Huwezi kuchukua nchi bila SYSTEM kuwa upande wako

Ishu sio kuitukana ishu hizo mamlaka ni wanufaika siku mirija yao ikikatwa hawatoweza ibeba.Hizi nadharia za umilele zimewaponza watawala na vyama vingi Sana tena vyenye nguvu kuliko ccm vikafa.Ili ccm idumu milele ni lzm ishuke kwa wananchi ipambane na shida za wananchi na sio kupambana na wapinzani wapinzani sio shida za watz
 
Hebu fafanua ni jinsi gani upinzani ufanye kazi na JWTZ na TISS
 
Hebu fafanua ni jinsi gani upinzani ufanye kazi na JWTZ na TISS
Njia nyingine ni wao kuanza kupata wanachama kutoka katika taasisi hizo hasa wanaoingia Kwenye active politics.

Tatizo lililopo ni kuwa ccm imevibrand vyama vya upinzani kama common enemies wa system na kuwapaka picha ya busy bodies badala ya chama mbadala vinavyopigania kutengeneza a new status quo.

Vyama vya siasa vya mageuzi vinatakiwa vipambane kuondoka hii brand ya UPINZANI badala yake vijenge dhana ya vyama mbadala.

Hii dhana ya chama cha upinzani inavifanya vionekane vipo kwajili ya kupinga status quo na siyo kwajili ya kubadilisha status ccm imefanikiwa kuvifanya vyama vya upinzani kama common enemies wa vyombo vya dola na ccm yenyewe.

We have a long way to go hatupaswi kupigania kiti cha urais tu tunapaswa kupigania a new order ambayo kujengwa kwa msingi wa kuimarisha itikadi na kuielewesha kwa wananchi.

Tukifanikiwa hilo jamii itakuwa imegawanyika sehemu mbili na hata huko kwenye vyombo vya dola vyama vitapata wafia chama na wafuasi wa itikadi.

Bado naamini nadharia ya Yeriko Nyerere kuwa vyama vya upinzani vimefanikiwa kuwaaminisha wananchi kuwa vinaweza kuongoza ila bado havijaiaminisha dola kuwa vinatosha kuwa mbadala wa ccm.

Hili linahitaji mikakati mipya ikiwemo kuondoa majority ya CCM bungeni kwanza, kuondoa status quo ya ccm kuwa ili mtu afanikiwe kimaisha hapa Tanzania lazima aiunge mkono CCM hali kama hii unaifanya CCM kuwa omnipotent katika politics za nchi.
 
CHADEMA Bila shaka watapokea kwa mikono miwili huu ushauri wako mkuu na kuufanyia kazi ipasavyo
Tatizo lillilopo kwa CHADEMA kwa sasa wameloose focus ya kupambana badala yake wanatapata kutafuta foothold.

Badala ya kufanya attack toka uchaguzi mkuu umepita wameretreat na kuanza kujilinda badala ya kushambulia this is a mistake ambayo hawakutakiwa kuiruhusu even for a second.

Wanapaswa kuregain their lost ground waanze kushambulia na wasitazame angle moja tu ya ufisadi serikalini hii hoja walineutralize wenyewe kwenye 2015 elections kwa kuchota kinyesi chooni na kukipeleka sebuleni wakijidanganya kuwa wangeua madhara ya kinyesi hicho kwa maji ya mkojo ( nafikiri umenielewa). Vivyo hivyo serikali ya awamu ikafanya polishing kuwa inapambana na ufisadi while it is not. Hoja hii haina nguvu tena na haitawasaidia.

Ukiangalia mapungufu ya awamu ya tano ni kwenye ustawi wa watu , badala ya kuboresha maisha ya watu na kuzalisha fursa nyingi za uchumi awamu ya tano imefeli badala yake imezalisha mafukara wengi sana hii ndiyo ilipaswa kuwa hoja ya msingi ambayo ilipaswa iwe detailed vya kutosha na ilani yao iwe na kitu kinachoeleweka.

Hali ya kisiasa nchini si salama sana kwa vyama vya mageuzi na wanachama wake hivyo imefanya vyama vya siasa vishindwe hata kupambana katika majukwaa kitu ambacho ccm wametumia kuregain their lost grounds.



