- Mara nyingi historia yake huwa na mafanikio kabla hajaanza ulevi, mfano utaambiwa alikuwa ana akili sana darasani, alikuwa hakosi kanisani, alikuwa mfano kwa vijana wengine, n.k.
- wanazijua siri nyingi sana kuhusu familia, anayajua mengi kumhusu dada yake (mama yako)
- Kila mwaka utasikia nusu afe
- huwa hawaoi au walishaachwa
- maisha yake yapo kwenye auto pilot ni ngumu kuelewa ana survive vipi ila ana survive
- yupo peace, mshauri mzuri, hana makuu, ila haheshimiki sababu hana hela
- kazika marafiki wengi na bado ana marafiki kibao
- huwa wana pair moja ya viatu
- hubaki kijijini kuwakilisha familia kila mtu akirudi mjini, husafisha mazingira, kulisha mifugo
- sio mlalamikaji, karidhika na maisha yake hata anapokosa msaada wa ndugu zake
Mmoja rafiki yangu sijui km mzima yule.
Yes alisoma hadi Makerere huko miaka hiyo ya 70, alirudi kijijini akawa chizi.
Mara ya mwisho kuonana nae aisee kala pamba kali sana namuuliza we uchizi vp tena akanambia ile njaa tu mjomba,
Alikua kauza shamba na kuhama pale kijijini kabisa.
Mwingine huyu alipigana huko Burma vita ya pili ya dunia alivyorudi akapigika huko kijijini mda tu.
Mdingi ndo alikua mjomba wake akaona isiwe tabu kaenda kamleta home akae, ana upande wake huko pembeni nyumba kubwa ilikua ni kupiga menyu tu.
Yule mzee alikua peace sana yaani pale home wala jirani hajawai kuzingua.
Maza tena leo ntamkumbusha nilishamsahau.
Maana walikua marafiki wakianza kupiga mastory na kiingereza chao utapenda.
Huyo Mwamba kila jioni akienda vilabuni kupiga vyombo😁, analianzisha e bana anapiga kilabu walevi wote😅😅😅.
Ila sasa akitoka baru hakimbilii nyumbani anaweza kupita home mbio huku anakimbizwa na walevi wenzie.
badae anarudi gheto kwake
Anatulia ka sio yeye
Alikufa yule,
Dingi nae walikua hamna story nyingi Watasalimiana kila asubuhi ataachiwa kilinda mfuko basi,ukiona tu anapiga pasi nguo zake ujue huyo anaenda sebuleni.(kilabuni)
Jambo namsifu usafi.
Hapo alikua 100%.
Kuna siku shati moja jeupe limechanika mgongoni lakini kakomaa nalo kalinyoosha vizuri kapiga koti na suruali huyo na kandambili zake kazama kitaa.
Mjomba tulikua na mastory sana yani dah,
Sa hivi na mimi mjomba tena.
No 3
Hawa Brothers walikua masela tu hapo Dom (Kaudo) truckers miaka hiyo.
Mi mdogo jioni home wanawake wamejaa ikiwa mda twenzetu dogo au utabaki na hawa wanawake?
Maana ilikua makelele tu.
Basi hao kwenye vibanda vya gongo kule makole,iringa road.
Aloo ule mziki jamaa wakilewa wakiuanzisha ni balaa.
Hapo mi napewa walet tangulia home.
Nakimbia hadi home.
Dah jamaa wanarudi badae wanahema tu kwa mbio🤣🤣🤣.
Wanaanza kupiga story matokeo kule.
Hawana hata abari wanacheeka,
sikuwai kuona polisi wala kesi pale home
Walimaliza mambo yao hukohuko.