Rare Sapphire
JF-Expert Member
- Jul 24, 2021
- 590
- 1,648
Wakuu kwema?
Inaweza kutokea ndugu yako akaomba kumpiga picha mtoto wako akisema mtoto amependeza au mtoto wako mzuri picha zitatoka vizuri, wakati mwingine inaweza kuwa hata kwa majirani au watu ambao huwajui kabisa.
Dunia imebadilika, huwezi kujua unayemruhusu ampige picha mtoto wako ameficha nini moyoni.
Picha hizo zinaweza kutumiwa kwa namna tofauti kama vile;
Mambo haya yanatokea kwa wingi kuliko vile tunavyofikiria, hivyo mzazi kuwa makini na mtoto wako, usiruhusu mtoto wako apigwe picha ovyo ukawa njia ya mtoto wako kwenda kufanyiwa ukatili.
Unaweza kusema unamuamini mtu anayempiga picha ni kaka yake, mjomba wake, shangazi yake, jirani mwema nk, lakini matukio mengi yameonesha si kila unayesema unamjua yupo hivyo kweli. Pamoja na hayo yote, kwanini apige picha ya mtoto wako, ili iweje?
Nini maoni yako kuhusu hili?

- Matangazo ya Biashara: Mtoto anapigwa picha na picha zake zinaenda kutumiwa kwenye matangazo mbalimbali bila ridhaa yako.
- Picha hizo kuuzwa kwa watu wenye 'fantancy' za kingono zinazohusu watoto.
- Picha hizo kutumika kama sampuli za kwenda kuonesha bidhaa (mtoto wako) kwa watu wanaojihusisha na biashara haramu za binadamu (human trafficking). Mteja akipenda mtoto wako itatafutwa mbinu itakayoweza kufanikisha kupatikana mtoto wako na atakachoenda kufanywa huko ni chochote atakachoamua mnunuzi, sababu tayari anamiliki 'bidhaa' hiyo.