Mtani wa Taifa
JF-Expert Member
- Aug 2, 2023
- 953
- 3,318
Dynastie vol 1 the wewe weka album yoyote ya Fally tuone.Hebu nitajie album ya Fere Golla ambayo inaweza kukompiti na album ya Fally Ipupa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Dynastie vol 1 the wewe weka album yoyote ya Fally tuone.Hebu nitajie album ya Fere Golla ambayo inaweza kukompiti na album ya Fally Ipupa
Hebu tutajie nyimbo 10 za ferre ulizosikiliza tuone kama kweli unamjua ferre le padre.Hakuna wimbo hata mmoja wa Fere Golla ambao sijasikiliza,ninapokwambia ni mwanamuziki wa kawaida ambaye hafai kulinganishwa na Fally Ipupa Namaanisha!
Semeni tuwashindanishe kwenye nini??Kujulikana, kuuza havihusiani na uwezo binafsi. Kuna kuimba muziki, biashara na kismati.
Note, si kwamba Fally hajui ila ukiwashindanisha, Ferre Gola ni moto
Ninmegundua wewe hujui muziki wa Rhumba ni nini na wakali wao sasa tulia nikueleze kwa ufupi sana.Hizi ndizo nyimbo mnazojidai nazo!
1.Vita iman
2.100 kilos
3.Kamasutra
Tofauti na hapo hakuna kitu!,Sasa msanii wenu mwenye singo 3 tu unawezaje kumlingamisha na msanii mwenye singo zaidi ya 100 halafu zote KALI?
Ninmegundua wewe hujui muziki wa Rhumba ni nini na wakali wao sasa tulia nikueleze kwa ufupi sana.
Kwa kizazi cha tatu cha muziki ambacho kinajumuisha hao kina fally na ferre basi upande wa rhumba mkali ni ferre then wanafuata kina watanabe n.k.
Fally anachanganya miondoko kwenye rhumba yupo, bolingo yupo, afro pop yupo na huko kote kuna wakali wake.
Unataka kuniambiaFelle na Fally wanaimba fani mbili tofauti fally anapiga sebene ferre anapiga rhumba
Watu tunamjua huyo Felle Gola kabla hata hajawa na band pumbavuMkuu wengi hawamjui ferre gola ndio maana hawalitambui hili.
Me nakutajia moja tu ambayo we huijui inaitwa Kinshasa itafute isikilizeHivi wewe unaijua Rhumba?,hebu nitajie nyimbo moja ya Fally Ambayo ni Rhumba
Ninmegundua wewe hujui muziki wa Rhumba ni nini na wakali wao sasa tulia nikueleze kwa ufupi sana.
Kwa kizazi cha tano cha muziki wa Congo ambacho kinajumuisha hao kina fally na ferre basi upande wa rhumba mkali ni ferre then wanafuata kina watanabe n.k.
Fally anachanganya miondoko kwenye rhumba yupo, bolingo yupo, afro pop yupo na huko kote kuna wakali wake.
Tunazungumzia rhumba mzee au umerogwa, huwezi kumshindanisha kwa kila kitu Ferre na Fally kwa sababu wanatofautiana sana kwenye vingi ila katika rhumba hakuna kama Ferre sio tu huyo Fally bali wote kwa kizazi chake. Hizo genre zingine Ferre wala haimbi.Semeni tuwashindanishe kwenye nini??
Kama ni kufanya vizuri kibiashara ferre Gola hagusi hata chembe!
Album ya Formule 7 Leo imefikisha streams milion 45 Spotify hakuna album yoyote ya rhumba Ina hizo namba tangu kuumbwa Kwa ulimwengu huu .
Unaposema tuwashindanishe kuimba unamaanisha nini ?
Kumuona msanii anajua kuimba ni kitu SUBJECTIVE. Unaemuona hajui kuimba Kwa wengine anajua kuimba!
Bibi kidude kwako wewe labda ulikuwa unamuona hajui kuimba ila alikuwa na mashabiki wake na alikuwa anapiga international show zaidi ya hao wasanii wako unaosema wanajua kuimba!
All in all Kazi nzuri hupimwa kwenye matokeo yake na kitakwimu.
FAlly ipupa kamzidi Fere Golla kwenye Kila takwimu.
International awards, international shows, kazi kufanya vizuri kimataifa.
Naufatilia mziki wa congo zaidi ya unavyofikiria.
Mnachoshindwa kujua ni kuwa muziki wa Sasa hivi kama hauwi VERSATILE MUSICIAN lazima upigwe chini . Si unaona Ali kiba aliamua aimbe Amapiano.
