LC 300 and alike is not for everyone.
Sugua sana goti msikituni na makanisani, omba sana Mungu utaishia kwenye prado mchaga.
Huku kwa ma LC 300 ni dunia nyingine, dunia ya maagano, lazima uwe na nguvu za giza sio kulinunua tu hata kuliendesha, hakuna mjinga atakubabidhi milioni 400 uzurure nayo mitaani kwenye kila aina ya risk.
Hakuna washirikina kama madereva wa serikali na mabasi ya mikoani plus malori, hizo kazi huzipata kwa kuroga na kuhonga sana, mjinga nani ajukabidhi na milioni upige nayo misele.
Tanzania ukichukua fomu tu ugombee ubunge watakuja wazee wakulazishe kukupa hirizi au wakufanyie kisomo.
Ikulu ya Magogoni kila siku ni ubani udi na madawa yanafukizwa tu.
Ukija kwa wamiliki the same, Mungu wetu kuna limit ya mafanikio ametuwekea sisi waafrica, kuna level tukifika huwa tunamkufuru, ndio maana misikitini na makanisani wale waumini wa kweli wanamaisha ya chini au ya kawaida sana, wale matajiri ukiwafuatilia ndio wamiliki wa majini, washirikina wakubwa.
Waafrica ni wanafiki sana, bado hatujaacha dini zetu za asili, kuanzia ijumaa mpaka jumapili tutaenda misikitini na nakanisani, tukitoka hapo tunapishana kwa waganga.
Asilimia kubwa tuko hivyo.
Tuendelee kuendesha crown tu ili tufike mbinguni.