Hebu yaondowe maneno yote yaliyotokana na Kiarabu katika maandiko yako hayo tuone kama tutaelewana. Jaribu.
Naam, tukisema tukisema "kibantu" hatumaanishi kabila fulani tunamaanisha jamii ya wabantu. Na neno kubwa linaloleta muunganisho wa wabantu ni "ntu". Hiyo "ba" ya kabla ni Kiarabu. Kwa maana hiyo, hata neno "Bantu" pia lina ustaarabu.
Maana ya "ustaarabu" si "civilization" kama ulivyoaminishwa na kuamini. Tafuta maana halisi ya neno "ustaarabu" ili likuingie na uelewe. Huwezi kuwa na ustaarabu halafu ukawa "cannibal" kwa sababu Waarabu hawana historia ya u "cannibalism".
Historia ya u "cannibalism" kutokea Kaskazini tumeisoma (na ushahidi wa maandishi upo) kuwa imekuja na "crusaders" wa kutokea Uropa.
Ukiijuwa maana kamili ya "ustaarabu" utabadili maandiko yako. Kwa hiyo tafsiri yako ya kulitafsiri neno la Kiswahili kwa Kingereza, neno ambalo 100% linatokana na Kiarabu inazidi kuyakinisha maneno yangu "Nnadiriki kusema leo hii, ili uongee na kuandika Kiswahili fasaha inabidi ujuwe Kiarabu. Bila hivyo utaboronga tu."
Kwa nini neno hilo la linalotokana na Kiarabu ulitolee tafsiri isiyoendana nalo wala isiyoleta maana halisi, kwanini hutafiti kiduchu kujuwa maana yake halisi ni nini ili ulielewe na ulitumie kiufasaha?
Jee, nikusaidie kwa kukufundisha maana halisi ya neno "ustaarabu"?
Nimeuliza kwenye post namba mmoja mstari wa mwisho "Jee, unajuwa maana ya "ustaarabu"?" akheri ya wewe uliyekuwa na ujasiri wa kujaribu kulijibu swali hilo kivyako kuliko wale waliojifanya hawajaliona hilo swali wakaliogopa na kulikimbia.