Huwa unamuamini asilimia ngapi mwenyeji wako anapokwambia usiogope, Mbwa wake hang'ati?

Amfunge kwanza ndo niingie ndani ya geti.
 
Katika viumbe ambao huwa siwaogopi ni mbwa na nyuki nimecheza nao muda mrefu najua tabia zao sana nyuki akikutana na mimi huwa anageuka kipepeo na mbwa anageuka mbuzi
Nilikua na rafiki yangu tunatembea, ghafla kuna mwanamke mmoja akapiga ukelele, tukashtuka kuna nini? "nyokaa" "nyokaa", tukasogea pale, jamaa wakaanza kumpiga yule nyoka mawe, nyoka akaingia kwenye kimti kwa chini amejificha, basi akatokea jamaa mmoja hivi mlevi na mwenzie anasema "msimpige macheni, nyoka mimi haniumi, nyoka wananijua muacheni nimkamate", basi tukaona ngoja leo tuone miujiza.

Ila tukamtahadharisha yule mlevi asifanye mchezo ile ni hatari.

Jamaa akasogea pale nyoka ameacha mkia, jamaa akamkamata mkiani kamnyanyua hakuwa mkubwa sana, yule nyoka akawa kichwa kipo chini jamaa kashika mkiani, yule nyoka akageuza kichwa kuelekea kwenye mkono wa jamaa, jamaa si akaona anang'atwa, hajamrushia huku tulipokua, acha watu wasambae , asee yule jamaa tulimfukuzaje?

Kama mwizi, jamaa pombe iliisha alikuwa anakanyaga kibati hatukumkamata yule nyoka sijui alipotelea wapi...
Hio kauli yako imenikumbusha hio moment, hizo kauli siziamini kabisa...😂🤣
 
Mkuu usije rudia tena kushika mbwa kichwani kama hauna urafiki nae, kuna baadhi ya mbwa atakufanya vibaya sana, mie shahidi, kuna wengine ukimshika masikioni umetangaza vita.
Story yako imenivunja mbavu, Pitbull wanaogofya...
Hawa jamaa pitbul wanatisha kimuonekano, lakini hata kivitendo, na pia wana nguvu sana. Niliona video flani ya kweli huko USA polisi walikwenda kumkamata jamaa fulan, wakati wanamkamata ile wanamfunga pingu basi pitbul wake hata alipotokea mi na wewe hatujui akamvaa askari mmoja ambae na yeye huyo askari alikuwa ameshika bonge la mbwa germansheffield, basi na yule germansheffield na yeye akamvaa pitbull hapo ndo palipokuwa patam kuwaachanisha ilibidi mtuhumiwa afunguliwe pingu na kuombwa amtulize pitbul wake huku na yule polisi akipambana kumtuliza germanffield wake ambae alikuwa ashaonesha kutokumtii kabisa. Kila apokuwa anamwambie aache kupambana na yule pitbul ndo kama vile alikuwa anamzidisha hasira huku pitbul nae akikataa kudhalilishwa mbele ya boss wake (mtuhumiwa mwenye mbwa)
 
Kuna chance ndogo ya Shepherd kumkabili pitbull, lakini shepherd ni mbwa ana akili nyingi, mjanja na mtiifu sana, shepherd anapoona mmiliki wake yupo hatarini atajaribu awezalo kusaidia, ndio maana huyo mbwa wa askari alikuwa mbishi.

Shepherd kwa ulinzi wapo vizuri.
 
Kwa maelezo yako haya, nimeamini kama wewe unawajua mbwa vizuri.
 
Mkuu usije rudia tena kushika mbwa kichwani kama hauna urafiki nae, kuna baadhi ya mbwa atakufanya vibaya sana, mie shahidi, kuna wengine ukimshika masikioni umetangaza vita.
Story yako imenivunja mbavu, Pitbull wanaogofya...
 
Duh noma noma,nilionaga video flani jamaa anashambuliwa na mbwa wawili huko marekani kati kati ya mitaa,jamaa yupo chini anaburuzwa tu,wale mbwa walikua wakorofi sana,wananchi walijaribu kuingilia lakini walishindwa na wengine wakaishia kung'atwa

Bahati nzuri waliwapigia askari simu,na askari wakawahi chap ndani ya muda mfupi sana wakawa wamefika,na wakajaribu kuwazuia wale mbwa ila wapiii na jamaa anavuja damu yupo hoi bin taaban

Polisi wakaona hapa tutampoteza jamaa kwa uzembe,wakachomoa bastola wakawapiga chuma wale mbwa wotee wakafa ndo wakamkimbiza mchizi hospitali
 
hao mbwa c ndo chotara wa simba hao?

Yaani Mimi toka nipigwe mtama na mbwa nikaangukia uso Sina hamu tena na wala Sina urafiki na mbwa kabisa .
 
Mbwa ni mmoja wa wanyama ambao ni hatari sana japo tunaishi nao kama walinzi wetu na marafiki zetu.
 
hao mbwa c ndo chotara wa simba hao?

Yaani Mimi toka nipigwe mtama na mbwa nikaangukia uso Sina hamu tena na wala Sina urafiki na mbwa kabisa .
Ilikuaje mkuu mpaka ukachotwa mtama? Aisee kuishi kwingi ni kuona mengi 🤣🤣🤣
 
Nisivyowapenda mbwa na paka uwafungie tu bandani. Sitaki habari za kuniambia usiogope hang'ati.
 
Mbwa hawaaminiki kama hawakujui, wale mbwa wa Kingunge wangemuua kabisa. Imagine mtu anaewalisha na wamemgeuka, itakuwa wewe wasiokujua?
Hata mbwa wa Kingunge hawakuwa wanamjua Kingunge kama ndio boss wao. Hii ni kwa sababu Kingunge aliajiri kijana ambae ndie aliekuwa anawalisha na kuwapa huduma zote walizozihitaji kupitia mfuko wa Kingunge, sasa mbwa wakajua kuwa yule kijana ndio boss wao, afu Kingunge wakamchukulia kama ni mpita njia tu ndo maana wakamvamia na kumchana chana vibaya.
 
Mbna inatisha sanaaaaaa, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…