Sasa Fally anaimba RnB kamsikilize kwenye NIDJA FTR. Kelly. FAlly anaimba pure rhumba kaikilize SE-YO.
FAlly anaimba modern french music kamsikilize kwenye ARMOUR.
FAlly anaimba Pure BOLINGO MUSIC kamsikilize kwenye Mkwaju unaitwa FORMULE 7.
Kingine kinachombeba fally jamaa ni Dancer kitambo.
FAlly anaimba Genre za muziki ndio zinambeba tofauti na Ferre Gola anaimba Genre Moja tu. View attachment 2849441
Mkuu, umemaliza kila kitu na uzi ufungwe kabisa, maana watu wanashindwa kujua kua ferre gola ni mwanamuziki pure kabisa kuliko fally ipupa ambae ni msanii mwenye kuimba kwa biashara zaidi.Tunazungumzia rhumba mzee au umerogwa, huwezi kumshindanisha kwa kila kitu Ferre na Fally kwa sababu wanatofautiana sana kwenye vingi ila katika rhumba hakuna kama Ferre sio tu huyo Fally bali wote kwa kizazi chake. Hizo genre zingine Ferre wala haimbi.
Tunaomjua Ferre alianzaga kama Fally wakati anaanza muziki akiwa Wenge mwaka 1994, alikuwa anarap, anacheza n.k ila Werrason akamshauri ajikite zaidi kwenye rhumba maana anaiweza zaidi, na kweli huko ndiko alikofanya maajabu mpaka leo hakuna kama yeye, hivi nikuulize wakati Ferre anatoa Vita Imana huyo Fally alikuwa wapi, najua hujui ila nakujuza, Fally alikuwa stage show na kuimba kidogo pale QI kwa Mopao.
Anayway nisikuchanganye zaidi ila we kaa ukijua Ferre ni mkali wa Rhumba kuliko mwanamuziki yeyote Congo kwa kizazi chake.
Kingine tambua kuwa Ferre amepiga band zaidi ya moja na amepiga na wasanii wengi wakiwemo magwiji wa muziki wa Congo kama Jb Mpiana, Ngiama Makanda, Mopao Quadra Kora Man ambao wote walimpa heshima ya juu, mfano Ferre ndio msanii pekee aliyevunja rekodi ya usajili wakati anasajiliwa kujiunga na QL International ya Koffi wakati huo Fally anashangaaa tu.
Ukitaka kujua anayofanya Fally kuimba kila genre Ferre alishafanya basi tafuta show ya Wenge BCBC ya mwaka 1996 uone Ferre alivyorap kama pure atalaku na hakuimba Rhumba hata moja show nzima.
Huijui we labda uijuie 100 kilos, kwa maelezo yako we ni mweupe kwenye mziki wa congo hujui mengi na pia umetanguliza mbele ushabiki kuliko uhalisia, mimi kama mpenzi wa muziki wa Congo nawapenda wasanii wote Ferre na Fally na kila mmoja ana ladha yake katika muziki na pia kila mmoja kuna anachokijua zaidi, mfano Ferre anajua zaidi muziki wa Rhumba kuliko Fally na hii ni kutokana na nyimbo zake nyingi za rhumba ni nyingi na nzuri kuliko Fally, ni kawaida kukuta album nzima ya Ferre imejaa rhumba tupu. Hii ni tofauti kwa Fally ambaye katika album zake nyingi nyimbo za bolingo (genre) tunayoitambua wabongo ndio nyingi lakini pia ndio zinaibeba album mfano Bakandja, 001, Ecole, Nzoto, Allo Telephone n.k. kwa hiyo Fally amempita katika nyimbo za bolingo zile za speed ambazo Ferre haziwezi. Sasa cha kujiuliza ni kimoja je Fally ni mkali wa bolingo kuliko Ferre lakini ni mkali kuliko wasanii wengine wa bolingo kwa kizazi chake? Ferre ni mkali wa Rhumba je kuna msanii mkali wa rhumba kuliko Ferre? Kama yupo mtaje.😃
Kwamba unadhani siijui mkuu
Kuanzia mwaka 1999 Hadi 2006
FAlly ipupa alikuwa chini ya Ya Koffi Olomide
Sikia verse zake hapa
View: https://youtu.be/_GxrZARFo8A?si=j1ruEApjmD7g9_GK
Na hapo alikuwa anapewa mara Moja moja aimbe na kucheza