Sent using Jamii Forums mobile app
 

..ccm wanaweza kudhulumu chaguzi za Zanzibar kwasababu hawapati challenge ya kutosha kutoka kwa vyama mbadala kwa upande wa Tanganyika.
 
Inategemea umeichukuaje nchi ,hiyo system huwa wanakimbia wakati wa uchukuaji

Sent using Jamii Forums mobile app
 
..ccm wanaweza kudhulumu chaguzi za Zanzibar kwasababu hawapati challenge ya kutosha kutoka kwa vyama mbadala kwa upande wa Tanganyika.
Kwa hali ilivyo vyama vya mageuzi vipambane kuidhoofisha ccm bungeni vitapenya kwa kwa urahisi sana maana wataweza kucommand mwelekeo wa serikali wanavyotaka.

Sheria mbovu zinazoibeba ccm zitaweza kubadilishwa.

Sera mbovu zisizo na tija kwa wananchi zitapigwa chini with easy.

Hii itajenga imani kubwa sana na support kwa vyama vya mageuzi kwa wananchi ambayo mpaka sasa wanayo japo imeanza kulegalega.

ccm inanufaika sana na bunge dhaifu kwa kupitisha sera na sheria mbovu zisizo na tija kwa wananchi.

Hii siyo safari ya lelemama ni mapambano ambayo vyama vya upinzani havipaswi kulegeza kamba hata kidogo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunayo sasa NCCR ya Mbatia ambayo inajipambanua kama wanaweza kushika 'Madaraka' ili watimize baja zao lkn si kutimiza mahitaji ya umma (Maendeleo)
Wanamtumikia nani? Kama si matumbo yao aje mtu atuambie NCCR hii itapigania katiba mpya, sheria mbovu, uwajibikaji wa wabunge na serikali pamoja na elimu ya uraia kwa umma!!!!??? Kama wataweza wasaini na umma kabla ya kura kuyatimiza hayo
 
Hakuna chochote zaidi ya wizi wa kura acha porojo.ndio maana mkisikia tume huru majiharishia
 
"Mabeberu'wakitaka muandamane kumtoa jiwe ni dk sifuri….kuna mtu alikuwa anatisha kama Muammar Mohammed Abu Minyar Gaddafi
 
Naamini japo sina uhakika sababu mojawapo ya cdm kumteua lowasa kuwa mgombea wao wa urais ni kuwin trust kutoka hivi vyombo vya usalama, maana huyu mtu wanamfahamu amekulia huko, sasa kama lowasa walimkataa, hii sababu inaonyesha zahiri haina nguvu tena, vyombo vyetu cha usalama vya nchi vinatakiwa viwe neutral kwa vyama vyote, maana hivi vyama vipo kwa mujibu wa sheria na katiba kwa msingi huo vina haki sawa kama vyama vinginevyo siasa pamoja na ccm, sasa unapoona hivi vyombo vinalalia upande mmoja, basi jua watu waliopo kwenye vyombo hivyo wametawaliwa na ubinafsi, hafanyi kwa maslahi ya nchi au wananchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
..Ni wazo zuri.

..kusiwepo na chama chenye kuweza kupitisha mswada bungeni bila kushirikiana na chama kingine.
Utapataje majority bungeni na tume fake ya uchaguzi?.hatua ya kwanza ni tume huru
 
Utapataje majority bungeni na tume fake ya uchaguzi?.hatua ya kwanza ni tume huru

..mnaosema Tume Huru kwanza mko sahihi. Kwasababu tume ndiyo inayosimamia uchaguzi na kutangaza washindi halali.

..wanaosema majority bungeni kwanza nao wako sahihi. Kwasababu bila majority bungeni huwezi kupitisha sheria itakayounda tume huru.

NB:

..kwa sasa uwezekano wa kuunda tume huru ya uchaguzi haupo, kwasababu wabunge wa ccm hawana nia hiyo.
 
Tuna Safari ndefu sana sishangai ndio maana afrika masikini
 
Ccm ndio system na system ndio Ccm,

kuwaambia wapinzani wajenge ushawishi kwa Ccm ili washinde ni kuwajaza ujinga.
Ukiacha ushabiki utaelewa

System iko kwa maslahi ya taifa ukiona chadema hawapewi nchi ujue kuna shida mahali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…