Huwezi kuchukua nchi bila SYSTEM kuwa upande wako

Huwezi kuchukua nchi bila SYSTEM kuwa upande wako

Nadhani mfumo uliopo, dola yote inaitumikia ccm. Polisi ni waziwazi. Hao wengine ndo kwa style ya kutokujulikana. Wote ni wale wale. Utaanzia wapi kukubaliwa na kufanya kazi na tiss hii ya ccm na ussitwe msaliti ama unataka kupindua nchi? Ccm wenyewe wenye mahusiano na upinzani wanadhibitiwa! Achilia mbali maafisa wa serikali na viongozi kama wakuu wa wilaya, mikoa nk.

Nguruvi3

..labda wale wa ngazi za juu kabisa.

..lakini ngazi za kati na chini ni vijana waliokulia ktk mfumo wa vyama vingi.

..ccm haiwezi tena kuvihodhi vyombo hivyo na ndiyo maana unaona inatapatapa.
 
leo umewaza mbali sana kuleta wazo kma hili, ila siyo lazima viwe upande wako pale ambapo kuna demokrasia ya kweli, kumbuka Ivory Coast, jamaa alikuwa na vyombo vya usalama pmja na jeshi lote nyuma yake, lakini wananchi waliamua...Tunisia, Misri ni mifano tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Known Fact:
Kule Ivory Coast Laurent Gagbo alikuwa na wanamgambo au kikundi chacke cha ulinzi nje ya majeshi rasmi, na ndio waliopambana kumlinda kutaka kumbakisha kinguvu madarakani hadi walipozidiwa, kisha mkuu wa wanamgambo akamsaliti na kukimbilia nchi jirani kujinusuru asikamatwe.
Huyo jamaa alikuja kujisalimisha akashitakiwa pamoja na Gagbo kule The Hague.

Kifupi Ivory Coast raisi aliyeshindwa hakuungwa mkono na majeshi, majeshi yalikuwa upande wa mpinzani wake.
 
..labda wale wa ngazi za juu kabisa.

..lakini ngazi za kati na chini ni vijana waliokulia ktk mfumo wa vyama vingi.

..ccm haiwezi tena kuvihodhi vyombo hivyo na ndiyo maana unaona inatapatapa.
Sasa ngazi za chini watasaidia nini na wakati wao ni wapeleka taarifa tu na labda utekelezaji wa maagizo?
 
..wapinzani kuanza kulalamikia system wakati hawajatimiza wajibu wao siyo sahihi.

..nimesisitiza mambo matatu ya msingi ambayo wapinzani wanatakiwa wayatekeleza.

..1. kuweka mgombea mwenye hoja zenye ushawishi. mgombea mwenye uwezo wa kumfunika kwa hoja mgombea wa ccm.

..2.kufanya mikutano mingi zaidi ya kampeni kuwazidi ccm. wagombea wa upinzani must out-work wagombea wa ccm.

..3.kampeni ya Uraisi lazima iwe in-sync na kampeni za wabunge. Hapa nazungumzia UJUMBE/ SERA / AHADI zenye mvuto.

..wapinzani wanatakiwa wafanye yote matatu kwa umahiri na ufanisi mkubwa. Au wafanye angalau mawili kati ya hayo matatu.

..wakiweza hayo hata hao "system" watavutika na kugeuka kuwa "cheer leaders" wa upinzani.

NB:

..Tuwe wakweli, ni lini kampeni za upinzani zilikuwa na mambo yote niliyoyataja hapo juu? Kwanini sisi tunaoshabikia upinzani tunataka ushindi wa miujiza au hila?
 
Sasa ngazi za chini watasaidia nini na wakati wao ni wapeleka taarifa tu na labda utekelezaji wa maagizo?

..umepitia jeshini?

..unajua umuhimu wa askari wa cheo cha captain kwenda chini?

..top brass are nothing kama huku chini hawako motivated na hawaamini ktk mission.

..tutafika wakati haitawezekana tena kuwalazimisha vijana kusikiliza mziki wa kizamani wakati wamekua wakisikia mziki wa kizazi kipya.
 
..umepitia jeshini?

..unajua umuhimu wa askari wa cheo cha captain kwenda chini?

..top brass are nothing kama huku chini hawako motivated na hawaamini ktk mission.
Ingekuwa hivyo kaka si ingekuwa rahisi kupindua nchi?
 
Chadema mnapofanya siasa zenu tambueni kuwa ni ngumu kuchukua nchi bila kufanya urafiki na vyombo vya ulinzi na usalama. Either mtatumia umwagaji damu, Vyombo vya ulinzi ndio watanzania wenyewe ukiona umekubalika 50% kwa watanzania na ndani ya ulinzi ndio hivyo hivyo, maafisa wa vyombo wanataka kujilidhisha na sera zenu juu yao.

