Huwa unatumia vigezo gani kumjua mshamba?

Dah hata wewe ni wale wale
 
Mtu anapiga simu zaidi ya mara tatu ndani ya wakati mmoja.
Ukipiga simu ya kwanza, ya pili haijapokelewa tuma ujumbe akutafute.

Kuongea kwa simu kwa sauti ya juu ili watu wasikie maongezi yako ambayo yanaashiria una hela/cheo kikubwa.
Au usipo pokea anakupigia simu kwa namba nyingine
 
Majority ya sisi wa tz ni washamba ikiwemo na mimi! Mfano ushamba wangu mimi ni kuangalia ndege angani ikipita . Tena ukute inapita huku inachora ule mstari mweupe baas, najisikia amani moyoni na roho inasuuzika yaani.
 
Mshamba ni :-
1. Mtu yeyote aliyeoa/kuolewa hasa kwa harusi
2.Mtu yeyote asiyefahamu kutumia kompyuta hasa hasa ku type.
3. Mwanaume yeyote anayeenda kwa mitume kukanyaga chumvi
4.mwanamke yeyote anayesukia rasta/kuvaa wigi
5.Mtu yeyote anayeweka R badala ya L kwenye sentensi
6. Mtu ambaye hana choo kizuri kwake
7.Mtu yeyote anayevuta tumbaku
8. Mtu yeyote anayeomba omba pesa wakati kazaa mwenyewe
9.Mwanamke yeyote anayepaka makeup
10.kama una sabufa na kimeza cha kioo wewe ni mshamba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…