
  • Terrain Eza Miné (2000)
  • Kibuisa Mpimpa (2001)
  • À La Queue Leu-Leu (2002)
  • Tindika Lokito (2003)
Akiwa na Koffi (QLI)
  • Boma Nga N’Elengi (2005)
  • Danger de Mort (2006)

Akiwa na bendi yake yeye na kina Bill Clinton hapa kuna album moja ya mwaka 2004.
  • Miracles (2004)

Akiwa kama solo artist mpaka sasa ametoa albums zifuatazo

  • Sens Interdit (2006)
  • Qui Est Derrière Toi (2009)
  • Avant Goût – EP (2011)
  • Boîte Noire (2013)
  • Dérangement – EP (2014)
  • QQJD (2017)
  • Dynastie (2022)
Kwa kuongezea tu watu wengi walimjua Ferre katika hiyo album yao ya mwaka 2004 maarufu kama Miracle kwa sababu ndani yake ndio kuna kibao cha rhumba kikali kuliko vyote Congo mpaka sasa ambacho ni 100 kilos na wala hiyo nyimbo haikuwa imebeba album.
Hiyo album yake ya Dynastie inaendelea maana ina volume 1 mpaka sasa zimefika vol 3 watu tunakula tu rhumba.

Mwisho niseme tu kuwa katika Rhumba ya muziki wa Congo basi hakuna kama Ferre. Kwa rhumba kali ukiwaweka Fally na Heritier Watanabe basi Wata anashinda saa 4 asubuhi.
 
Mkuu basi hizo albums wanazijua basi hawa mashabiki maandazi wa fally ipupa😂😂 labda wakazitafute sasa hivi, ngoma ya ferre gola wanayoijua ni 100kilos basi.
 
Uzi ufungwe sasa, mpaka sasa ferre gola 5 fally ipupa 0. Mtani wa Taifa kamaliza kila kitu😂😂
Asante mkuu, nimesikitika mtoa mada mwenyewe kaishia kupigwa ban sijui kaharibu nini tena kwa pilato mod, sie acha tuendelee kuburudika na rhumba za mkali Ferre.

Naweka nyimbo 5 ninazozipenda zaidi
1. 100 kilos
2. Kinshasa
3. Zazzou
4. Eclipse
5. Kamasutra
 

Attachments

Mkuu basi hizo albums wanazijua basi hawa mashabiki maandazi wa fally ipupa😂😂 labda wakazitafute sasa hivi, ngoma ya ferre gola wanayoijua ni 100kilos basi.
Wao wanaujua 100 kilos tu wakati now tuko kwenye album ya Dynastie Vol III. Sisi hatumrate Ferre kutokana na wimbo mmoja wa Rhumba bali ni kwa mfululizo wa nyimbo zake kuanzia alipoanza muziki hadi sasa.
 
Reactions: A43
Mkuu hizi ninazo labda hii zazzou ndio nimeidownload sasa hivi naisikiliza ni hatari, nilikua nasikiliza sillivi aisee ni bonge la ngoma. Mkuu wewe ni noma✌, Kuhusu kupigwa ban kwa mleta mada haituhusu nahisi na hii kumlinganisha ferre gola na fally ipupa imewakasirisha mods😂😂
 
Wao wanaujua 100 kilos tu wakati now tuko kwenye album ya Dynastie Vol III. Sisi hatumrate Ferre kutokana na wimbo mmoja wa Rhumba bali ni kwa mfululizo wa nyimbo zake kuanzia alipoanza muziki hadi sasa.
Kweli mkuu na hiyo wanaijua kwasababu inapigwa sana bar bila hivyo wasingeijua naamini.
 
Muziki huenda na vionjo na hisia za mtu binafsi. Unaweza ukauona huu mzuri kwako, mwenzako akapenda mwingine ambao wewe wala haukuingii kabisa. Ni sawa sawa na mwanamke vile. kwahiyo usishangae, watu wote hatuwezi kupenda kitu hiki kwa vile tu wewe umekipenda. Learn to appreciate diversity
 
Fally Ipupa 🔥🔥🔥,Ila Jamaa kwenye show zake ananishangazaga sana ujue Hanaga shobo na pisi Kali hataa....anacheza kwa kutulia afu kwa heshimaa sana.

Kuna Moja Hamisa alimfuaata staging,Fally hata hakubabaikaa....yaan Mimi siwezi kujizuia kabisa kwa pisi Kali.
 
Anakutana na Pisi Kali machotara Paris ulaya usa ndo ashoboke na wabongo.
Pili yupo kazin
 
Wao wanaujua 100 kilos tu wakati now tuko kwenye album ya Dynastie Vol III. Sisi hatumrate Ferre kutokana na wimbo mmoja wa Rhumba bali ni kwa mfululizo wa nyimbo zake kuanzia alipoanza muziki hadi sasa.
Ferre gola atabak kuwa juu
 
Baba yangu mzaz, , kaka na wife... Wamekuwa wakiniona naskilza sn ngoma za akna Fally ipupa na ferre gola wakatokea kupenda ngoma zao zaid na zaid


Lakin katka wawili hawa kla mtu kw nafas yake alikiri kuwa Ferre gola n zaid ya Fally ipupa sio kwny Sebene sio kwny rhumba


Yaan hta wana kitaa nikisikilza sn wanawahi kujua ahaa hiz ngoma n Fally lakin kadri muda unazd kwenda wanasema na huyu n nan mbona ngoma zke n kali zaid. Wakimfatilia tu wamekwishaaaaa wanabak kusema Fally haoni ndan kw huyu jamaa


[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji41][emoji41][emoji41][emoji41][emoji41][emoji41] Ferre gola le padre tge best of the best ni Copy ya papa wemba na zaid anajua balaaa sio live band sio masebene sio rhumba sio takataka gan sjui
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…