Sijui nikuite Punguani au Layman?
Bila NATO Urusi ataifanya Nini Marekani?
NATO ina jumla ya Wanajeshi 450,000. Kati ya hao Wanajeshi wa Marekani ni 370,000. Nchi 29 zilizobaki Zina Wanajeshi 80,000 ndani ya NATO.
NATO ina Aircraft Carrier 27. Kati ya Hizo 22 ni za Marekani. Nchi 29 zilizobaki Zina Aircraft Carrier 7 tu.
NATO ina Combat Tanks 27,000. Kati ya Hizo, 19,000 ni za Marekani. Nchi 29 zilizobaki kwa pamoja Zina Combat Tanks 8,000.
Bajeti ya NATO kwa mwaka ni $ 1,019,000,000,000.($ 1.019T). Kati ya Hizo, $ 760,000,000,000 ni za kutoka Marekani. Nchi 29 zilizobaki zinachangia Nusu ya Marekani kwa pamoja $ 300,000,000,000.
NATO ina Jumla ya Nuclear Waepons 7,200. Kati ya hizo, 6,500 ni kutoka Marekani. Nchi zingine 29 kwa pamoja Zina Nuclear Waepons 700 tu.
NATO ina Jumla ya Fighter jets 3,500. Kati ya Hizo, 2,700 ni Kutoka Marekani. Nchi zingine 29 zinachangia Jumla ya Jets 800 tu.
Huwa mnaposema sijui eti Marekani bila NATO hawezi kupigana wakati mnajua kabisa Marekani ndio NATO kwenye Kila Kitu,bila Marekani hakuna NATO.
Lengo la Marekani kwenye NATO sio kutafuta Support ya nchi za Ulaya Kijeshi bali ni Hofu ya Marekani kwamba Urus atazimeza nchi za Ulaya Mashariki tangu USSR kusambaratika. Ndio maana kwenye huu mgogoro wa URUS na UKRAINE,Mataifa madogo ya Ulaya Mashariki Kama LATVIA,LITHUANIA,ROMANIA na ESTONIA ambao ni wanachama wa NATO wameiomba Marekani iongeze Wanajeshi wake kwenye Mataifa hayo na Siraha nzito ili kuyalinda dhidi ya Urusi.
Ndio Maana Marekani imeahidi kwamba endapo Urus itaivamia Ukraine kijeshi basi Marekani haitatuma Wanajeshi wake kwasababu Ukraine sio Memba wa NATO. Lakini ikaahidi Urus itajutia kitendo chake make Marekani itaongeza idadi ya vikosi vyake na Siraha nzito kwenye Mataifa ya Ulaya Mashariki ili kuyalinda dhidi ya uvamizi wa URUS. Ndio Maana mpaka Sasa Putin kagoma Kuvamia Ukraine.