Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,817
Umekwepa maswali ya msingi kwani ni wewe uliyeanzisha somo la nani kaja na kakuta nani na si mimi, sasa nnakuuliza kuhusu hayo hayo uliyoyaleta unasema hiyo mada nyingine! Hivi unaelewa ulichokiandika awali, hebu rudi kajisome.
Au umeona hapo hapajibiki ni suicide?
Sasa nnakupa challenge ndogo sana, katika hizo post zako ulizoandika Kiswahili, yatowe maneno yanayotokana na Kiarabu halafu tuone kama tutakuelewa ulichokiandika.
Duh! mpaka sasa naishiwa nguvu nafikiri labda hatuelewani! Kwani kuna mahali nimebisha au nimekataa kwamba Kiswahili hakina maneno ya Kiarabu?
Ngoja nirudie tena kwa mara ya mwisho labda!
Kiswahili ni Lugha ya kibantu kwa 100% ambacho kimeazima maneno kutoka lugha mbalimbali hapa Duniani kikiwemo Kiarabu sasa kama nikitoa maneno ya kuazima siyo tu kutoka Kiarabu bali hata Kiingereza, kireno, Kijerumani n.k sitaweza kuandika nilivyoandika na hii siyo kwa Kiswahili tu, kwa mfano nimesema shule, neno shule ni la Kijerumani sasa nikitoa Shule nitakosa neno la kuweka lkn haimaanishi kwamba Kiswahili kimetokana na Kijerumani!
Leo hii Kiarabu chenyewe pia kinaazima maneno mengi kama Computer, Atom, Quantum, Software, Satellite,Chip, Technology, the Universe n.k sasa ukimwambia Muongeaji wa Kiarabu atoe neno Computer pia atakwama lkn haimaanishi kwamba Kiarabu ni Kiingereza au Kigiriki kwa kuwa tu wanatumia hayo maneno niliyoyataja!