Hapa sibishani nnatoa darsa. Ukinisoma kwa uwazi bila kuwa biased utanielewa tu.
bila kuwa biased? changes begin with who?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hapa sibishani nnatoa darsa. Ukinisoma kwa uwazi bila kuwa biased utanielewa tu.
kiswahili sio kiarabu over
Ni wapi paliandikwa Kiswahili ni Kiarabu?
Kiswahili "si lugha ya asili" halafu tunachukuwa herufi za kilatini ambacho nacho "si lugha ya asili" kuandikia lugha ambayo "si lugha ya asili" tutakielewa kwa kina kweli? nimeweka link hapo juu za magwji waliobobea katika historia ya Waafrika na vyanzo vya lugha ili iwe rahisi watu kuelewa.
Wanasema lugha ni ile yenye "script" sasa lugha ya karibu kabisa na Kiswahili na yenye "script" na iliyotumika awali kuandika na kusoma Kiswahili ni kwa herufi za Kiarabu.
Upo hapo ulipo?
Hii thread imenipa elimu kubwa sana. Ngoja niendelee kuwasoma wataalam wa kiswahili.
Huu mnakasha ulikatika ghafla baada ya Barbarosa ambae aliuchangamsha sana kushindwa kujibu maswali mawili au matatu ya historia, imenisikitisha sana.
Nimesikitishwa na kutokujibiwa hayo maswali kwa kuwa, niltegemea majibu, na sijaelewa kuwa Barbarosa alikuwa anayajuwa majibu ya maswali niliyoyauliza na akahisi kuyajibu inakuwa ni "suicide" kwake au alikuwa hayajuwi na akaona bora asikisie.
Vyovyote ilivyo, kwanza nnampongeza sana kwa kujitahidi kuchangia hoja zake na pili nnasikitika kwa "kuingia kwake mitini" ghafla.
Nimewaita hapa si kutaka kushutumu au kutowa sifa mbaya, bali kutoa darsa dogo sana "if you know you have responsibility", nimejifundisha hayo kwa lecturer wangu mmoja wa mtandaoni kwa jina "Mfundishi".
Barbarosa, binafsi nnahisi nna "responsibility" kubwa sana mbili, moja ya kufikisha kwa wengine yale niyajuayo. Na nyingine ya kujifunza yale nisiyoyajuwa kutoka kwa wanayoyajuwa, hata kama ntatofautiana kwa kuwa tu nilikuwa siyajuwi kabla, basi ntayafanyia kazi ili niyaelewe. Hiyo ndiyo elimu.
Elimu si kurudia yaleyale wanayoyajuwa walewale waliotaka uelewe yaleyale wayatakao walewale.
Labda, tunaweza kutofautiana namna ya kuyafikisha lakini kwa vyovyote hilo ni jukumu langu kufikisha niyajuwayo, na nnauhakika mengi sana si kama yale uliyofundishwa katika elimu yako uliyopitia.
Hali kadhalika nnahisi kila mmoja wetu ukiwemo wewe Barbarosa una "responsibility" ya kufundisha yale uyajuwayo na una "responsibility" ya kujifunza yale ambayo hayajuwi ili uongeze uoana wa muono na elimu yako.
Leo nnawapa zawadi, zawadi yangu si nyingine bali nnawaomba sana, m google video za haya majina nnayowawekea hapa chini ili mfaidike kama ninavyofaidika mimi.
Kwa kuanzia nnawapa hawa wawili tu, mafundisho ni mapana sana na ambayo hutakiwi kuyajuwa na wale waliokufundisha yale.
1) Dr. Booker T. Coleman
2) Mfundishi.
Naomba wasikilizeni sana hao ma lecturer wangu na mta enjoy sana kwa darsa la hali ya juu wanalotowa.
Kuwasikiliza kwenu hao mnaweza kupata kujuwa relation ya lugha tofauti kwa njia tofauti na yenye maana kuliko ile mliyofundisha na wale wale.
Kwenye mjadala wangu sikutaka kwenda deep sana, kwani nnaelewa yataluwa ni mambo na elimu mpya kabisa kwa wengi wenu. Mfano, wengi wenu hamuelewi kuwa Kiingereza siyo lugha ya asili. Kwa sababu gani? Wasikilize hao ma lecturer utapata jibu. Tena kwa kuongezea tu, hali kadhalika kwa Kifaransa na Kihispania. Na zipi zingine? Wasikilize ma lecturer wangu, utafunguka zaidi.
