Huwezi kuchukua nchi bila SYSTEM kuwa upande wako

Huwezi kuchukua nchi bila SYSTEM kuwa upande wako

Unamfahamu mtu mwenye mamlaka ya kuteua wakuu wa vyombo vya dola?
Fuatilia pia utoaji amri na utimizaji wake vyombo vya dola.
Hoja ya msingi, kujenga imani kwa vyombo vya dola ni muhimu sana. Kanuni muhimu ya maisha hata adui anapenda kuonyeshwa unamjali na upendo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wafanye kazi na TISS? Umesahau ya Abdulrahman Kombe?

Siku zingine acha Kukurupuka Kuyataja Majina ya Watu kama unajua huyajui vizuri au hujajiridhisha nayo. Umejichoresha sana!
 
Shida ni ccm, ikifa hakuna cha tiss wala nani.


..masuala ya system kuwa against upinzani mimi nadhani ni kukatishana tamaa na kutishana tu.

..Ushindi ktk uchaguzi unapatikana kwa kuweka mgombea mzuri / wagombea wazuri, kuwa na a good and inspiring campaign message, na la mwisho ni kufanya kampeni ya nguvu na kuwa more organized kuliko unayeshindana naye.

..Kuna watu walikuwa hawaamini kwamba Wamarekani wanaweza kuchagua mtu mweusi. Walikuwa na imani hizihizi kwamba kuna an " invisible hand " / system itakayomzuia mtu mweusi.

..But what happened alipopatikana mgombea mweusi ambayo alikuwa na sifa tatu ambazo nimezielezea hapo juu?

..Wapinzani waweke mgombea ambaye atamzidi mgombea wa ccm kwa hoja. Pia wawe na ilani nzuri ya uchaguzi na mgombea wao awe na uwezo wa kuitetea. Mwisho mgombea awe na stamina ya kufanya kampeni kumzidi mgombea wa ccm.

..Mgombea wa Uraisi wa upinzani ana mchango mkubwa sana ktk kuwabeba wagombea wa ubunge. The two campaigns have to be coordinated and in sync.
 
Asee sijui unatumia akili gan hivi unaijua siasa na utawala wewe
leo umewaza mbali sana kuleta wazo kma hili, ila siyo lazima viwe upande wako pale ambapo kuna demokrasia ya kweli, kumbuka Ivory Coast, jamaa alikuwa na vyombo vya usalama pmja na jeshi lote nyuma yake, lakini wananchi waliamua...Tunisia, Misri ni mifano tu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
..mgombea wa upinzania anatakiwa amfunike yule wa ccm.

..hilo likitokea hicho mnachoita " system " kitakuwa haina jinsi zaidi ya ku-lineup nyuma ya mgombea aliyeshinda.

..kama "system" ya makaburu iliweza kumlinda na kumtii Mzee Mandela, sioni kwanini "system" ya hapa Tz ishindwe kumtii mpinzani.
 
Labda watakuelewa kwa vile mwenzao.

All in all hongera kwa mara ya kwanza umetoa ushauri mzuri sana.
 
Chadema mnapofanya siasa zenu tambueni kuwa ni ngumu kuchukua nchi bila kufanya urafiki na vyombo vya ulinzi na usalama. Either mtatumia umwagaji damu, Vyombo vya ulinzi ndio watanzania wenyewe ukiona umekubalika 50% kwa watanzania na ndani ya ulinzi ndio hivyo hivyo, maafisa wa vyombo wanataka kujilidhisha na sera zenu juu yao.

Hivyo wapinzani mnapotaka kufanya siasa msijitenge na vyombo kama Police, TISS na JWTZ ni ushauri wangu tu wa leo kuvishutumu vyombo vya ulinzi mala kwa mala mtajenga kutoaminika kupewa nchi ndio maana wanawasumbua sana maana wanajuwa mkiingia mtawageuka na kuwachukulia hatua. Siasa imebadilika vyombo vya usalama ni muhimu ili kwenda hasa ikulu.

Ili jambo litaponza upinzani miaka mingi sana na tutachelewa kuondoa mfumo mbovu wa taifa endapo upinzani hautabadilika na kuwa upinzani wa sera za mageuzi na sio lawama kwa vyombo vya usalama siasa zetu tuzifanye na kumshutumu Magufuli lakini sio taasisi za ulinzi wa nchi.
Kumbe hivyo vyombo aiku hizi ni vya siasa navyo?? Siasa za Afrika ni mavi matupu.

Huko kwa wenzetu wanaoona mbele mnapambana kisiasa kuchukua madaraka tu. Hivyo vyombo vyenyewe vinakuwepo tu na mnavikuata nakuviacha na habipaswi kufungamana na siasa zisizolinda msitakabali wa taifa.
 
..nadhani unazungumzia kwa nafasi ya URAISI.

..vyama vya upinzani havijawahi kuwazidi ccm ktk kampeni za Uraisi.

..mara zote wameweka wagombea ambao ni weaker compared to mgombea wa ccm.

..pia mara zote wamekuwa out-campaigned na out-organized na ccm.

..ccm wamekuwa wakifanya kampeni kwa nguvu zaidi kuwashinda wapinzani.

..ccm pia wamekuwa wakifanya kampeni ambazo ziko more organized kuzidi kampeni za ccm.

..Kuna mambo matatu ya msingi. La kwanza MGOMBEA. La pili CAMPAIGN / UJUMBE. La tatu ORGANIZATION.

..Wapinzani wajitahidi washinde mambo mawili kati ya hayo matatu na hakutakuwa na kisingizio cha system kuwazuia.

cc Kalamu1, Nguruvi3
Mwanaccm unaisharuri jinsi ya chadema kushinda?? Amazing...
 
Back
Top Bottom