Hivyo wapinzani mnapotaka kufanya siasa msijitenge na vyombo kama Police, TISS na JWTZ ni ushauri wangu tu wa leo kuvishutumu vyombo vya ulinzi mala kwa mala mtajenga kutoaminika kupewa nchi ndio maana wanawasumbua sana maana wanajuwa mkiingia mtawageuka na kuwachukulia hatua. Siasa imebadilika vyombo vya usalama ni muhimu ili kwenda hasa ikulu.

Ili jambo litaponza upinzani miaka mingi sana na tutachelewa kuondoa mfumo mbovu wa taifa endapo upinzani hautabadilika na kuwa upinzani wa sera za mageuzi na sio lawama kwa vyombo vya usalama siasa zetu tuzifanye na kumshutumu Magufuli lakini sio taasisi za ulinzi wa nchi.
Kwani ndiyo umejua leo wewe Mkenya? Huko kwenu Kunyaland vipi??
 
Ingekuwa hivyo kaka si ingekuwa rahisi kupindua nchi?

..kwanini upindue wakati ni rahisi zaidi kuruhusu demokrasia?

..wanaopinduana ni wale ambao hawana vyama vya siasa kabisa.

..Nigeria walikuwa wanaongoza kwa kupinduana Afrika.

..Lakini tangu waazishe mfumo wa vyama vingi hakujatokea mapinduzi.
 
Chadema mnapofanya siasa zenu tambueni kuwa ni ngumu kuchukua nchi bila kufanya urafiki na vyombo vya ulinzi na usalama. Either mtatumia umwagaji damu, Vyombo vya ulinzi ndio watanzania wenyewe ukiona umekubalika 50% kwa watanzania na ndani ya ulinzi ndio hivyo hivyo, maafisa wa vyombo wanataka kujilidhisha na sera zenu juu yao.

Hivyo wapinzani mnapotaka kufanya siasa msijitenge na vyombo kama Police, TISS na JWTZ ni ushauri wangu tu wa leo kuvishutumu vyombo vya ulinzi mala kwa mala mtajenga kutoaminika kupewa nchi ndio maana wanawasumbua sana maana wanajuwa mkiingia mtawageuka na kuwachukulia hatua. Siasa imebadilika vyombo vya usalama ni muhimu ili kwenda hasa ikulu.

Ili jambo litaponza upinzani miaka mingi sana na tutachelewa kuondoa mfumo mbovu wa taifa endapo upinzani hautabadilika na kuwa upinzani wa sera za mageuzi na sio lawama kwa vyombo vya usalama siasa zetu tuzifanye na kumshutumu Magufuli lakini sio taasisi za ulinzi wa nchi.
Kwani Usalama wa taifa na vyombo vya ulinzi sio watanzania, wao hawaoni kinachotokea? Au they don't feel?? Inawezekana kuna baadhi ya mambo yanafanywa na serikali hata wao hayaendi.
Mifano iko mingi tu duniani kuna'marais wameingia tu madarakani wakatimua Mkuu wa jeshi' polisi na usalama.

Mwisho wa siku maamuzi ni wapigakura. (Wananchi).
 
..Lowassa afya yake haikuwa nzuri, and he did not put up any fight.

..pia kampeni yake ilikuwa out of sync na kampeni za wabunge wa ukawa.

..zaidi mgombea wa ccm, Magufuli, alifanya mikutano mingi ya kampeni kuliko mgombea wa ukawa, Lowassa.

..vilevile kulikuwa na media blackout kwa mgombea uraisi wa ukawa na wagombea ubunge.

..lakini pia Lowassa alipata kura nyingi ambazo hazi-reflect udhaifu wa kampeni aliyofanya.
Naamini kwamba mgombea wa CHADEMA Lowassa, 2015, angekuwa ni yule Lowassa Waziri Mkuu wa Kikwete, Magufuli asingekuwa rais hii leo.

Lowassa alishindwa kutokana na mwonekano wake jukwaani ulivyojionyesha.
Kidogo inashangaza kwamba hadi leo bado anadunda, maanake wakati ule alionekana kama atadondoka wakati wowote.

Lowassa na CHADEMA walishindwa uchaguzi ule kwa sababu kama ulizoziorodhesha hapo.

Mkutano wake wa kwanza wa kampeni pale jangwani ndio ulioondoa matumaini kwa wengi, alipoanza kusema watu wakasome 'sera' kwenye mtandao.
 
..wakati mwingine nahisi huenda hata hizo alizopata nyingine zilitokana na wizi.

