Stephano Andrew
New Member
- May 12, 2015
- 4
- 1
ni ujinga au uvivu wakujifunza jamani!!!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Si kwamba sijui/sijuwi, lakini nahisi inaweza kuwa tafsiri yako na yangu zikawa tofauti na hivyo tunaweza kubishana kwa tunalinganisha chungwa na parachichi.
Kwako wewe pengine lugha sio 'nasibu' na haibadiliki (static), na hivyo 'kiswahili fasaha' ni kile kilichozungumzwa kabla ya wakoloni kutoka Uropa na kinachotumia lafudhi/lafidhi ya kiarabu.
Kwani wasemaji wa kiswahili wanashindana hivyo hivyo mara nyingi...
Kama inabidi kweli kujua kiarabu ili kutumia kiswahili kwa fasaha pia eti itabidi kujua kilatini au kifaransa ili kutumia kiingereza kwa fasaha. Pia naweza kujua maana ya kustaarabu bila kujua kiarabu vilevile mtu wa kiingereza anaweza kujua neno ya "bureau" bila kujua kifaransa.
Bila shaka itasaidia kujua lugha zinazohusika na lugha yako lakini si lazima. Yaani yeyote anaweza kuelewa maana ya neno kabisa akipata neno kwa etymology (yaani maelezo ya maneno kwa historia). Tuangalie kiingereza - Wasemaji wa kiingereza wangapi wanajua kifaransa? lugha ambayo inahusika na zaidi ya 30% ya maneno yote. Zamani kingereza kilibadilika sana wakati wafaransa wakivamia ungereza.
Mtoa Hoja..kwa maelezo yako inamaana kiswahili ni kiarabu...na kwako kiswahili fasaha ni kiarabu ndio maana unazihusiahanisha hizi lugha kwa ukaribu hivyo...hivyo hakuna kiswahili bila kiarabu ndivyo unavyotaka kutuaminisha..labda kwa maana rahisi tuambie kiswahili fasaha ni kipi?..kiarabu ni lugha iliyo athiri kiswahili tu kama lugha zingine zilivyo kiathiri kiswahili hivyo mantiki yako kuwa uweze kiswahili fasaha ni hadi ukijue kiarabu me nakataaa kwa miguu yote na mikono
Kiswahili ni lugha ya wenyeji wa pwani ya Afrika mashariki, ni lugha iliyotokana na nasibu ya kiarabu kwa wingi wa maneno yake na kibantu kadhalika , , wenyeji wa pwani ya Afrika mashariki ndiyo hasa walioitwa "asswahili"na pwani hiyo ilijaa waarab ambao ndiyo walioitumia sana pwani hiyo kibiashara.
Hivyo ni sawa kusema ili uwe na lafudhi nzuri ya kiswahili, hakuba budi kujua kiarabu au matamshi yake
Kwa majibu yako wewe ni mbishi tu na hata tukeshe autakubali....ivi kiswahili kina Asilimia ngapi ya misamiati ya kiarabu? Na unashindwa kueleza maana yako ya kiswahili fasaha......tatizo ni kukariri eti mtu akiwa anaongea kwa lafudhi ya kipwani ndio anajua kiswahili teh....yahe kheri akhsante taarabu...aya baki maana zako izoKwanini utie maana yako ambayo haipo kwenye andiko langu na ufikirie tu kuwa mimi nnamaanisha hiyo? mimi nnamaanisha nilichokiandika, huwa sichei na akili ya mtu, kama unajichezea akili yako ni wewe mwenyewe tu.
Hii inaonesha ni vipi Tanzania watu badala ya kuwa na reality wana "hallucinate". Mmoja tu au wawili mpaka sasa ambao sijaona kuwa wamebadili maana ya nilichokiandika, Watanzania wachache sana wako kama hao wawili. Wanaelewa wanachokisoma na hawabadili maana.
Ni nani leo hii anaekataa kuwa Kiswahili hakipo kama nilivyoandika kwenye post yangu namba moja para ya kwanza?
Kwa majibu yako wewe ni mbishi tu na hata tukeshe autakubali....ivi kiswahili kina Asilimia ngapi ya misamiati ya kiarabu? Na unashindwa kueleza maana yako ya kiswahili fasaha......tatizo ni kukariri eti mtu akiwa anaongea kwa lafudhi ya kipwani ndio anajua kiswahili teh....yahe kheri akhsante taarabu...aya baki maana zako izo
Tafuta maandiko yooyote yenye maneno zaidi ya elfu moja halafu chambuwa maneno ya Kiarabu, Ki Uropa na Ki bantu, utapata jibu "roughly".
Hapa sipo kubishana nipo kupanuana mawazo.
Nisome tena post namba moja kwa utuvu. Utanielewa tu.
Tafuta maandiko yooyote yenye maneno zaidi ya elfu moja halafu chambuwa maneno ya Kiarabu, Ki Uropa na Ki bantu, utapata jibu "roughly".
Hapa sipo kubishana nipo kupanuana mawazo.
Nisome tena post namba moja kwa utuvu. Utanielewa tu.
Tafuta maandiko yoyote ya Kiswahili yenye maneno zaidi ya elfu moja halafu chambuwa maneno ya Kiarabu, Ki Uropa na Ki bantu, utapata jibu "roughly".
Hapa sipo kubishana nipo kupanuana mawazo.
Nisome tena post namba moja kwa utuvu. Utanielewa tu.
