Wewe sasa ndo zuzu kabisa, kuwa wa kwanza kuunda vitu haimanishi huwezi kupitwa, china ashaanza unda ndege za abiria ila mpaka upewe kibali cha kuanza kuziuza kwa ajili ya usafirishaji kuna mchakato unapita, na unachukua miaka.
Ndehe za kivita ndo sasa katoa generation ya ndege zake ambazo wanasema ni superior kuliko hata ndege za kirusi.
China ndiyo nchi pekee duniani inayomiliki space station.
Ukitoa Marekani, na Urusi, China ndiyo one man show aliyeshusha vifaa mars. Hizo nchi za ulaya wana agency ya anga moja wanashirikiana.
Space station nyingine wanashirikiana russia, US, na nchi za ulaya.
Kwa roho mbaya ya marekani akataka wasimpe ruhusa china kuitumia hiyo space station, mchina akaona isiwe tabu ngoja nitengeneze yangu, na anayo na anazidi kuitanua iwe the biggest station huko angani.
Steve jobs aliwahi kuulizwa kwanini wanapenda kufanyia production china, jibu lake lilikuwa china ndo nchi ambayo ukitaka skilled labor ya watu wanaojua kitu flani, watajaa stadium, wakati US hawajai hata meza.
Speed ya China ya mabadiliko katika muda mfupi inatisha ni mabadiliko ya muda mfupi sana.
China ndiye mwenye train zenye speed kuliko train ya nchi yoyote, nadhan unajua kuhusu maglev technology, train inayoelea kwenye reli na kukimbia speed ya bullet.
US sasa anaigopa china ndo maana anahangaika na vikwazo kuipunguza speed navyo vina matokeo ya muda mfupi.
Huawei baada ya kuwekewa vikwazo, soon wanataka kuanza kuzalisha vifaa wenyewe kwa ajili ya electronics.
Kuna kampuni inadeal na mambo ya quantum computing mwaka jana imepata breakthrough, US kwa uoga kuwa ikifanikiwa inaweza hack na kubreak security zake kaipga vikwazo wakati ana makampuni kibao yanafanya research ya quantum computing.
Bado silaha, kala mfuatiliaji mwishoni mwa mwaka jana katest kifaa kikaenda into space kikarudi kwa speed kali sana lakini bado kikawa maneuvered kutua. Wataalam wa US wakashangaa maana hawana kifaa kama hicho, kifaa chochote kikiwa kwenye high speed from space kwenye reentry huwezi kukimaneuver kwa technology walionayo, iliwashangaza mchina kufanya hivyo. Na walikuwa hawajui ni kifaa cha kubeba wanaanga au silaha.
Baadae wanakuja kugundua ni kwa ajili ya vyote, inaweza tumika kubeba silaha au ikatumika kama rocket ya kupeleka vtu space.
Mchina anatengeneza drones, tena advanced drones za ulinzi.
It is a matter of time wale jamaa ni unstoppable.
Nawaogopa sana maana wakishakaa pale top kabisa wakatulia hii dunia itapata shida sana maana ni wanyonyaji haswa.