Huwa sielewi watu wanatoa wapi Uhalali wa kumfananisha Mwanamuziki Fally Ipupa na Feregola!

Huwa sielewi watu wanatoa wapi Uhalali wa kumfananisha Mwanamuziki Fally Ipupa na Feregola!

Fere Golla nyimbo maarufu na nzuri ni hizo 2 tu (100 Kilos & Kamasutra) lakini Fally Ipupa nyimbo zote ni hatari na nusu!.


Uzuri wa fally ipupa nyimbo za taratibu na sebene ni gwiji
Carte Rose isikie tu
 
Kwa utunzi wa mashairi gola yuko mbali sana kwa fally ni kama kiba na mond
 
Wewe weka 100 Kilos hapo isikie vizuri yaan vyumba vikishajaa kichwani alafu uwekewe hio Ngoma hapatoshi

Mkuu kwahiyo hiyo 100 kilos mpaka Vyombo vijae kichwani ndo ionekane nzuri?


Sasa hapo huoni kama MAYDAY,ALLIANCE,MARIA,ASSOCIE,LIPUTA & OGARSY zitakuwa zinakuonea?
 
Nsikuchoshe na Usinchoshe,tusichoshane!


Hivi huwa mko Serious au huwa mnatania?,yaani Mwanamuziki Fally Ipupa mnamfananisha na Fere Golla?

Sijajua aliyeanzisha huu mpambano kama yuko timamu kichwani.


Koffi olomide amewahi kukaliliwa akisema "Moja kati ya waimbaji na wana jumuia wangu wa bendi ya QUARTIER LATIN ambao sitoweza kuwasahau ni Fally Ipupa,huyu mtu amebarikiwa kipaji cha aina yake katika muziki,bila shaka ukimtoa Marehemu Papa Wemba na mimi,basi atakuwa anafuata yeye"

Kwa maneno hayo ya Mkongwe na Gwiji la muziki wa Dansi na Rhumba kutoka Africa bila shaka Fally Ipupa ni Habari nyingine kabisa!.Vijana huyu Fally Ipupa uenda mtakuwa mmejua juzi tu baada ya kutoa wimbo wa Bakandja,Maria na Mayday!.

Lakini mimi mkongwe na wakongwe wenzangu tunaomfahamu Fally Ipupa toka Enzo hizo akiwa Stage Show na Rapa wa Koffi Olomide kutoka bendi ya QUARTIER LATIN wala hatushangai namna alivyo hatari!


Vijana niwapendekezee tu,kama humfahamu Fally Ipupa hebu nendeni karudieni show aliyoifanya Dar es salaam mwaka 2009 ndo mtaelewa ni mtu wa aina gani!(Nendeni YouTube huko mtaikuta hii show)

Kwenye ile show walipanda wasanii wenu mnaowaaminia Amini & Barnaba wakaimba wimbo unaoitwa KIDIAMFUA,aiseee nilicheka sana maana wale wasanii wenu ni kama walikuwa wanaigiza siyo kuimba😂,hapa ndipo nilijua hakuna msanii kitoka Tanzania anayejua kuimba bali huwa ni wababaishaji tu!


FALLY IPUPA acheni kabisa kumlinganisha na watoto wadogo katika muziki!
Wadanganye wajinga wasiojua Rhumba , Fally hampati Ferre hata kwa namna gani , Kwanza Fally ana style moja tu ya kuimba kiasi ambacho amekwisha chuja vibaya sana , ferre gola ni mtaalam wa sauti na anaweza kuimba sauti ya mwanamuziki yeyote unayemjua dunia , mpangilio wa Rhumba ya Ferre gola ni wa kipekee , huyu ni fundi hasa wa Rhumba
 
Huu mpambano nataka nishije Kipaza sauti niingie nacho kiitaani kuwauliza wananzengo!,Lazima mshindi apatikane!
 
Wadanganye wajinga wasiojua Rhumba , Fally hampati Ferre hata kwa namna gani , Kwanza Fally ana style moja tu ya kuimba kiasi ambacho amekwisha chuja vibaya sana , ferre gola ni mtaalam wa sauti na anaweza kuimba sauti ya mwanamuziki yeyote unayemjua dunia , mpangilio wa Rhumba ya Ferre gola ni wa kipekee , huyu ni fundi hasa wa Rhumba


Wewe utakuwa na matatizo ya kiakili siyo Bure,yaani umfananishe mwanamuziki bora wa kongo kwa miaka 15 mfululizo na huo uchafu?
 
Are U serious?

Hebu weka mashahiri ya wimbo wa Fere Golla hapa halafu na mimi niweke ya Fally Ipupa halafu tuyatafisiri tuone nani zaidi!
Ndo iko hivo mkuu utakataa lakini ndo ukweli fally unampenda kutokana na ile amsha amsha yake ila gola anaroom yake na kina madilu huko
 
Back
Top Bottom