Huyo De Gea ni jini!

Huyo De Gea ni jini!

Mfano jana Totenharm kipindi cha pili kwa presha waliyokuwa nayo wangeweza kufunga magoli mawili au matatu golikipa yoyote yule ambaye haitwi De gea
 
Jamani nimevumilia ila nimeshindwa kuzia sifa zangu za dhati kwa goalkeeper hodari wa Manchester United 'Degea'kwa umahiri wake mkubwa wa kuzuia mashambulizi ya Tottenham...Jamaa kaonyesha uwezo mkubwa sana..Hii ndio kazi binafsi pasipo kutegemea timu. Sio shabiki wa Man U ila uwezo wake nimeulewa sana...De gea ni moto wa kuotea Mbali...

Sent using Jamii Forums mobile app
de gea sio goal keeper ni jini
 
Kwahiyo kaka huyu De gea ni Zwazwa tu kama mazwazwa wengine?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kipa mzuri sana tokea akiwa Atletico madrid he was the best.... Ila sio best in the world yupo level moja na kina schmeichel,Ederson,Kepa n.k the best in the world ni Jan Oblak pekee na huo mjadala ulishafungwa tokea 2016 kma De Gea ni the best mnaweza nisaidia kwanini kila mechi anafungwa?? Yaani 259 games 256 conceded..... Alafu kma Jan Oblak sio the best nisaidia kwanini katika mechi 170 ana clean sheets 100!! Yaani ana clean sheets nyingi kuliko mechi alizofungwa?

Mpira ni takwimu sio mahaba
 
De Gea toka amekuja kacheza mechi 259 na ameshafungwa magoli 256 ikimaanisha kwa average anafungwa kwenye kila mechi na ameokoa penalty 2 tu maisha yake yote man U??

Ulipaswa kuweka takwimu hizi (overall) ila wewe kwa ukanjanja wako umeweka za msimu ndomana nikakujibu vile. Hili ndiyo tatizo la Jf kuingiza watu walioujulia mpira kwa kubeti

Tuliza mambupu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haaahaaaa hapana mkuu hakuna siasa tunaenda kwa takwimu..... Oblak hajafungwa goli kwenye mechi 100 katika mechi 170 alizocheza hiyo rekodi nani kawahi iweka?? Wakati huyo De Gea msimu huu katika kila mechi anayocheza anafungwa goli 2+ sasa ana jipya gani??

De Gea ni mzuri ila nachopinga sio best in the world.... Ukipata muda soma uchambuzi wa takwimu then urudi kusema De Gea ndio best

Why Jan Oblak tops David de Gea as world's best goalkeeper
Mkuu ndo maana nkasema stats generation,hizi hua znafunika the bigger picture,mfano stats znasema giroud,sidibe,kimpembe i,mandanda na lloris hawa wote ni world cup winners ila nna uhakika ukiwatupia team yko unayoipenda,wanaweza wakakosa namba lbd lloris anaweza kua sub,
Ishu ya oblak kwnz lig yao ile mechi unaweza ukachek hadi ukasinzia,ila team yke ina ukuta safi nasfia bila shaka,angalia back 4 ya man u asee,daah bila degea sijui ingekuaje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ndio ushabiki kwani De Gea ameanza kudaka wakati wa mourinho?? Shida JF ya siku hizi imevamiwa watu hawana uelewa wa mambo alafu wanataka kuwa wachambuzi

De Gea toka amekuja kacheza mechi 259 na ameshafungwa magoli 256 ikimaanisha kwa average anafungwa kwenye kila mechi na ameokoa penalty 2 tu maisha yake yote man U??

Sasa tuje kwa Oblak.... Kacheza mechi 170 na amefungwa kwenye mechi 70 pekee ikimaanisha hajafungwa mechi 100 sasa unasemaje De Gea ni best in the world??

