Huwezi amini kwamba hawa nao ni wasomi wa UDSM wanasaka degree

Huwezi amini kwamba hawa nao ni wasomi wa UDSM wanasaka degree

siyo kweli bhana... hii picha ya longtime kitambo kama miaka mitatu hivi iliyopita
aliyeileta naye hajaifanyia uchunguzi, walikuwa wanashoot movie ambayo haijatoka mpaka sasa
 
The universities of great thinkers are muhas, St.joseph only bt not udsm.
This is my own thoughts
 
Kuna siku ataingia mwanafunzi darasani bila suruali halafu "great thinkers" watailaumu serikali...
 
Mdau tuwekeee photo za kutosha toka hapo hostel za lifestyle hasa night. Kwa ufaham wangu hii ni trela tuu, things are worse than this. Kwan hizo meza kama hiyo ya kushoto siyo vitanda cku hizi?
 
Hayo ni machache, mengi yapo kama kulala chini, kula ukoko n.k/ Kuhusu wanafunzi kutafuta kazi kwa muda wa ziada ni ngumu maana ajira za aina hii ni ngumu katika Jiji hili kwani hata wahitimu wenyewe hawana kazi.
 
kutoka Mabibo Hostel:

View attachment 85821


inasikitisha sana na kuhuzunisha kuona watoto wa wakulima wanaotafuta shahada ya elimu ya juu (university) ndani ya chuo bora kabisa Tanzania na Africa kwa ujumla

Halafu eti unategemea hawa 'wasile rushwa' na 'uiba fedha za umma'wakishapata kazi..
 
my take:
ni aibu kwa kwa serikali,chuo kikuu cha dar es salaam (UDSM) na wasomi wote waliopo na waliowahi kupitia chuo kikuu cha dar es salaam (UDSM)
Si shangai kwa unachoandika kwa sababu kujiunga JF it does not take more than 2 minutes na hakuna aptitude test ndiyo maana tuna kila aina ya watu.
Sikubaliani na wewe jinsi ulivyotumia hiyo picha kulaum serikali,uongozi wa chuo na kusema ni aibu wa wanaosoma udsm na waliowahi kusoma udsm."Sometimes it is better to be quite because when you start talking or writing posts you give information about who you real are".
Information nilizopata kuhusu wewe kutokana na post yako ni
1.Inawezekana ulisoma udsm ukadisco au hujawahi kusoma hapo ila ulikuwa unapenda sana usome hapo
2.Udsm inaonekana walikufanyia kitu ambacho hukupenda maishani mwako
Nikirudi kwenye picha yako,sijui o-level ulisoma shule gani,ila shule nyingi ktk Geography form3 au 4 kuna somo la map and photograph interpretation,nahisi kama ulikuwa unakimbia vipindi.uwezo wako wa kuextract information kutoka kwenye picha samahani kusema nauona ni mgodo.
Nikirudi kwenye picha
1.Hicho chumba kina vitanda double deck2,jumla kulala ni watu wanne,inamaanisha magodoro yanatakiwa kuwa manne hapo yanaonekana magodoro mawili,umejiuliza ni kwa nini?
2.Unapofika chuo ukilipia chumba(accomodation) unapewa receipt unaenda nayo kwa warden anakupa funguo za room na godoro(kama godoro halipo chumbani).Hao jamaa kwenye picha wako watatu na godoroni moja ,wewe hapo umejifunza nini kama great thinker(if and only if you are one).Hawajalipia pesa za kukaa hapo walipo,kama wangekuwa wakazi halali wangeenda kuomba magodoro.
3.Inawezekana hicho ni kipindi cha likizo watu hawapo chuo,washikaji wamebaki ili wabakiwe na pesa amelipia mmoja na wengine ndiyo kama hivyo.
Kuhusu swala lako la watu kufanya part time wakiwa chuoni,sijui kama unaelewa ratiba ya vipindi ikoje si kila mtu anaweza fanya part time,na pia sijui foleni za dar unazijua au unaongea.unaweza enda kwenye part time alafu ukakwama kwenye foleni,si utamiss vipindi.
Angalia hapo red highlighted,shule au vyou wanafunzi wanakuwepo kwa muda maarum ukimaliza course unaondoka chuoni,sijakuelewa kwa nini iwe aibu kwa waliosoma hapo zamani "what is the connection?".
Vyuo vipo vingi na vizuri tu na kila chuo kina uzuri wake na mapungufu yake,jitahidi usionyeshe hisia zako kuhusu chuo fulani.
Usiwapotoshe watu kwa kutaka ilaumiwe serikali au uongozi wa udsm,katika uliyoandika swala la majengo kutokuwa na feni hilo sawa the rest is garb***
Read between kines,dont take it personal,think before you post.
Regards
Aqua
 
