Huwaga kuna yule mjomba ni mlevi tangu umezaliwa

Huwaga kuna yule mjomba ni mlevi tangu umezaliwa


- Mara nyingi historia yake huwa na mafanikio kabla hajaanza ulevi, mfano utaambiwa alikuwa ana akili sana darasani, alikuwa hakosi kanisani, alikuwa mfano kwa vijana wengine, n.k.

- wanazijua siri nyingi sana kuhusu familia, anayajua mengi kumhusu dada yake (mama yako)

- Kila mwaka utasikia nusu afe

- huwa hawaoi au walishaachwa

- maisha yake yapo kwenye auto pilot ni ngumu kuelewa ana survive vipi ila ana survive

- yupo peace, mshauri mzuri, hana makuu, ila haheshimiki sababu hana hela

- kazika marafiki wengi na bado ana marafiki kibao

- huwa wana pair moja ya viatu

- hubaki kijijini kuwakilisha familia kila mtu akirudi mjini, husafisha mazingira, kulisha mifugo

- sio mlalamikaji, karidhika na maisha yake hata anapokosa msaada wa ndugu zake
Haha sijui umefikiria nini ila ni ukweli mtupu na mara nyingi huwa ndio last born katika familia ya kina mama zetu
 
Mjomba anamiliki real estate na mafremu ya kutosha yeye maisha yake hatengemei kikokotoo, kiinua mgongo au malipo ya pensheni ya nani sijui, nyumbaani kwake ukifika huamini ukiaambiwa huyu ndio mwenye mji huu, utawauliza mara 2 maana utahisi km unataniwa tu kumbe ndio unaambiwa ukweli
 
Back
Top Bottom