Huwezi amini Wazungu ndio wanalisha Hoteli za Kitalii Tanzania, Hii aibu kuu

Huwezi amini Wazungu ndio wanalisha Hoteli za Kitalii Tanzania, Hii aibu kuu

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2011
Posts
7,872
Reaction score
9,263
Hivi tunalima products zipi hasa? Make Hoteli za kitalii nyingi zinalishwa na Wazungu, kule Njombe kuna Wazungu kule wanalima kila aina ya Mboga ambazo husapply Arusha, Dar na Zanzibar.

Arusha kuna Wazungu, kuna wenye Mashamba kule West Kilimanjaro, yale mashamba yalio kuwa ya TBL wakilima shayri, wale wanalima balaaa tupu na wana offisi zao pale Arusha mitaa ya jirani na kiwanda cha Bia, wana lisha Hoteli nyingi sana za Arusha, na Polini, huwa nawauziaga netti fulani hivi hivyo natimbaga sana offisini kwao na huwa nasikitika sana.

Hilo shamba lao ni ni hekari 1000+ ni kubwa mno kwa kifupi.

Sisi tunazalisha products zipi hasa, au ni hizi za kuuziana sisi Kibongo bongo?

Hawa wazungu some time hata wanatudharau wako sahihi kabisa kwa asilimia 100 kama wanakuja na wanalima na wanalisha Mahoteli ya Kitalii na Camp whay sisi? hii ilikuwa ni kazi yetu ila hatuwezi.

Hio picha nilipiga mwenyewe kwenye offisi zao Arusha, na hizo Products zinatoka West Kilimanjaro.

Kuna haja ya kujiuliza tunalima nini hasa sisi?
IMG_20230111_092304.jpg
 
Wazungu wanapewa kila aina ya msaada na serikali. Lakini ukweli ni kwamba Watanzania na serikali yetu hatujipanga kuilisha Tanzania au kuwa serious na kitu chochote cha msingi.

Ni Bora tuwa-support hao wazungu walime kisasa.
 
Sapoti ipi hatupewi? Make kilimo ni Biashara sawa na unavyo weza fungua Hoteli, Car wash, Guest House na kadhalika, kwani hizo biasjara hapo huwa kuna Sapoti unapewa na Serikali? Wale sijaona sapoti wanayo pewa zaidi ya wao kulima na wana wafanya kazi wao, wameajiri mwa bwana shamba na Bib Shamba
 
Aione Bashe Na Farming Blocks Zake Ambazo Mwakani CAG Atatupa Hasara Yake Hapo Chinangali II Dodoma Tanzania
Hivi zile Block zinalima nini hasa? Yaani wanazalisha mzao gani pale? Make sina info za kutosha kuhusu Blocks
 
Hivi tunalima products zipi hasa? Make Hoteli za kitalii nyingi zinalishwa na Wazungu, Kule Njombe kuna Wazungu kule wanalima kila aina ya Mboga ambazo husapply Arusha, Dar na Zanzibar.

Arusha kuna Wazungu, kuna wenye Mashamba kule West Kilimanjaro, yale mashamba yalio kuwa ya TBL wakilima shayri, wale wanalima balaaa tupu na wana offisi zao pale Arusha mitaa ya jirani na kiwanda cha Bia, wana lisha Hoteli nyingi sana za Arusha, na Polini, huwa nawauziaga netti fulani hivi hivyo natimbaga sana offisini kwao na huwa nasikitika sana.

Hilo shamba lao ni ni hekari 1000+ ni kubwa mno kwa kifupi,

Sisi tunazalisha products zipi hasa, au ni hizi za kuuziana sisi Kibongo bongo?

Hawa wazungu some time hata wanatudharau wako sahihi kabisa kwa asilimia 100 kama wanakuja na wanalima na wanalisha Mahoteli ya Kitalii na Camp whay sisi? hii ilikuwa ni kazi yetu ila hatuwezi.

Hio picha nilipiga mwenyewe kwenye offisi zao Arusha, na hizo Products zinatoka West Kilimanjaro.

Kuna haja ya kujiuliza tunalima nini hasa sisi? View attachment 2604810
Njombe sehemu gani wazungu wanalima mboga? Mm nipo huku sijawahi Ina hao wazungu wanalima hizo mambo 😃😃 labda ungeweka picha zao
 
Exposure gani wakati tunalima ndani ya nchi na kuuzia ndani ya nchi? İna maana kulima products za kuuza hasa kwenye hoteli tunahitaji Exposure? Mtaji sh ngapi?
Jaribu set up 3 acres weka irrigation....weka hoho...nyanya bilinganya na kitunguu ....ah nyanya chungu ....mtafute soko....baada miezi 6 rudi tuongee zaidi ...supply supermarket hotel unatakiwa uwe contact supply mwaka mzima ....ndio maana unasikia acre 1000 amezigawa.....vizuri awe contact supply ....maintained quality ....ukileta ushabiki sawa.....
 
Nini kinashindikana? Hamuwezi ungana? Hakuna kinacho shindikana sema tume invest kwenye kulalamika sana, sioni kisicho wezekana, Costant supply ni muhimu yes, huwezi peleka mzigo leo then wiki ijayo ukasema hauna.

Wao wana mashanba makubwa ok ni sawa je sisi tunashindwa kuunganisha haya yetu? Shida iko hapo
 
Sisi tunalima kienyeji Sana, wao wanakula kitu kilichotoka kwenye green house halina contamination na wadudu wa aina yeyote
Sio product zao zote ni za green house mkuu, wanalima sana Oppeni field, na oia kwa kuzidiwa na mzigo huwa wana nunua kwa local ila sasa sisi local full usaniiii mwingi mno, yaani asilimia 90 ni usanii, ila si kwamba hatuwezi lima hio quality tunaweza sema hatujajipanga na hatuko serious
 
Back
Top Bottom