Hii sasa inaharibu ubora wa Jamii Forum. Pamoja na matatizo ya malazi kwa wanafunzi wa vyuo vikuu hapa nchini hasa UDSM, mabibo hostel kuna magodoro 300 ya akiba kwa aajili ya kukidhi dharura ya aina yoyote, pia hakuna kitanda kinachokwa wazi labda awe mwenye nafasi hiyo hajafika maana kimsingi lazima kiwe kimepangiwa mtu. Mwisho vitanda vya mabibo hostel unavijua au umeambiwa? Tafuta nafasi umuone Meneja wa malazi au rafiki au yeyote anayeishi Mabibo akupeleke upaone hali halisi ya madirisha, vitanda, magodoro na mazingira yake. Hivyo uongo uliowekwa hapa uondolewe maana wanaolala humo wanakuona kituko.
 
Hii sasa inaharibu ubora wa Jamii Forum. Pamoja na matatizo ya malazi kwa wanafunzi wa vyuo vikuu hapa nchini hasa UDSM, mabibo hostel kuna magodoro 300 ya akiba kwa aajili ya kukidhi dharura ya aina yoyote, pia hakuna kitanda kinachokwa wazi labda awe mwenye nafasi hiyo hajafika maana kimsingi lazima kiwe kimepangiwa mtu. Mwisho vitanda vya mabibo hostel unavijua au umeambiwa? Tafuta nafasi umuone Meneja wa malazi au rafiki au yeyote anayeishi Mabibo akupeleke upaone hali halisi ya madirisha, vitanda, magodoro na mazingira yake. Hivyo uongo uliowekwa hapa uondolewe maana wanaolala humo wanakuona kituko.

Kweli mkuu hii itakuwa UDOM tu bila shaka.
 
Yaani hiyo hali ni mateso bila chuki;yaani elimu ya bongo kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu ni shida tuuuuuu hadi lini?Kwa mazingira kama hayo kwanini watu wasiandamane na kufeli pia kunafatia.
Hiyo inaonyesha utawala ni mbovu kuanzia chini hadi juu.
 
angalia hilo dirisha upande wa kushoto
angalia hiyo meaza ndefu nyeupe
angalia hito chata/nembo kwenye kitanda ambayo inasomeka vizuri kwamba

UDSM/MAB/HOST/.......

Picha hii ni halisi na imechukuliwa jana tarehe 5/3/2013.
mwenye macho haambiwi tazama.

ebwana ni kweli kabisa,nimesoma
 
Ukisoma UDSM unatakiwa kuwa flexible ili ufit popote coz lfe la pale ni la kibishi,ndo maana mboga nane wanaenda St.,..
 
Mbona hakuna cha ajabu katika hiyo picha?! Kulala mzungu wa pili mlimani imeanza miaka mingi sana, na inaendelea mpaka sasa, na itaendelea sijui mpaka lini!! Labda huyo wa juu kutokuwa na godoro! Wote hatujui kama aliamua kuliondoa mwenyewe kwa sababu zake binafsi, au kuna tatizo. Nakubaliana na wale wanaosema pengine kabebwa, na mwenye chumba hajafika. Hivyo, hakuna la ajabu hapo, mmewaanika bure tu wasomi wetu!
 
Acha kuongeza idadi ya thread wewe, hao vijana hawajalipia bado kodi za vyumba na hii ilitokana na kuwahi mjini kusign hela ya kujikimu but wonderful enough ikachelewa kidogo......acha maneno ya kinafiki ya kukichafua chuo kwa hila zako binafsi....tutakutafuta pumbaaaaaaaf wewe...
 
WAMEJITAKIA wenyewe hao.kama waliandamana waongezwe japo elf ya kujikimu je kwa KULALA kwenye FLAT BAR?
 
Nimeishi hapo miaka mitatu, sio mabibo hiyo.
hii picha iliandaliwa kupigwa,huyo wa juu akatoa godoro....nimeishi mabibo godoro nyingi sana na mpya kila mwaka zilikua zinaingia....kama ni kweli hakutoa godoro basi hajalipa ada ya hostel ndio maana hana godoro.
 
Bila shaka hawa jamaa walikuwa hawajalipia hicho chumba hivyo hawakuwa wamepewa magodoro. Kumbuka mwanafunzi anapopangiwa chumba anaweza kuchonga funguo hivyo wanaweza kuwa waliingia chumba hicho isivyo harali. Pili kama mmoja wao alilipia chumba na kupewa godoro huyo mwingine ameomba msaada apate pa kujishikiza



UDSM inamapungufu mengi lakini si kukosa magodoro. LICHA YA HIYO KUNA TATIZO KUBWA LA UCHACHE WA VYUMBA
 
Back
Top Bottom