Huwezi amini Wazungu ndio wanalisha Hoteli za Kitalii Tanzania, Hii aibu kuu

Huwezi amini Wazungu ndio wanalisha Hoteli za Kitalii Tanzania, Hii aibu kuu

Mkuu elewa mfumo wa nchi jinsi ulivyo,huku kwetu tunalima ufuta,ilipofika muda wa kuuza tuliuza 1500kwa kilo badala ya 3000,mnunuzi alienda kuuza Dar 6000kwa kilo Tena mulnunuzi Ni mwanasiasa mkubwa ambae alitakiwa atusimamie tupate pesa badala yake ametupiga who cares??

Mimi nilime ekari 10 za mbogamboga so what? Kama Sina exposure nikatafuta soko mjini zitaozea shambani tu!!
Exposire ipi? Ulimuuzia kwa hiari yako huo ufuta ay alikushikia bunduki? Kama ni bunduki hapo kuna tatizo kubwa ungereport
 
Ekari 1000+? Siyo kweli.

Uzuri ni kwamba nawafahamu sana hao wazungu wa Simba Farm na historia ya shamba hilo nalijua.

Wana green house kadhaa na wanafanya open farming ya ekari ambazo kwa idadi hazifiki hata 100.

Kuhusu kulisha hoteli za Watalii nadhani ni Commitment. Wao wanalima muda wote wa mwaka. Na mazao shambani kwao yanatoka kama ambavyo order yao inasema kutokana na mikataba baina yao na hoteli husika.

Ni nadra kuwapata Wabongo wanaozalisha kipindi chote cha mwaka kwa kiwango na ubora unaotakiwa na hoteli husika.

Mtanzania anataka alime msimu mmoja na hoteli husika ziwe ndiyo wateja wake. Hiyo haipo.
 
Hivi tunalima products zipi hasa? Make Hoteli za kitalii nyingi zinalishwa na Wazungu, Kule Njombe kuna Wazungu kule wanalima kila aina ya Mboga ambazo husapply Arusha, Dar na Zanzibar.

Arusha kuna Wazungu, kuna wenye Mashamba kule West Kilimanjaro, yale mashamba yalio kuwa ya TBL wakilima shayri, wale wanalima balaaa tupu na wana offisi zao pale Arusha mitaa ya jirani na kiwanda cha Bia, wana lisha Hoteli nyingi sana za Arusha, na Polini, huwa nawauziaga netti fulani hivi hivyo natimbaga sana offisini kwao na huwa nasikitika sana.

Hilo shamba lao ni ni hekari 1000+ ni kubwa mno kwa kifupi,

Sisi tunazalisha products zipi hasa, au ni hizi za kuuziana sisi Kibongo bongo?

Hawa wazungu some time hata wanatudharau wako sahihi kabisa kwa asilimia 100 kama wanakuja na wanalima na wanalisha Mahoteli ya Kitalii na Camp whay sisi? hii ilikuwa ni kazi yetu ila hatuwezi.

Hio picha nilipiga mwenyewe kwenye offisi zao Arusha, na hizo Products zinatoka West Kilimanjaro.

Kuna haja ya kujiuliza tunalima nini hasa sisi? View attachment 2604810
we mwenyewe umelima hata ekari moja? ni ya zao gani.
 
Back
Top Bottom