..nadhani unazungumzia kwa nafasi ya URAISI.
..vyama vya upinzani havijawahi kuwazidi ccm ktk kampeni za Uraisi.
..mara zote wameweka wagombea ambao ni weaker compared to mgombea wa ccm.
..pia mara zote wamekuwa out-campaigned na out-organized na ccm.
..ccm wamekuwa wakifanya kampeni kwa nguvu zaidi kuwashinda wapinzani.
..ccm pia wamekuwa wakifanya kampeni ambazo ziko more organized kuzidi kampeni za ccm.
..Kuna mambo matatu ya msingi. La kwanza MGOMBEA. La pili CAMPAIGN / UJUMBE. La tatu ORGANIZATION.
..Wapinzani wajitahidi washinde mambo mawili kati ya hayo matatu na hakutakuwa na kisingizio cha system kuwazuia.
cc
Kalamu1,
Nguruvi3
Mkuu JokaKuu,
Kwanza nianze kwa kukataa hoja ya mleta mada; pamoja na kwamba sijasoma aliyowasilisha ndani ya mada yake. Nakataa nadharia yake kutokana na kichwa cha habari aliyowasilisha.
Lakini hili siyo lililonivuta kuja hapa na kuitikia wito wako.
Nimekusoma kwa haya uliyojadili hapo juu, na mimi nikaona nidandie hapo hapo kuweka yale ambayo nimekuwa nikiyawaza kwa muda mrefu kidogo kuhusu siasa zetu hizi za Tanzania.
Nimekuwa nikiwaza mawazo haya niyaanzishe mada yake pembeni, lakini nimekuwa nikisita.
Nitatumia nafasi hii kuyaweka hapa na wewe pamoja na wasomaji wengine pengine mkiona yanastahili mjadala mkubwa, basi, utakuwa ni mwanzo wa kuyaeneza.
Tumekuwa na vyama vya upinzani kwa muda mrefu sasa, tokea 1995, na tokea hapo takribani vyama vyote vilivyotaka kushiriki vimekuwa huru kushiriki kwenye chaguzi mbali mbali na Chaguzi Kuu za Rais na Wabunge.
Mara zote hizi CCM ndio imekuwa mshindi, kwa kura nyingi kwa Rais, na kupata wabunge wengi. Ni mara chache sana, sikumbuki uchaguzi uliofanyika CCM ikakosa kupata wabunge zaidi ya nusu Bungeni.
Imekuwa hivyo nyakati zote, kiasi cha kwamba, nadhani yamekuwa ni mazoea kwa watu kutegemea CCM ishinde na kupata wabunge wengi.
Nasema imekuwa mazoea, kwa sababu hakuna anayeuliza kwa nini iwe hivyo kila mara?
Vyama vya upinzani, naona kwa sababu nisizozielewa, hili haliwasumbui, kwa sababu huwa sisikii wakilijadili wala kulisemea kwenye kampeni ili watu walijue. Mara zote, nasisitiza, kwa sababu sina ushahidi tofauti ya haya ninayoyaandika, mara zote, wapinzani lengo lao ni kushinda urais na wabunge wengi bungeni kama anavyofanya CCM. Hilo ndilo huwa wanalisisitiza mara zote.
Sasa najiuliza, kwa nini iwe hivyo? Na hasa baada ya Rais Magufuli kuonyesha wazi anavyopenda na kufaidika na ushindi wa asili mia. Ule wa serikali za mitaa bado hakuridhika na asili mia tisini na tisa; atafurahi safari hii Oktoba akipata 100%!
Baada ya kuona aliyofanya tokea 2015, kwa nini waTanzania wasielezwe; hapana, wasikumbushwe athari ya mazoea yao ya kuchagua CCM na wabunge karibu wote Bungeni kuwa wa CCM?
WaTanzania wanahitaji kukumbushwa na kutahadharishwa waache hii tabia ya kuchagua chama kimoja na kukirundikia madaraka yote.
Magufuli na Ndugai wametuonyesha waziwazi bila ya kificho chochote ubovu wa tabia hii.
Hata kama waTanzania bado wanayo mashaka ya vyama vya upinzani kuwa na uwezo wa kutawala, ni kuwaweka wengi wao zaidi bungeni ili wapate huo uzoefu wanaoutaka, mbali ya kuwa na sababu mhimu zaidi ya kumzuia Magufuli na Ndugai kumiliki kila kitu.
Nisirefushe sana mawazo haya, nadhani ninachotaka kukieleza, hata kama sikukinyoosha kitakuwa kimeeleweka.
WaTanzania wahimizwe na waache tabia ya kurundika bungeni wabunge wengi toka chama kimoja, hasa hiki chama cha CCM.
WaTanzania wawapeleke wabunge wengi toka upinzani Bungeni, angalao hata wafikie nusu ya wabunge waliomo humo.
Naomba nieleweke vizuri. Sijaandika mahala popote kwamba Magufuli ni lazima ashinde kura hapo Oktoba. Lakini kama akilazimisha kushinda, hata hao wabunge wengi atalazimisha wananchi wakubali?
(Sikuhariri).