Kuna jamaa nilienda kumtengenezea gari kwake. Kufika kwake nikakuta anafuga mbwa wawili, yan pit bull wakubwa walioshiba.
Akanambia wewe fanyakazi tu wala usiogope. Kwa vile ilikuwa mara yangu ya kwanza kufika kwake, nikajifanya sina uoga na viumbe wale.
Nikiwa katika harakati zangu za kazi mara jamaa akanifuata na kuniambia kuwa anatoka mara 1 kwenda kumfuata mtoto shuleni (sio mbali sana na anapoishi) akasema wewe usiwe na wasi wasi hao hawawezi kukufanya chochote.
Dah kukataa nikashindwa na kukubali pia nikashindwa nikabaki kumeza fundo la mate huku nikijifanya sina wasi wasi na viumbe wale. Jamaa akaniachia funguo 1 ya gate la nje akafungua gate akatoka na kutuacha sisi watatu, yani mimi na ile mi pit bull miwili, basi ikawa inaniangalia huku inanikazia macho kama vile inataka nijichanganye kidogo tu inichane chane, maana tayari ulimi uko nje, huku mijino kama vidole vya mtu mzima.
Kitu cha kwanza nikatoka chini ya gari na kuingia ndani ya gari. Sasa wakati nikiwa ndani ya gari nikasikia honi ya gari inaita kwa nje ya nyumba, nikajiuliza huyo ni mshikaji amerudi anataka nikamsaidie vitu au ni mtu mungine anapiga honi nyumba ya pili, honi ikaendelea wale mbwa wakakurupuka na kukimbilia mlangoni wakawa wanabweka ile mbaya.
Hapo nikajua anaepiga honi yuko mlangoni na pia inaonesha sio mwenyeji wa nyumba ile maana ingekuwa ni mwenyeji wasingebweka vile, kidogo simu inaita jamaa ananambia nichukue funguo alioniachia nikamfungulie mgeni wake.
Hapo ndio palikuwa patamu maana jamaa nilikuwa nishamuonesha kuwa wale mbwa siwaogopi, sasa naanzaje tena kumwambia kuwa naogopa kwenda kufungua? Ikabidi nimwambie kuwa niko msalan nakata gogo, akasema poa fanya fasta basi ukamfungulie.
Jamaa akampigia akamwambia mgeni asubiri nikimaliza kukata gogo nitamfungulia. Baadae akanipigia tena bado tu, nikabidi nimwambia ndo najisafisha natoka sasa hivi.
Nikasema potelea mbali wakinivamia atanilipa, nikaanza kulifuata gate la nje kwa kunyata kumbe washanisikia ghafla nikaona hao wanakuja mbio upande wangu, nikaona nikikimbia watanivamia, ikabidi nioneshe ukakamavu ghafla hawa miguuni, sasa nilichofanya nikamshika yule dume kichwani kama nampalaza palaza likatulia huku likionesha kuelewa ninachokifanya nikawa natembea mdogo mdogo kuelekea getini huku wakinifuata kama vile ni mtu wanaenifahamu, ile kufika getini nafungua na mwenyeji namuona yule kwa mbali anakuja. Basi wakaingia wote mwenyeji, mtoto na mgeni tukafunga geti.
Aisee siku ile sintoisahau.
Kwa wale wasiomjua pit bull, huyu hapo pichani kulaleki 😂