Hiyo ni zawadi yangu kwenu kwa leo. Nyinyi na wengine wataobahatika kuisoma hii post.
kiswahili kimetokana na kiarabu na kibantu? kibantu ndio lugha gani? hakuna bantu language, kuna bantu speaking people, nikimaanisha kuwa kuna lugha ambazo zina muingiliano fulani na ambazo utakuta baadhi ya maneno yanaelekeana ingwawa yaweza kuwa machache sana kiasi kwamba uwezekano wa kuelewana kati ya makabila mawili yaliyo kwenye mkusanyiko wa bantu speaking people.
Kiarabu kama ilivyo kwa lugha nyingine kimechangia kiasi katika maneno ya kiswahili lakini haina claim kwenye kiswahili maana kuazima maneno kutoka kwenye lugha moja kwenda lugha nyingine ni kitu cha kawaida mno duniani
na kwa kuwa kiarabu sio oldest language under the sun then nacho kitakuwa kimeundwa na maneno kutoka katika lugha nyingine kwa hiyo hizo lugha inawezekana ndo zimechangia kwenye kiswahili kwa kupitia mkondo wa kiarabu.
ustaarabu kwa tafsiri ni "civilization" sasa nao hauwezi kuwa confined kwa watu au tabaka fulani..kitu kinachoitwa ustaarabu kwa mmanyema sio lazima kichukuliwe hivyo na m-Danish..bali kila jamii ya watu ina kipimo chao cha ustaarabu...kwa baadi ya watu cannibalism inachukuliw kama kipimo kikubwa cha ustaarabu wakati kwa wtu wengine watajudge kuwa ni barbaric deed!!!
"nina" Kiswahili ni matusi.
wakati mwingine unakuwa na ubishi usio na tija. kwa hiyo neno sukuma ni tusi?
Hebu yaondowe maneno yote yaliyotokana na Kiarabu katika maandiko yako hayo tuone kama tutaelewana. Jaribu.
Naam, tukisema tukisema "kibantu" hatumaanishi kabila fulani tunamaanisha jamii ya wabantu. Na neno kubwa linaloleta muunganisho wa wabantu ni "ntu". Hiyo "ba" ya kabla ni Kiarabu. Kwa maana hiyo, hata neno "Bantu" pia lina ustaarabu.
Maana ya "ustaarabu" si "civilization" kama ulivyoaminishwa na kuamini. Tafuta maana halisi ya neno "ustaarabu" ili likuingie na uelewe. Huwezi na ustaarabu halafu ukawa "cannibal" kwa sababu Waarabu hawana historia ya u "cannibalism".
Historia ya u "cannibalism" kutokea Kaskazini tumeisoma (na ushahidi wa maandishi upo) kuwa imekuja na "crusaders" wa kutokea Uropa.
Ukiijuwa maana kamili ya "ustaarabu" utabadili maandiko yako. Kwa hiyo tafsiri yako ya kulitafsiri neno la Kiswahili kwa Kingereza, neno ambalo 100% linatokana na Kiarabu inazidi kuyakinisha maneno yangu "Nnadiriki kusema leo hii, ili uongee na kuandika Kiswahili fasaha inabidi ujuwe Kiarabu. Bila hivyo utaboronga tu."
Kwa nini neno hilo la linalotokana na Kiarabu ulitolee tafsiri isiyoendana nalo wala isiyoleta maana halisi, kwanini hutafiti kiduchu kujuwa maana yake halisi ni nini ili ulielewe na ulitumie kiufasaha?
Jee, nikusaidie kwa kukufundisha maana halisi ya neno "ustaarabu"?
Nimeuliza kwenye post namba mmoja mstari wa mwisho "Jee, unajuwa maana ya "ustaarabu"?" akheri ya wewe uliyekuwa na ujasiri wa kujaribu kulijibu swali hilo kivyako kuliko wale waliojifanya hawajaliona hilo swali wakaliogopa na kulikimbia.
hivi shule ulienda kusomea ujinga? yaani maana ya neno la kiswahili ulipate kwa Lugha nyingine? Maana sahihi ya neno linatokana na Lugha husika...hata kama ustaarabu kwa kiarabu una maana tofauti na ustaarabu kwa kiswahili hiyo haifanyi maana ya kiarabu ndo iwe sahihi.
Neno ustaarabu ni 100% linatokana na Kiarabu - kumbuka hilo.
Kiingereza na kiswahili madame unasema si halisi.
Je, kiarabu ni lugha ya asili?
Binadamu wote walianzia africa, kwa mujibu wa utafiti sio kama dini zinasema, kwa iyo lugha zote hata hicho kiarabu kilikopa maneno from ancient african languages.
Kiarabu ni asili?