Huwa unatumia vigezo gani kumjua mshamba?

Huwa unatumia vigezo gani kumjua mshamba?

Mshamba ni nani?

Jibu : Mshamba ni mshamba.


Haya sasa utamjuaje mshamba au huwa unatumia vigezo gani kuconclude kwamba mtu fulani ni mshamba?

Mimi huwaga naangalia vitu kadha wa kadha. Baadhi ya vitu hivyo ni hivi hapa chini[emoji116]

1. Akiwa anatumia True Caller.

Unapiga simu kwa Mwnyekiti mtendaji wa Bonyokwa halafu anapokea anataja jina lako " Hello Bwana Likud wa Jf habari yako" . Tayari najua nadili na mshamba.


2. Ana namba za simu ambazo ni unique.

Mfano: Ndugu zangu namba zangu za simu ni:

0766 22 33 44 au 0755 55 55 55 au 0765 11 22 33. Moja kwa moja huwaga najiridhisha kwamba nadili na mshamba. ( most of the time namba hizi huwaga wanazinunua kwa wale mawakala wanaopita barabarani)


3. Ana namba za simu zaidi ya moja za mitandao tofauti halafu zina banana.


Mfano: Ndugu zangu mkitaka kunipata nitafuteni kupitia :

Tigo: 0712 35 67 89

Voda ; 0766 35 67 89.

Airtel: 0688 35 67 89.

siwezi kutaja vigezo vyote taka na Wewe vigezo vyako
Dah hata wewe ni wale wale
 
Mtu anapiga simu zaidi ya mara tatu ndani ya wakati mmoja.
Ukipiga simu ya kwanza, ya pili haijapokelewa tuma ujumbe akutafute.

Kuongea kwa simu kwa sauti ya juu ili watu wasikie maongezi yako ambayo yanaashiria una hela/cheo kikubwa.
Au usipo pokea anakupigia simu kwa namba nyingine
 
Mshamba ni :-
1. Mtu yeyote aliyeoa/kuolewa hasa kwa harusi
2.Mtu yeyote asiyefahamu kutumia kompyuta hasa hasa ku type.
3. Mwanaume yeyote anayeenda kwa mitume kukanyaga chumvi
4.mwanamke yeyote anayesukia rasta/kuvaa wigi
5.Mtu yeyote anayeweka R badala ya L kwenye sentensi
6. Mtu ambaye hana choo kizuri kwake
7.Mtu yeyote anayevuta tumbaku
8. Mtu yeyote anayeomba omba pesa wakati kazaa mwenyewe
9.Mwanamke yeyote anayepaka makeup
10.kama una sabufa na kimeza cha kioo wewe ni mshamba
 
Back
Top Bottom