Skia nikuambie kitu kimoja...lugha hizi hata kisarufi ni tofauti...jaribu kuchukua hata mfano mdogo tu wa mkazo wa lugha ya kiswahili na ule wa lugha ya kiarabu...alafu nipe jibu faster nakusubiria...nambie mazingira ya mkazo ya lugha ya kiarabu na ule wa kiswahili....chukua maneno ya mkopo kama tathmini, barabara, hukumu...alafu yasiyo ya mkopo kucheza kuimba kupika kupiga alafu ndio tuje katika ufasaha
Ni chini ya asilimia 30 tu ya msamiati wa kibantu katika kiswahili kama malcon Guthrie na meinhof wanavyosema...athari ya kiarabu ipo kwa kiswahili lakini sio hadi kuathiri ufasaha wa kiswahili...lugha hizi zingekuwa zinafanana kisarufi kama muundo wa sentensi..mwishilizo wa vitenzi ..uambishaji... unyambulishaji kidogo ningekubali...lakini lugha hizi ni tofauti kabisa...chunguza kwa umakini usitangulize ujasiri...angalia mwisho wa maneno mengi ya kiswahili hamna coda ila kiarabu maneno kama sahel Allah yanaishia na konsonati sasa nashindwa kuelewa ufasaha wa kiswahili kusababishwa na kiarabu unakujaje hapa....kiswahili fasaha sio utamkaji wa kheri...taaratibu ila ni kuheshimu taaratibu za kisarufi....
Duh.....hoja za nguvu tena! Hiyo post namba moja haina cha maana, sana sana inaonesha ulivyo 'mdini' tu!Nisome post namba moja, halafu ujione ulivyo "stagnant" kichwani mwako.
kiliandikwa kwa...Kiswahili kabla ya kuja maandiko ya Kilatini kikiandikwa kwa herufi zipi?
1:hiliKama unaamini Kiswahili kimeazima maneno, jee neno swahili ambalo ni kiashiria cha kwanza cha lugha ya Kiswahili nalo limeazimwa pia? limeazimwa kutoka wapi? na kabla ya hali neno Kiswahili kulikuwa kuna neno lipi?
Unajuwa kitu kimoja, wewe unataka kulazimisha kuwa Kiswahili hakikutkana na Kiarabu lakini wakati huohuo unajisahau kuwa hata neno Kiswahili ni la Kiarabu.
Maatizo uliyonayo ni madogo sana, yanayokufanya usifikirie kwa mapana na marefu zaidi yahpo ulipofikia. Tatizo la kwanza ni unataka kuongelea luga wakati historia hauijuwi. Kwanza anza kuchambuwa historia ndipo utapoielewaa vizuri lugha ya Kiswahili imetokana na nini, kwa kuanzia:
Nifahamishe, nini maana ya neno Swahili? na Waswahili ni akina nani? ili twende vyema, kwani Kiswahili ni lugha ya Waswahili. Kumbuka, kama hauwajuwi Waswahili ni akina nani na historia yao ni ipi hutoweza kujuwa Kiswahili kimetokea wapi.
Kujitosheleza kwa lugha au kutojitoshelezza kwa lugha hakumaanishi kuwa "imeazima" maneno ya lugha nyingine. Mimi nnaona ni vyema tukasema "imechukuwa" maneno ya lugha nyingine kwa maana chakuazima hurudishwa, wewe umeshindwa kueleza Kiswahili kitarudisha lini maneno "iliyoazima". Mimi nnasema; Nisome post namba moja sentensi ya kwanza.
Hata hilo neno ulilotumia ni la Kiarabu sasa sijuwi unamaanisha nini ukisema "lugha hizi"?
Hakuna maneno ya "mkopo" kama umeyakopa utayarudisha lini? unarudi kule kule ambako swali hilo limeshajadiliwa.
Mmoja juu huko alikuja na maneno ya "kuazima", cha kuazima chako? sasa wewe umebadili unakuja na kukopa, cha kukopa hurudishwa, wewe utarudisha lini? Fikiri.
Hayo maneno yanatokana na Kiarabu na yanaunda Kiswahili. Hakuna kukopana wala kuazimana. Na ndiyo maana ukinisoma vizuri post namba moja, para ya kwanza, sentensi ya kwanza kabisa, nimeandika hivi:
"Kiswahili ni lugha ambayo imetokana na Kiarabu na Kibantu na maneno mengine machache yaliongezeka kidogo kidogo kutoka lugha zingine za Afrika, Uropa na Asia"
Sasa ni nini usichokielewa hapo? sasa rudi post namba moja, ujibu swali langu, lipo mwisho kabisa wa maandiko yangu.
Hujalisoma au limekuwa gumu kwako na unalikwepa?
Bado unarudi pale pale ambapo nilikueleza kuwa unaandika bila kuijuwa historia.
Swali langu moja tu, sijuwi kama unalikumbuka, soma post namba moja mstari wa mwisho, nijibu hilo kwanza ili tuendelee vyema.
Ukishajibu hilo, sasa jibu na hili kwa kuwa umelianzisha pazuri kabisa, kwenye historia, Ubantu ulikuja lini pwani ya Afrika ya Mashariki ambako ndiyo chimbuko la Kiswahili?
Naona "argument" yako ya "kuazima" sasa haipo tena na umekubaliana nami kuwa ni kuchukuwa na si kuazima.
Kwa hiyo hapo ukumbuke, ni kuchukuwa na si kuazima kama ulivyofikiria awali.