Huwa unaruhusu mtoto wako kupigwa picha na watu mbalimbali ikiwemo ndugu? Unajua madhara yake?

kwenye hili la picha nakumbuka kuna mganga alishikwa akiwa na picha za watu mbalimbali ambao alidili nao katika kazi zake
 
Upo sawa kabisa lazima tuwe makini watu si wema sana siku hizi picha ni rasilimali muhimu sana kwa mtu anayetaka kukudhuru hasa tunaoishi uswahilini..
 
Angalizo zuri,lakini nikitaka picha za watoto,naiingia mtandaoni TU,zimejaa kibao,mpaka video.
 
mbona watu wengi tu wana weka picha mitandaoni inamaana km mtu anataka picha si anachukua tuu huko? au picha ya kupiga na muhusika in matter sana kuliko zinazo postiwa mitandaoni
 
mbona watu wengi tu wana weka picha mitandaoni inamaana km mtu anataka picha si anachukua tuu huko? au picha ya kupiga na muhusika in matter sana kuliko zinazo postiwa mitandaoni
Kuna ambazo zinapigwa kwa matumizi ya biashara kutangaza kitu fulani mzazi akiwa anajua kinachoendelea, na picha iliyopigwa haiibui hisia nyingingine japokuwa hilo haliguarantee wenye nia mbaya kufanya kitu kibaya au kuona zaidi ya kinachooneshwa, na nyingi ambazo zipo kwa dhumuni la biashara zinakuwa hazina taarifa kumuhusu mtoto huyo kama vile; jina, shule anayosoma, anapoishi nk, tofauti na sisi watu wa kawaida tunaoweka picha za watoto wetu kila wakati kwenye events mbalimbali na taarifa nyingi zinazowezesha mtu yoyote mtandaoni kukufikia hata kama hakujui/hamna ukaribu.
 
Wakizitaka picha wanazidownload kwenye mitandao wazazi wengi utupia picha za familia zao huko
 
haimake sense bwana imani zenu tuu mtu anawezaje kupost picha akatoa maelezo yote hayo?/ mahali anapoishi, shule na details nyingine? watu wanapost watoto kwenye event mbalimbali miaka nenda rudi... dunia ya sasa ni utawazi mtu anapost tokea mtoto anazaliwa hadi anahitimu chuo na hakuna baya lolote linalomkuta.... me imani ya mtu tu na mawazo yake....
 
Usiseme haiwezi kutokea wakati matukio yanatokea kila kukicha fanya utafiti utakungundua hilo, lakini pia kuna taasisi nyingi zinazoshulika na haki na usalama wa watoto, nenda upate taarifa halafu urudi hapa....nakukuhakikishia utatengua kauli
 
Kwa mazingira ya tanzania ambayo unakutana na watoto kila pembe unayopita wakiwa peke yao wanacheza, wanauza machungwa, wamelala, wanaomba, wanafuata ngoma ya mdundiko, wanafuata gari lolote la matangazo n.k wala hakuna haja ya kuingia katika wakati mgumu kama huo ili kuwapata wa kuwauza.
 


Dawa ni kuomba Mungu, mtoto akienda shule ni nani analinda yote haya?
 
Kwahiyo tatizo ni mtoto akipigiwa picha au picha ya mtoto ikipatikana popote pale
 
Acha ku complicate maisha man.
 
Mwisho utaanza kusema sitaki ndugu nyumbani kwangu. Acheni complications za kipumbavu kwenye maisha. Fikra kama hizo zinapunguza upendo kwenye jamii na kuchochea ubinafsi. Mitoto inakuwa haina heshima kutokana na upuuzi wa wazazi kuendekeza ubinafsi. Cha kushauri ni watu kuwa na kiasi kwenye kutumia simu zao kwa sababu siku hizi watu wameshajiona wao ni wapiga picha na maripota wa matukio.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…