Huwaga kuna yule mjomba ni mlevi tangu umezaliwa

Huu utamaduni wa kurithishana majina ya babu siupendi aisee,sema bas tu nishapewa hili jina.
Babu yangu alikua mtu mzurii sana sanaa/ Huwa ni respect mashangazi na baba zangu wakubwa kwa wadogo Huwa Wana ni respect kama baba YaoπŸ˜†πŸ˜Š

Katika woteeeeeee walio itwa Hilo jina Mimi pekee ndie ninaliishi jina la Babu mzaa baba zetuu wengine wotee watatu ni mizinguo kama mjomba alie elezewa..
 
Hongera kwa hilo mkuu..huu utamaduni upo sana kule kwetu songea,Mbinga..ni kurithishana majina tu. Mtoto wa kwanza kama wa kiume anachukua jina la babu mzaa baba..kama wa kike jina la bibi mzaa baba.

Mtoto wa pili kama wa kiume jina la babu mzaa Mama,kama wa kike jina la bibi mzaa Mama.
 
Hii ipo sana hata kaskazini na hata lake zone..

Mimi mwenyewe nime apply tena mama huyu binti yangu wa kike ni jina la kwake ana alitoa yeye mwenyewe 😊😊😊
 
Mmoja rafiki yangu sijui km mzima yule.
Yes alisoma hadi Makerere huko miaka hiyo ya 70, alirudi kijijini akawa chizi.
Mara ya mwisho kuonana nae aisee kala pamba kali sana namuuliza we uchizi vp tena akanambia ile njaa tu mjomba,
Alikua kauza shamba na kuhama pale kijijini kabisa.
Mwingine huyu alipigana huko Burma vita ya pili ya dunia alivyorudi akapigika huko kijijini mda tu.
Mdingi ndo alikua mjomba wake akaona isiwe tabu kaenda kamleta home akae, ana upande wake huko pembeni nyumba kubwa ilikua ni kupiga menyu tu.
Yule mzee alikua peace sana yaani pale home wala jirani hajawai kuzingua.
Maza tena leo ntamkumbusha nilishamsahau.
Maana walikua marafiki wakianza kupiga mastory na kiingereza chao utapenda.
Huyo Mwamba kila jioni akienda vilabuni kupiga vyombo😁, analianzisha e bana anapiga kilabu walevi woteπŸ˜…πŸ˜…πŸ˜….
Ila sasa akitoka baru hakimbilii nyumbani anaweza kupita home mbio huku anakimbizwa na walevi wenzie.
badae anarudi gheto kwake
Anatulia ka sio yeye
Alikufa yule,
Dingi nae walikua hamna story nyingi Watasalimiana kila asubuhi ataachiwa kilinda mfuko basi,ukiona tu anapiga pasi nguo zake ujue huyo anaenda sebuleni.(kilabuni)
Jambo namsifu usafi.
Hapo alikua 100%.
Kuna siku shati moja jeupe limechanika mgongoni lakini kakomaa nalo kalinyoosha vizuri kapiga koti na suruali huyo na kandambili zake kazama kitaa.
Mjomba tulikua na mastory sana yani dah,
Sa hivi na mimi mjomba tena.
No 3
Hawa Brothers walikua masela tu hapo Dom (Kaudo) truckers miaka hiyo.
Mi mdogo jioni home wanawake wamejaa ikiwa mda twenzetu dogo au utabaki na hawa wanawake?
Maana ilikua makelele tu.
Basi hao kwenye vibanda vya gongo kule makole,iringa road.
Aloo ule mziki jamaa wakilewa wakiuanzisha ni balaa.
Hapo mi napewa walet tangulia home.
Nakimbia hadi home.
Dah jamaa wanarudi badae wanahema tu kwa mbio🀣🀣🀣.
Wanaanza kupiga story matokeo kule.
Hawana hata abari wanacheeka,
sikuwai kuona polisi wala kesi pale home
Walimaliza mambo yao hukohuko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…