Huwa unamuamini asilimia ngapi mwenyeji wako anapokwambia usiogope, Mbwa wake hang'ati?

mbwa ambaye haumi wenyeji ulio nao hawezi kukuuma wewe,kosa la kwanza ni kuanza wenge kama unachomoka mabawa mgongoni na kukimbia hovyo ukitengana na wenyeji wako,atakuuma.

saikolojia ya mbwa hubadilika anapoona mgeni,lakini mgeni salama ni yule aliye na mwenyeji wake au aliye mtulivu hata baada ya yeye kubweka.

kuna mpuuzi nilienda naye nilipopanga kulikuwa na geti na mbwa,nikamtahadhalisha mbwa haumi,awe mtulivu heee,kufungua tu geti mbwa akamsogelea jamaa akaanza kutuka ruka kama kuku kavaa mvuko mguuni😂😂,mpaka ananirukia mimi,yaani nilimind sijui alikuwa na majini mjinga yule.
 
Hapana kwakweli ni asilimia 0.000% maana mimi Mbwa au Ng'ombe bora nikutane na simba au chatu.
 
Mimi ile wanakuja kwangu tu, ningeludi ndani ya gari mbio hahahaha
Mbwa akishakuwa karibu yako hautakiwi kukimbia, maana kitendo cha kugeuka ili ukimbie mwenzako atakichukulia kama vile unapanga shambulizi dhidi yake, so atakuwahi na atakuchana chana vibaya sana.

Unapomuona ashakufikia karibu, unachotakiwa kufanya ni kuuvaa ujasiri kwa kujifanya umemzoea, unampenda na uko tayari kucheza nae. Kwa kuwa mbwa wamepewa fahamu, basi ataweza kufahamu kuwa wewe sio adui yake bali ni rafiki yake, na hapo ule mpango wake wa kukuvamia ili akudhuru utakuwa umekufa kibudu.
 
Wewe ni jasiri sana kwa hapo mimi ningeliwa tu mana ningetoka mbio na hili ni kosa. Mbwa sinaga urafiki nao kabisa wakati mtoto waliwahi kuniumiza hadi leo hii hawa viumbe hatuna ukaribu kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
🤣🤣🤣 Mkuu pamoja na kwamba niliogopa ujio wao, lkn niliona sina njia nyingine ya kufanya ili nijinusuru ikabidi nijifanye tunafahamiana. Na wao kwa bahati nzuri wakanielewa.
 
Kuna jiran yetu kipind tupo watoto alikuwa anafuga mbwa mbuzi na mifug mingi tuka agizwa kufwata mbolea kwa jirani yetu tulipofika tukagonga akasema piteni mimi na kihelehele kuingia ndani mbwa alikotokea sijui mpka leo akawa nakuja kwa kasi nikawa napiga kelel yeye mwenye mbwa anaangalia tu alipo ona anakalibia kabisa ndio akamuita jina lake akaondoka tulipo ludi nyumban nikawahadithia wakatukataza kwenda tena mpka leo siamin mtu kwenye hiyo kauli
 
Katika viumbe ambao huwa siwaogopi ni mbwa na nyuki nimecheza nao muda mrefu najua tabia zao sana nyuki akikutana na mimi huwa anageuka kipepeo na mbwa anageuka mbuzi
Mkuu nipe tip hyo ya nyuki
 
Hahaaaaa
 
Aisee! Hakuna mnyama rafiki kama mbwa,mnyama yeyote ukurarua tu pale anaposikia harufu ya uoga wa MTU....kutikisika kwingiii...lakini ukijiamini nae anaogopa hawezi kukugusa.

Na kuhusu kuamini kauli ya mwenyeji ni kwamba kama aliongopa tu ili kuniaminisha bas nikiguswa ajiandae kuzika mbwa wake.
 
Mkwara huo
 
Wenyeji wengine ukizongwa na mbwa wao wanacheka tu[emoji1787],

Mie mbwa akitaka kunizongo nakuwa mkali zaidi yake,tena kama kuna mawe nampiga,

Home nachekaga tu usiku watu wanavyokimbia kuogopa mbwa,wangejua mijibwa yenyewe inabweka tu wala haing'ati[emoji16]
 
[emoji1][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]kiumbe ambae huwa ctakiii hata anisogeleee
 
Ungekimbia tu ungeisoma namba [emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…