Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,817
Kiswahili kabla ya kuja maandiko ya Kilatini kikiandikwa kwa herufi zipi?
Kiliandikwa kwa Kiarabu lakini kuandikwa kwa kiarabu hakukifanyi Kiswahili kuwa Kiarabu! Maandishi hayana uhusiano wowote ule na asili ya Lugha!
Kwa Mfano Kiirani/Kipersia/Kiafghanistani pia vinaandikwa kwa kutumia maandishi ya Kiarabu na Je Kipersia/Kiirani/Kiafghanistani ni Kiarabu? Au unahitaji kujua Kiarabu ili uweze kuongea Kipersia/kiafghanistani?
Hapana Kiirani/Kipersia siyo kiarabu na havina uhusiano wowote ule ingawaje Kiirani/Kipersia kina maneno zaidi ya 50% ya Kiarabu hivyo Kiswahili kuandikwa kwa harufi za Kiarabu au Kilatini hakukifanyi kuwa kiarabu au Kizungu (kilatini) leo hii pia tunaweza tukaandika Kiswahili kutumia alama za Kichina je utasema kwamba Kiswahili ni Kichina?