Chadema mnapofanya siasa zenu tambueni kuwa ni ngumu kuchukua nchi bila kufanya urafiki na vyombo vya ulinzi na usalama. Either mtatumia umwagaji damu, Vyombo vya ulinzi ndio watanzania wenyewe ukiona umekubalika 50% kwa watanzania na ndani ya ulinzi ndio hivyo hivyo, maafisa wa vyombo wanataka kujilidhisha na sera zenu juu yao.
Hivyo wapinzani mnapotaka kufanya siasa msijitenge na vyombo kama Police, TISS na JWTZ ni ushauri wangu tu wa leo kuvishutumu vyombo vya ulinzi mala kwa mala mtajenga kutoaminika kupewa nchi ndio maana wanawasumbua sana maana wanajuwa mkiingia mtawageuka na kuwachukulia hatua. Siasa imebadilika vyombo vya usalama ni muhimu ili kwenda hasa ikulu.
Ili jambo litaponza upinzani miaka mingi sana na tutachelewa kuondoa mfumo mbovu wa taifa endapo upinzani hautabadilika na kuwa upinzani wa sera za mageuzi na sio lawama kwa vyombo vya usalama siasa zetu tuzifanye na kumshutumu Magufuli lakini sio taasisi za ulinzi wa nchi.
Hili nalo ni neno....
Lakini ungeenda mbele kidogo kwa kuwashauri wafanye nini ili wawe karibu na vyombo hivi...
Anyway, let me try say something as ushauri kwa wanaotaka kuiondoa CCM barabarani...
Jambo kubwa kabisa kulifahamu ni kuwa, ni ukweli usiopingika kuwa "SYSTEM IKIWA UPANDE WAKO", there's no way kuwa utashindwa kuchukua nchi....
Kinyume chake, " The SYSTEM" ikiwa against you, hata kama umeongoza kwa kura 90%, there's no way kuwa watakupa nafasi ya kuongoza nchi....
Kwa maoni yangu, nadhani kuna umuhimu wa kina Freeman Mbowe, Zito Kabwe na Maalim Seif Shariff Hamad kuona namna ya kuingia special agreements na "SYSTEM" ili kuwakikishia usalama wao mara watakapowapa nchi kwa kuzingatia maeneo yote muhimu watakayo yaweka mezani kama msingi (basis) ya makubaliano....
Ni ukweli usiopingika kuwa, watu wa SYSTEM na WATAWALA kwa umoja wao wametenda mengi ya ovyo na maovu kiasi ambacho hawatakuwa tayari kuona mtawala aliyepo chini ya CCM anaondoka maana likitokea hili wao pia wako hatarini.
Yaani wanaona ni bora zaidi wafe na shetani waliyenaye sasa kuliko kumkaribisha mwingine wasiyejua agenda zake kwao especially ktk kuwakikishia maisha yao baada ya mabadiliko hayo....!!
Kila mtu anaogopa mabadiliko. System nayo inaogopa mabadiliko yenye athari hasi kwao. Ni lazima kama hujaeleweka, wakuzuie kwa namna yoyote kupenya...
For sure, this is a difficult task to be done, but it is possible..
Kwa sababu, binafsi deep inside my heart, natambua kuwa hii kitu tunayoiita "SYSTEM" kwa maana ya vyombo vya ulinzi na usalama (polisi, JWTZ &TISS) hawaridhishwi na hawapendi kabisa jinsi mambo yanavyopelekwa ktk nchi hii kwa sasa chini ya uongozi wa serikali iliyoundwa na CCM....
Hii mtu apende kusikia au asipende, lakini ukweli ndiyo huu maana walio ndani ya system wengine ni rafiki zetu, tunaongea nao kwa njia zetu, wanasema haya waziwazi, hawafichi kitu....
Na pia nafahamu kuwa, ili kuzuia haya kutokea, watawala wa sasa wanajaribu kuwapa kila aina ya INCENTIVES wakuu wa taasisi hizi pamoja na affiliates wao ili kuwazuia na kuwashawishi wasije kuwageuka....
Mathalani; wafanyakazi wa taasisi hizi (polisi, JWTZ na TISS) kuanzia wakuu wao hadi wafanyakazi wa kada ya chini kabisa, wana marupu rupu bora na mazuri sana kuliko wafanyakazi wengine wa umma wote...
Aidha, wengi wa watu toka taasisi hizi (hasa wanajeshi wa JWTZ na wale toka TISS) wamepewa kushika nyadhifa nyeti serikalini kuanzia wizara mbalimbali, ma-RC, DCs, DEDs na kuwa wakuu wa idara/taasisi nyeti kama PCCB, BoT, NEC nk
Si hivyo, kwa jinsi utawala uliopo unavyohakikisha umeikamata vyema "SYSTEM", sasa mpaka ngazi ya kata na tarafa unafanya recruitment ya vijana wa kike na kiume wenye element na mtazamo huu na kuwaweka huko wasimamie mambo yao...!!
Sasa tujiulize, hawa kina Tundu Lissu , Zito Kabwe, Maalim Seif Shariff Hamad, Freeman Mbowe na wengine watapitia wapi?.. Ni lazima kuwe na njia zenye ubunifu wa ziada kubadili mambo haya ili yawe upande wao, na INAWEZEKANA....!!
Sasa tunaweza kuona kuwa hii pekee inaifanya SYSTEM iwe na utiifu kwa utawala uliopo madarakani kwa viwango vyote na hivyo kuwa vigumu sana kuusalitiana wao kwa wao japo INAWEZEKANA hili kutokea if something special has to be done.......
Therefore, NOTHING IS IMPOSSIBLE ON EARTH...
Why? Kwa sbb hawa ni watu kama alivyo mtu yeyote. Wana familia na ndugu zao wengi kwa maelfu na malaki wanateseka dhidi ya utawala huu mwovu..
Hii pekee pamoja na mengine mengi yaliyo dhaifu kabisa yanaweza kutumika kama fursa ya kubadilisha mwelekeo wa mambo...
Tukumbuke kuwa, nyama na wali na makando kando yake ndiyo chakula kinachopendwa na chenye hadhi ktk maeneo ya jamii nyingi...
Lakini, ukila hicho tu kila siku unakikinai na MTU angependa siku nyingine ale hata "mchembe" ama chakula cha aina nyingine...
Vivyo hivyo hata kwa "SYSTEM" yetu, inawezekana wanapata chochote watakacho, lakini ukinaifu na kuchoka kupo tu na lazima wanahitaji mabadiliko fulani ambayo watawala waliopo hawawezi kuwapatia...
Tumie fursa hiyo, take advantage na zungumzeni nao. IT'S POSSIBLE to change the direction...!!