..mgombea anayefanya kampeni ya aina ile haiyumkiniki akapata kura nyingi kama alizopata Lowassa.
 
..Mkuu asante sana.

..umeweza kueleza kwa ufasaha mkubwa kile nilichokuwa najaribu kukieleza.

..natumaini wapinzani watarekebisha makosa ya 2015. Na baadhi yao wanakiri mapungufu ya kampeni yao ya 2015.
Sina hakika, au labda, sahihi zaidi niseme sijui kama kuna marekebisho mhimu yaliyofanyika ndani ya hivyo vyama ili kampeni hizi za Oktoba ziwe tofauti na zile za 2015.
Kuna sababu nyingi zinazoweza kuwa zimewazuia kujiandaa vyema zaidi kama walivyotegemewa wajiandae; moja ya sababu kubwa ni kuvurugwa walikofanyiwa katika miaka hii mitano.

Wamevurugwa mno, toka kupigwa risasi; kufungwa jela na kununuliwa kwa wabunge wao.

Washukuru tu kwamba wameweza ku'survive'.

Tulichohimiza wakifanye katika miaka mitano, yaani kuvipeleka vyama vyao na kujiimarisha mashininani, sijui kama kazi hiyo wameifanya kwa ufanisi. Hapa ndipo nilipo na wasiwasi mkubwa, na kunifanya niseme 'SIJUI".

Wangefanikiwa kuifanya hii kazi huko mitaani,, kwa jinsi Magufuli alivyovuruga nchi, pangekuwepo na matumaini kuwa CCM wataondoka.
Hapajawahi kuwepo na wakati mzuri kuiondoa CCM madarakani kama ilivyo wakati huu. Lakini maandalizi yaliyotakiwa yafanyike kwa umakini mkubwa hayakufanyika (sijui kama yalifanyika).
 
..wakati mwingine nahisi huenda hata hizo alizopata nyingine zilitokana na wizi.

..mgombea anayefanya kampeni ya aina ile haiyumkiniki akapata kura nyingi kama alizopata Lowassa.
Kama kweli alizipata, ni kutokana na 'residual sympathy' aliyokuwa nayo. Ni ishara kwamba hali yake ingekuwa ni nzuri, ilikuwa afagie kabisa.
 
Umma wa Watanzania ni bure, hata upokonywe ushindi mchana kweupe hawatakutetea zaidi ya kwenda kunong'ona vyumbani na wake zao.
Wana haki kwani hata ukishinda unarudi kuwagawia pesa si unakula na wakwenu .Wahangaike nini
 
..nadhani unazungumzia kwa nafasi ya URAISI.

..vyama vya upinzani havijawahi kuwazidi ccm ktk kampeni za Uraisi.

..mara zote wameweka wagombea ambao ni weaker compared to mgombea wa ccm.

..pia mara zote wamekuwa out-campaigned na out-organized na ccm.

..ccm wamekuwa wakifanya kampeni kwa nguvu zaidi kuwashinda wapinzani.

..ccm pia wamekuwa wakifanya kampeni ambazo ziko more organized kuzidi kampeni za ccm.

..Kuna mambo matatu ya msingi. La kwanza MGOMBEA. La pili CAMPAIGN / UJUMBE. La tatu ORGANIZATION.

..Wapinzani wajitahidi washinde mambo mawili kati ya hayo matatu na hakutakuwa na kisingizio cha system kuwazuia.

cc Kalamu1, Nguruvi3
Wala si kweli hata kidogo!!!
 
Na vile huwa wanasema wakiingia ikulu watawafukuza kazi polisi wote! Hehehe....
Hapo sasa polisi mwenyewe atakubali kulinda sanduku la kura la Huyo mpinzani lisiibiwe wakati anajua akishinda huyo mpinzani kazi Hana si atatoa hadi defender kulibeba hilo sanduku kukimbia nalo
 
Hiyo nikwa dunia nzima au ni hapa kwetu tu kwenye siasa maji taka ya zama hizi.
 
Vyombo vya ulinzi huwa vipo neutral upima nguvu ya umma ikiwa kubwa usimama na wananchi tumeshuudia nchi nyingi.Ili kulinda amani ya nchi.
Hata 2015 vilisimama na wananchi ndio maana Magufuli akapita
 
Siyo kihivyo. Wewe tu. Naenda kurekebisha kwasababu mwenye busara JokaKuu amenikumbusha na kunisahihisha.

Kwahiyo kwa maana nyingine unakiri Kwangu kuwa kumbe ulikuwa huna Busara ndiyo maana ukakosea vile? Waswahili bhana!
 
Back
Top Bottom