FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,246
- 123,145
- Thread starter
- #81
Hiyo post ya kwanza ni kiroja tu. Zaidi ya udini wako inaonesha hujui Kiswahili wala Kiarabu, ndio sababu unafikiri kuzungumza Kiswahili fasaha ni lazima ujue Kiarabu (what a shame!).
Hivi ni waislamu wangapi wa Tanzania wanaweza kuongea kiarabu (acha hicho mnachofunza huko madrasa)? Wangapi wanaweza kwenda Riyadh, Madina au Mecca na kuwasiliana na Waarabu bila kuhitaji mkalimani? Kiswahili ni lugha kamili inayojitegemea kama ilivyo kwa Kiarabu. Zote mbili zinakua na kubadilika kwa kadri ya wakati na hazitegemeani. Ufasaha wa lugha moja hauwezi kuletwa na lugha nyingine. Lugha ni sauti za nasibu na ni jamii husika ndio inaamua kipi ni fasaha na kipi si fasaha kulingana na wakati.
Kwa hivyo hoja kuwa mtu hawezi na hatoweza kuzungumza au kuandika kiswahili fasaha kama hajui lugha ya kiarabu, ni hoja unayoweza kuitoa kwenye vijiwe vyenu vya kahawa nje ya misikiti kule kariakoo tu.
Sasa huo "udini" ulioukazania uko wapi? Unanshangaza.
Wewe inaonesha hata maana ya dini hauelewi. Unajuwa kuwa neno "dini" linatokana na Kiarabu? Hata hiyo "nasibu" unaishadidia pia inatokana na Kiarabu. Unalijuwa hilo?
Sijuwi utakikwepa vipi Kiarabu katika Kiswahili. Na ili uwe na lafdhi na kina cha kuelewa maneno basi kama haujuwi kusoma na kuandika kwa herufi za Kiarabu unapitwa na mengi sana.
Hao Waswahili uliowataja wanaanza kufundishwa kusoma na kuandika Kiarabu kabla hawajaenda mashuleni, Hulijuwi hilo? au ni gumu kulimeza?
Utabeza sana lakini mwisho wa siku hutamsikia au kumuona aliyesoma herufi na irabu za Kiarabu kukosea "L" akaweka "R" na aongeapo, utajuwa tu, kuwa huyu ana ustaarabu.
Jee, unajuwa maana ya Ustaarabu?
