Huwa unakagua usafi sehemu unayoenda kupata chakula?
Nakazia… kuna mazingira yako wazi yanaogopesha, kuna mazingira yamejificha mpk uchokonoe… ndio maana kabla ya kula tunapaswa kuombea chakula 😂😂

kule Morombo kwenye mbuzi panaitwaje? mshamba_hachekwi nilienda mara 1, namna nilikuta hata kwenye gari sikushuka, na tokea hapo sijawahi kurudipo.
😀😀😀😀🙌🏻kwa mromboo ni habari ingine wallah
 
Mimi sio mpenzi wa kula migahawani ila tu ikitokea nikala nje ntaenda kwenye hotel ya hadhi kiasi
Muonekano wa hotel nzuri utaijua tu. Wahudumu walivyo na hata chef alivyo

Napenda usafi sana hata hotel za kulala huwa Nakagua kwanza kama haijaniridhisha naaga kwa heshima tu naenda nyingine
Kwa hapa bongo usafi umetushinda kabisa hata hizo 5 star hotel baadhi ni za ovyo na hii inasababishwa na wamiliki kutojali wafanyakazi wao , kudhalilishwa ovyo kutukanwa...
 
Mimi sio mpenzi wa kula migahawani ila tu ikitokea nikala nje ntaenda kwenye hotel ya hadhi kiasi
Muonekano wa hotel nzuri utaijua tu. Wahudumu walivyo na hata chef alivyo

Napenda usafi sana hata hotel za kulala huwa Nakagua kwanza kama haijaniridhisha naaga kwa heshima tu naenda nyingine
Na huo ndiyo uungwana
 
si wanasema ukimchunguza sana bata huwezi kumla
Hasa migahawa ya Uswahilini DSM michafu na wengi wanaokula ni kama akili hazipo sawa. No offence intended. Kuharisha na uchafu nje nje.

Mitaa hii kwa DSM ichunguzwe; Kimara, Mabibo, Mbagala, Tandale na mingine mingi kama hiyo.

Utaijuaje? Utaijua kwa kusikia sikia majina kama Asha, Fatu, Mwaju, Zai nk[emoji23]
 
Niliona muuzaji anapiga chafya kwenye mbonga ya majani anayochambua bila kuzibq mdomo, nilichoka sana
Pia nilishawahi kushuhudia hili, shortly ni kuwa best and delicious food ni kile unaandaa mwenyewe. No one cares about your health at all, they care about your pocket.
 
siku za weekend nafunga safari ya 40km mpaka Tabata
spots zote ni swafi,
huku niliko nikivamia mgahawa tu, nijiandae kuhara damu
Aisee, kuhara ni kubaya sana. Wengi wa wateja wa migahawa hiyo ni kama siyo binadamu kamili. Wengi ni mateja na desperate people. Aisee Uswazi ni bullshit.
 
Wengine kuchokonoa puaaa

Ndomana sehemu za kula jiko linakuwa wazi wapishi unawaona
Wanavyofanya madikodiko
Hapo angalau kidogo kuna kausalama

Ova
Na kingine... asilimia kubwa ya wanaume huingia maliwato kupata haja ndogo halafu hawasafishi mikono baada ya kushika mtarimbo. Hili lipo sana sana, na anakuja kupeana mkono na watu...
 
_20231202_143111.JPG
 
Niliona muuzaji anapiga chafya kwenye mbonga ya majani anayochambua bila kuzibq mdomo, nilichoka sana
Kuna wengine wanauza vyakula na vinywaji huku wanachokonoa pua.
 
Tabia ya hovyo zaidi ni kutumia jagi la kunawashia linalowekwa kwenye bakuli ya maji machafu yaliyonawia kuchotea maji pia.
 
Na kingine... asilimia kubwa ya wanaume huingia maliwato kupata haja ndogo halafu hawasafishi mikono baada ya kushika mtarimbo. Hili lipo sana sana, na anakuja kupeana mkono na watu...
Nje ya mada
 
Wakuu weekend inaendaje?

Usafi ni muhimu kila sehemu, na linapokuja suala la chakula mkazo zaidi unahitajika, maana ukizembea kidogo tu unaweza kuathiri vibaya walaji wako hata kupelekea kifo uchafu aliokutana nao hapo ni mkubwa na kutengeneza sumu kali.

Umeshawahi kukagua sehemu unayokula ukaangalia kama maji wanayotumia kuosha vyombo na kupikia ni masafi, kama vyombo unavyotumia vinasafishwa vizuri, au hayakuhusu ukifika unakula tu unasepa zako?

Pichani, ni sehemu ya chakula Dar ambako ilikuwa sehemu pendwa ya kupata mbuzi. Siku moja nikaona hayo maji kwa uzuri, maji ambayo yalikuwa yakitumika kusafishia visu vinavyokatia nyama, ndimu, pilipili, na ndio maji hayo walikuwa yanatumika kusafisha meza na sehemu ambayo nyama (ya ng’ombe, mbuzi, kuku) inawekwa kwaajili ya kukata vipande vya mteja.

Ili kusafisha anachovya kitambaa ambacho nacho rangi inaenda kufanana na maji hayo kwa kuuzoea uchafu huo.

Maji hayo kama unavyoyaona yalivyomachafu, bado kunakuwa na vimabaki vya chakula ambayo vinakuwa vinaanguka hapo akiwa anajiandaa kumfungia mteja, na kuna kisabuni kwa mbaliii!

Siku hiyo nikamfata jamaa aliyekuwa anawasimamia kumuuliza kwanini hawabadilishi maji wanayofanyia usafi hapo mpaka yanakuwa machafu hivyo, jamaa akasema akasema unajua hiyo ni leo tu yanabadilishwa sasa hivi, nilijua anadanganya ila nikamwambia sawa, nitafatilia jambo hilo. Nilichukua picha lakini niliipoteza, hivyo nikarudi siku nyingine maana nlijua ntakuta tu maji machafu.

Siku nyingine niliyoenda ndio nikachukua na picha hii, ambayo kwakweli uchafu ni ule ule tu.

Hii ni hatari, kama tumbo lako hoya hoya unaweza kupigwa na sumu ya chakula matata sasa. Mabwana afya huwa wanapita kweli sehemu hizi za vyakula na kuhakikisha usafi unafuatwa?

Sehemu unayokula ikoje Mkuu, usafi ni wa hali ya juu au tumemjachia mungu?
Cyo usafi tu, mm mwanamke anayenyonyosha siwezi kula chakula chake aisee watanisamehe tu
 
Nakazia… kuna mazingira yako wazi yanaogopesha, kuna mazingira yamejificha mpk uchokonoe… ndio maana kabla ya kula tunapaswa kuombea chakula 😂😂

kule Morombo kwenye mbuzi panaitwaje? mshamba_hachekwi nilienda mara 1, namna nilikuta hata kwenye gari sikushuka, na tokea hapo sijawahi kurudipo.
Aisee....
 
Back
Top Bottom