Huwezi Pinga Kuwa Dini (madhehebu yote) yamegeuka kuwa biashara zinangonya waumini. Kama una hoja utasikilizwa na kujibiwa

Siku moja wakati nipo kijijini nilikuwa natoka kanisani na jamaa mmoja akawa analalamika sana swala la michango kuzidi.....yule mwamba siku hizi nasikiia aliamua kuwa muislam
Shida yetu ukisema ukweli unaonekana eti unataka kuasi kanisa kimsingi unakuwa na hoja na unatakiwa usikilizwe na kujibiwa vyema. Mnashikana mashati halafu Hela zinaliwa ovyo tu. Ukweli michango Kwa Sasa inaogopesha sana.
 
Siku moja wakati nipo kijijini nilikuwa natoka kanisani na jamaa mmoja akawa analalamika sana swala la michango kuzidi.....yule mwamba siku hizi nasikiia aliamua kuwa muislam
Dizain yako kuandika uwongo jambo lionekane zuri ni chap tu,hakuna mtu labda awe mwendawazimu atauza roho yake kwa issue ndogo kama hiyo.

Muulize mleta mada akikaa kimya bila kutoa hiyo anayoiita michango kuna mtu anamfata kumuamsha akatoe?
 
Dini ni Utapeli, dini ni.uzwazwa, dini ni chanzo cha ubaguzi
Kwenye dini na madhehebu ndio maficho ya majambazi, wauaji, watekaji. Waizi na wazinzi.

Dini ni chanzo cha vita, dhambi nyingi zimejificha humo.

Ewe Mtanzania epuka hu utapeli wa mchana kweupe.
Hiyo Mbingu wanayokuhubiria wao hawaitaki? Mbona wanazini na wake za watu, mbona wanaroga, wanazaa nje?
 
Dini ni chanzo cha vita, dini zinakunyima amani ambayo Mungu alikuumba nayo. Angalia Somalia, Sudani, Gaza, Syria na Yemeni.

Dini usiziamini.
Ushoga na usagaji umejificha humo. Kimbia Braza acha kupoteza muda wako.
 
Karibia taasisi zote za dini Zina hizi biashara na michango Iko palepale. Mnanyonywa Hadi basi
 
Nimeshawakomboa watu kama sita wanawake wawili na wanaume wanne, wamenishukuru sana.

Dini na mashehebu ni vyanzo vya kuzalisha hofu na uhasama kwenye jamii.
Mafundishi yao yako hivi

1. Wanakuroga ndio maana huolewi
2. Wanakuroga ndio maana biashara zako zinakufa
3. Wanakuwangia ndio maana unaumwa umwa.
4. Wanakuonea wivu majirani zako ndio maana watoto wamwkuwa wahuni.
5......yaani upuzi mwingi sana. Hata ndugu siku hizi hawakaribishani wala kutembelea kwa hofu ya kurogwa na mikosi
 
Dini zote ni biashara ya kumuuza Mungu asiyethibitishika kuwepo kutatua matatizo yaliyoshindikana kwa watu wasiojielewa.
Eti Mungu ambaye ni Mfalme wa Amani ameshindwa kuleta Amani Gaza, Syria, Congo, Sudani, Somalia, na Tanzania( wasiojulikana).

Huyo Mungu mbona anatia mashaka sana.
 
Eti Mungu ambaye ni Mfalme wa Amani ameshindwa kuleta Amani Gaza, Syria, Congo, Sudani, Somalia, na Tanzania( wasiojulikana).

Huyo Mungu mbona anatia mashaka sana.
Mungu ni chaka tulilolitengeneza wenyewe ili tupate sehemu ya kutupia matatizo yetu yote ambayo hatujaweza kuyatatua tuyafiche humo mpaka tutakapoweza kuyatatua.
 
Pastor Mgogo alishasema mbinguni hakuna account fedha inaliwa hapahapa
Sasahivi ni biashara kabisa kuliko kipindi chochote kile.
 
Alafu Mrogaji Kama Si Jirani Yako Basi Ndugu Yako Wa Karibu,,Rafiki n.k Kwanini Vita Visizuke?Wanachonganisha Watu Huku Mitaani,,Wajitahidi Kuhubiri Upendo Na Kuchapa Kazi Zaidi
 
Mkuu umeandika vingi sana kwa upande wako unaweza kuwa na hoja but kwangu hainiingii akilini,miaka ya nyuma Kanisa Katoliki lilikuwa linapata misaada kutoka nje ila toka 2000s misaada ikakatwa so waamini wenyewe sisi ndiyo tunapaswa kulisimamia,kutoa sadaka hakufilisi kama unatoa kwa akili ulizojaaliwa na Mungu,watu hela tunahonga,tunakula beers michango ya harusi tunachanga vitu vya hovyo kabisa lakini kuiheshimu imani tunashindwa.

Lengo siyo kujisifia,hapo chini nimeenda leo kununua column speakers kwa ajili ya Kanisa lililonilea kijijini kwetu baada ya kuhudhuria ibada mwezi august nikasikia moja ya mipango ya Paroko ni kubadilisha spika zilizokuwepo (za radio) hazifai zinunuliwe nyengine,nimewiwa tu kushiriki ktk hilo na siyo kwamba nina hela nyingi sana.picha nilizipiga kwa ajili ya kumbukumbu zangu ila bahati mbaya sana nazitumia hapa naweza kuonekana kama najivuna but sivyo lengo langu ni ili watu wajue hata kama imani zao zimelala wapo bado ambao zipo hai.
 

Attachments

  • IMG_20241216_151006.jpg
    432.6 KB · Views: 1
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…