Huwezi kumpiga mtu na Kumnyima haki ya kulia

Huwezi kumpiga mtu na Kumnyima haki ya kulia

ubongokid

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2017
Posts
2,436
Reaction score
4,756
Naandika haya nikitambua kwamba kila mtu anaweza kuwa na tafsiri yake kwa mujibu wa mtazamo na uelewa wake."Kuwa na uwezo au haki ya kumpiga mtu hakukupi haki au uwezo wa kumzuia kulia"Huu ni msemo wa wenye hekima wengi.

Ni wajibu wa serikali na viongozi wote wa serikali kuhakikisha kwamba raia wake wanapata chakula bora,malazi bora na wanakuwa na afya bora.Ni wajibu wa serikali na sio wajibu wa raia mmoja mmoja.Kila raia mmoja mmoja anao wajibu mmoja tu kutumia vizuri zile fursa anazopatiwa za kula vizuri,kulala vizuri na kwa na afya bora.

Serikali yoyte ile halali haiwezi kujivua wajibu huo na iwapo haitekelezi sera na mipango yake katika mrengo wa kuhakikisha kwamba wananchi wanapata chakula,malazi na afya bora basi serikali hio haina mamlaka wala uhalali wa kuendelea kuwepo.

Kama wewe ni baba na umeshindwa kuwapatia watoto wako pamoja na wewe mwenyewe chakula bora basi wa kulaumiwa ni viongozi wa serikali.Kama wewe ni mtoto nwa wazazi wako wameshindwa kukupatia mahitaji yako yote basi wa kulaumiwa ni serikali yako.Iwapo wewe ni mgonjwa na umeenda hospital na hukupata huduma na dawa basi wa kulaumiwa ni serikali.Hata kama ni mwanamke umekosa MME basi wa kulaumiwa ni serikali.

Kabla ya kuendelea nirudie"Hakuna mwenye haki ya kumpiga mtu na kumnyima haki ya kulia" Ndio haki ya kulia haiwezi kuondolewa na hivyo basi tusiache kulia.TULIE kwa uchungu.HAIFAI KUPIGWA TUPIGWE NA HAKI YA KULIA PIA TUNYIMWE.

Kwa nini wanafunzi wanyimwe mikopo na wakilalamika wanyimwe haki ya kulalamika?Huu ni unyanyasija uliopita kipimo.Tuninyimeni mikopo lakini msituniyime na haki ya kulalamika pale tuapoumia.Kama mmetusomesha mpaka degree mbili lakini hamtupatii fursa za ajira je TUSILIE?Kwa nini mtunyime ajira na bado mkatae sisi KULIA kwa kukosa AJIRA tuacheni TULIA,Ninyi mnayo haki ya kutuniyima ajira lakini hamna haki ya kutuziua tusilie kwa kukosa ajira.

Ndio tunafanya kazi lakni hatupati hata nyongeza ya mshahara kwa miaka mingi huku gharama za misha zinapanda kwanini?Tuacheni TULIE kwani haki ya kutunyima nyongeza ya mshahara mnayo lakini hamna haki ya kutunyima kulia na kulalamika.

NAsisitize tena"MSITUNYIME KULIA, KULAUMU na KULALAMIKA HIO NI HAKI YETU SISI HAMUWEZI KUICHUKUA


Kuna mengi yanatendka na ambayo yanaliza.TUACHENI TULIE,HAMUWEZI KUTUZUIA KULIA.
 
Back
Top Bottom