Huwa unamuamini asilimia ngapi mwenyeji wako anapokwambia usiogope, Mbwa wake hang'ati?

Me toka nifukuzwe na mbwa la kizungu na limepanda juu sana na likaniangusha chini likabaki linanilamba Lamba usoni tu, kipind hicho tunaruka fensi tunaingia ndani Kwa mzungu kuokota makopo jalalani ya kutengenezea magari miaka hyo na hakuning'ata na wenzangu kabla washadakwa na kung'atwa vibaya, basi mbwa simuogopi kabsa... Yule mbwa alinijengea confidence sana...wenzangu walipoona sekeseke walikimbia Japo walikua njee ya fensi ya mabanzi... Baadayee tunaonana wanabaki wananishangaa... Utoto raha sana..
 
Binafsi nimeishi na mbwa toka utotoni mpk leo nazeeka ninao. Nimeshafuga mbwa wa aina zote hadi nimechoka kwa sasa nina mbwa watano wa kienyeji nawalisha vizuri wako gado.

Katika kuishi na mbwa nimewahi kuumwa mara 2 na mbwa wangu mwenyewe na pia kuna mmoja alinichania suti ya gharama

Kuna project Kibaha nitaianza 2023 Inshallah ya kubreed mbwa niwauze. Ni bonge ya ulinzi. Nikilala nyumba haina mbwa nakosa imani usiku. Nahisi kama naweza kukutana na kibaka keshanifikia mlango wa room bila hata kujiandaa
 
Alijua ni mwizi[emoji23]
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Katika ujinga ambao sipendagi kuusikia ni huo. Huwa namuona Mwenye nyumba ni kama tapeli hivi.

Kama unanitarajia nakuja kwako basi cha muhimu fungia Mbwa wako kwenye Banda lao.
Hiyo ni mbinu moja wapo ya kukufanya uingie ndani kwa lazima

Mimi mwenyewe nina mpango wa kufunga mbwa sio kwa ajir ya ulinz ila kwa ajil ya wageni wa kike tu ambao sina udugu nao
 
Hiyo ni mbinu moja wapo ya kukufanya uingie ndani kwa lazima

Mimi mwenyewe nina mpango wa kufunga mbwa sio kwa ajir ya ulinz ila kwa ajil ya wageni wa kike tu ambao sina udugu nao
Heheh
 
Mnyama hana urafiki
Kuna bull dog wa jamaa akiwa kwake mtoto wa ndugu yake wa miezi 18 akawa anacheza nae
Ghafla alimng"ata kichwa hakuachia mpaka mtoto akakata roho huku akimzunzusha kama mwanasesere

Jina ujinga na mbwa kabisa nilishawahi kuumwa utotoni na mbwa wa jirani

Nikija kwako kama una mbwa na kuambia mfungie sehemu
Hivi ni sifa kumuacha mbwa akae na wageni? Ili iweje show-off ama
 
Kwa uzoefu wangu mbwa hata aweje huchukua siku chache kuzoea harufu mpya

Niliwahi kupanga nyuma moja ina mbwa mkali asee, tena nilikua nasotea kazi sehemu flani miaka hiyo.
Yule mbwa mchana huwezi kumuona mpaka saa tano usiku ndo anafunguliwa

Mara ya kwanza nilitoka nje usiku akaja na kasi ya ajabu ila hakufanya kitu, kesho tena nikajaribu kutoka nje mpaka akanizoea nikawa namfungulia mwenyewe na kumfungia bandani
 
Alikuwa mbwa koko
 
Mkuu usije rudia tena kushika mbwa kichwani kama hauna urafiki nae, kuna baadhi ya mbwa atakufanya vibaya sana, mie shahidi, kuna wengine ukimshika masikioni umetangaza vita.
Story yako imenivunja mbavu, Pitbull wanaogofya...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…