Huwezi amini Wazungu ndio wanalisha Hoteli za Kitalii Tanzania, Hii aibu kuu

Huwezi amini Wazungu ndio wanalisha Hoteli za Kitalii Tanzania, Hii aibu kuu

Hivi tunalima products zipi hasa? Make Hoteli za kitalii nyingi zinalishwa na Wazungu, Kule Njombe kuna Wazungu kule wanalima kila aina ya Mboga ambazo husapply Arusha, Dar na Zanzibar.

Arusha kuna Wazungu, kuna wenye Mashamba kule West Kilimanjaro, yale mashamba yalio kuwa ya TBL wakilima shayri, wale wanalima balaaa tupu na wana offisi zao pale Arusha mitaa ya jirani na kiwanda cha Bia, wana lisha Hoteli nyingi sana za Arusha, na Polini, huwa nawauziaga netti fulani hivi hivyo natimbaga sana offisini kwao na huwa nasikitika sana.

Hilo shamba lao ni ni hekari 1000+ ni kubwa mno kwa kifupi,

Sisi tunazalisha products zipi hasa, au ni hizi za kuuziana sisi Kibongo bongo?

Hawa wazungu some time hata wanatudharau wako sahihi kabisa kwa asilimia 100 kama wanakuja na wanalima na wanalisha Mahoteli ya Kitalii na Camp whay sisi? hii ilikuwa ni kazi yetu ila hatuwezi.

Hio picha nilipiga mwenyewe kwenye offisi zao Arusha, na hizo Products zinatoka West Kilimanjaro.

Kuna haja ya kujiuliza tunalima nini hasa sisi? View attachment 2604810
Mkuu kaa mkao wa kula, kuna mwekezaji wa kuku alisema anataka kuja wekeza Tz... hili tamko lilitolewa na serikali alipokuja makamu wa rais wa USA.
 
Mleta hoja mbona tena majibu unatoa mwenyewe! Ni kama unaandika utafiti ambao findings unazo, sio utafiti sasa!

Well,
Kimsingi kanuni ya soko inasema “produce for the market” !

Sasa ili uzalishe kwa ajili ya soko kwa maana ya zalisha kile ambacho soko linataka unapaswa kujua kua soko linataka nini? Kwa maana ya market research iwe ya kutosha ili ujue kumbe hoho nyekundu zinatakiwa kwa kiasi fulani na nani na sio ulime ndio utafute soko.

Je value chain au mnyororo wa thamani wa zao hilo unauelewa kuanzia pembejeo mpaka masoko na wadau wake.

Je unao mtaji unaohitajika ukiambiwa utatakiwa kwa wastani u supply tani kadhaa kwa mwaka utaweza?

Vipi teknojia umejiandaaje ambayo pia inategemea mtaji wako!

Vipi unajua sheria kanuni na taratibu zinazoongoza uzalishaji huo?

Network yako ya wadau iko strong ie kwenye masoko etc..

Tuanzie hapo…..
 
Exposure gani wakati tunalima ndani ya nchi na kuuzia ndani ya nchi? İna maana kulima products za kuuza hasa kwenye hoteli tunahitaji Exposure? Mtaji sh ngapi?
Mkuu elewa mfumo wa nchi jinsi ulivyo,huku kwetu tunalima ufuta,ilipofika muda wa kuuza tuliuza 1500kwa kilo badala ya 3000,mnunuzi alienda kuuza Dar 6000kwa kilo Tena mulnunuzi Ni mwanasiasa mkubwa ambae alitakiwa atusimamie tupate pesa badala yake ametupiga who cares??

Mimi nilime ekari 10 za mbogamboga so what? Kama Sina exposure nikatafuta soko mjini zitaozea shambani tu!!
 
Madili kama hayo huwezi sikia kwenye mtandao ndio maana nasema dili za pesa hazizagai mtandaoni. Na wabongo tunalawama sana kama una mtaji wa kulima heka 1000+ za mboga si utafute soko upige kazi kumlaumu mzungu alietoka kwao na kuonanfursa hapa ni upopoma
 
Same as ufuta mikoa ya kusini, ilikua na soko cha ajabu wananchi wakawa wanaweka mchanga katikati ukipima uzito unaongezeka! Ikaondoa trust ya dealers!
Shida huanzia hapo, hata tumbaku walikuwa wanaweka mawe, na maana mtu anapima kilo nyingi baadaye wakienda huko wanakuta mawe kilo zinapungua wanaanza kulalamika kumbe shida ipo kwao, yaani sijui shida huwa ninini! Kutokuwa na elimu au akili za kuzaliwa ni shida[emoji53]
 
na majeans wanapaka mafuta?mi nilifikiri ni mchele tuh hupakwa nafuta mkuu
Jamani mchele unamafuta mpaka unajisikitikia huku unanunua, mwanzo nilikuwa najiuliza huu mchele vipi nikajua bahati mbaya nikamfuata mfanyabiasha mmoja akaniambia sio bahati mbaya daa afya zetu ni kwa huruma ya mwenyezi Mungu
 
Jamani mchele unamafuta mpaka unajisikitikia huku unanunua, mwanzo nilikuwa najiuliza huu mchele vipi nikajua bahati mbaya nikamfuata mfanyabiasha mmoja akaniambia sio bahati mbaya daa afya zetu ni kwa huruma ya mwenyezi Mungu
karoti wanaosha na sabuni za unga mara mchele waweke mawe makusudi kuongeza kilo, mtu unaingia nae biashara mfano kila siku saa 11 alfajiri akulete maziwa lita 2500 na ana jipambanua kabisa anauwezo mara unaenda vizuri katikati ananza dharula zisizo na msingi matokeo yake anakurudisha nyuma kumbe unakuta anauza sehemu nyingine nje ya mkataba wako nahaweki wazi kwamba sasa biashara na wewe basi.
 
Back
Top Bottom