Huwa unapotezeaje kumpa shikamoo mtu usiye kuwa na uhakika anastahili shikamoo?

Huwa unapotezeaje kumpa shikamoo mtu usiye kuwa na uhakika anastahili shikamoo?

Salamu yakitaifa, Habari yako ndugu, hii itajumlisha woteeee
 
sio ya kwetu,ni ya utamaduni wa mwarabu,

Sent using Jamii Forums mobile app
Unaweza kusema pia "amani iwe juu yako"
ni kitu kile kile haina jinsia wala mkubwa au mdogo.
ikishindikana unaweza kuendelea tu na ya wazungu muhimu ujumbe ufike na maslahi yapatikane.
maslahi ni kwamba kwa upande wa waislamu ambao mnaita waarabu ni kwamba unapomsalimia mtu "assalam alaykum " tayari unaandikiwa thawabu haijalishi ameitikia au hakuitikia, ila akiitikia na yeye anapata pia thawabu,pia haijalishi aliesalimia ni mwarabu au mzungu malipo yapi kama kawaida
sasa kwanini kupoteza fursa?
 
me siku hizi stoi shikamo... ni mwendo wa mzee kwema?
Usimwite mtu Mzee hakuna mtu anaitwa jina la mzee. ukimuona mtu mzima sana mwambie Baba hali yako au Mama hali yako kama dada hali yako nadhani ina sound better.
 
Hakuna kitu kinanichukiza kama hizi salamu mpya Salaam alaykum halafu bwana yesu asifiwe. Salam alaykum sio salamu ya kidini ni neno la kiarabu amani juu yenu hata neno Hali au Salama ni maneno ya kiarabu. Kwenye hali halisi mitaani watu wanasalimiana Asalam alaykum mpaka kesho na unaweza kumsalimia hata mtu mzima ni salamu inafit marika yote mkubwa au mdogo. Lakini sijawahi kusikia mitaani watu wakisalimiana Bwana yesu asifiwe sijui imetoka wapi hii au ndio dhana ya ushindani wakati hakuna uhalisia wa salamu hii tumeanza kuisikia juzi juzi tu hawa wanasiasa uchwara.
 
Usimwite mtu Mzee hakuna mtu anaitwa jina la mzee. ukimuona mtu mzima sana mwambie Baba hali yako au Mama hali yako kama dada hali yako nadhani ina sound better.
Waite hayo majina wewe mwenyewe, huo muda sina. Nimuite baba kivipi? kwanini? sina huo muda.
 
Kipindi fulani niliwahi kuwa mwalimu.Sasa nikiwa na maticha wenzangu tumetoka zetu kambini tunaenda misele tukakutana na mama flani hivi bonge la mama mtu mzima.sasa mimi si nikamwambia shikamoo ,wenzangu baada ya pale wakawa wanacheka hawana mbavu, nawauliza kulikoni ndio wananiambia leo mwalimu amemsalimia mwanafunzi wake shikamoo.Sasa yule binti aliacha shule form 2 na mimi nilikuwa nafundisha form 3&4 tu.Sikua familia Sana kuwatambua.

Kwahiyo hasa Hawa wanawake wengine akishazaa watoto 2 wengine wanakongoroka wanakuwa Wazee au wanafutuka hadi sura zinapotea wanakuwa watu wazima.

Tangu wakati huo mpaka nimpe mwanamke shikamoo niwe nimejiridhisha Sana.
 
Shikamoo ni hadi ujiridhishe huyo mtu amekuzidi kweli umri miaka kama 7 na zaidi
 
Hakuna kitu kinanichukiza kama hizi salamu mpya Salaam alaykum halafu bwana yesu asifiwe. Salam alaykum sio salamu ya kidini ni neno la kiarabu amani juu yenu hata neno Hali au Salama ni maneno ya kiarabu. Kwenye hali halisi mitaani watu wanasalimiana Asalam alaykum mpaka kesho na unaweza kumsalimia hata mtu mzima ni salamu inafit marika yote mkubwa au mdogo. Lakini sijawahi kusikia mitaani watu wakisalimiana Bwana yesu asifiwe sijui imetoka wapi hii au ndio dhana ya ushindani wakati hakuna uhalisia wa salamu hii tumeanza kuisikia juzi juzi tu hawa wanasiasa uchwara.
Wakristu tunasema pia ^Neema na amani viwe kwenu^
 
Mbona infracty soja anatuamkia shikamoo ili hali wengine ni wadogo zake
 
Halow bro.
Halow sister.
Goodmorng.
Goodafternoon.
Goodevening.
Mzee wangu polee na kazi.
Shikamoo kwangu ulimi huwa mzito sana. Pia sipendi kusalimiwa salimiwa maana mpaka sasa sijawai kuona faida yake.
 
Back
Top Bottom