Njooni na takwimu sio ushabiki..... Huyo De Gea anabebwa na media tu ila kuna makipa hawafikii mfano Ter stegen, De Gea, Handanovic,Donarumma n.k ila kwakuwa mnaongozwa na mahaba basi mnamuona ndio the best.
Hizo takwimu zako ziweke vizuri,vinginevyo nawe ni shabiki tu
Unasema De Gea kacheza mechi 259 na kufungwa magoli 256
Oblak Mechi 170 na kafungwa mechi 70, hapa kwanini usiweke idadi ya magoli kama ulivyofanya kwa De Gea?

Binafsi namkubali sana Jan Oblak na nishabiki wake, uwezo wake hauachi mashaka kabisa.
 
Mkuu,tangu nimeanza kuona michango yako humu JF sijawahi kuona ukichangia pumba kiasi hiki.

Nakusihi katika jina la Yesu uendelee kubaki katika Jukwaa la siasa kwakuwa sipendezwi kuona ukitema Pumba/mataputapu yenye viwango vikali kama hivi.

Hakuna shabiki wa mpira mwenye utulivu wa akili anayeweza kujaribu hata kimoyomoyo tu kumfananisha DDG na kipa yeyote yule hapa duniani kwa sasa!
 
Ni kipa mzuri sana tokea akiwa Atletico madrid he was the best.... Ila sio best in the world yupo level moja na kina schmeichel,Ederson,Kepa n.k the best in the world ni Jan Oblak pekee na huo mjadala ulishafungwa tokea 2016 kma De Gea ni the best mnaweza nisaidia kwanini kila mechi anafungwa?? Yaani 259 games 256 conceded..... Alafu kma Jan Oblak sio the best nisaidia kwanini katika mechi 170 ana clean sheets 100!! Yaani ana clean sheets nyingi kuliko mechi alizofungwa?

Mpira ni takwimu sio mahaba

Kwa Defence ya Manchester United inayolalamikiwa na kila mtu kwa misimu zaidi ya minne hivi sasa, ni vigumu sana kwa kipa kupata clean sheets nyingi, sipingangani na takwimu maana najua ni kweli Jan Oblak anacleansheets nyingi tangu 2014, lakini anapata hizo cleansheets kwa ubora wa mabeki na viungo wakabaji wa Atletico Madrid ( ingawa kwa msimu huu wanamapungufu kwenye defence line yao kama ni mfuatiliaji mzuri wa La Liga utaelewa hili) lakini kwa misimu minne iliyopita Atletico Madrid ndo team yenye defence nzuri kuliko team zote kwenye top 5 best leagues in Europe.
kwahiyo sishangai kuona hizo statistics zikimfavour Jan Oblak, Kama unatakwimu za saves walizofanya unaweza kuweka, lakini under poor defence hata Jan Oblak anaperform vibaya jaribu kuangalia performance yake akiwa Slovenia utaona hilo.
 
Mlete epl huyo ndo utaelewa kama ni mzuri au la ligi ile ni ya timu 3 au 4 ukimuongeza sevilla
Kwa Defence ya Manchester United inayolalamikiwa na kila mtu kwa misimu zaidi ya minne hivi sasa, ni vigumu sana kwa kipa kupata clean sheets nyingi, sipingangani na takwimu maana najua ni kweli Jan Oblak anacleansheets nyingi tangu 2014, lakini anapata hizo cleansheets kwa ubora wa mabeki na viungo wakabaji wa Atletico Madrid ( ingawa kwa msimu huu wanamapungufu kwenye defence line yao kama ni mfuatiliaji mzuri wa La Liga utaelewa hili) lakini kwa misimu minne iliyopita Atletico Madrid ndo team yenye defence nzuri kuliko team zote kwenye top 5 best leagues in Europe.
kwahiyo sishangai kuona hizo statistics zikimfavour Jan Oblak, Kama unatakwimu za saves walizofanya unaweza kuweka, lakini under poor defence hata Jan Oblak anaperform vibaya jaribu kuangalia performance yake akiwa Slovenia utaona hilo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizo takwimu zako ziweke vizuri,vinginevyo nawe ni shabiki tu
Unasema De Gea kacheza mechi 259 na kufungwa magoli 256
Oblak Mechi 170 na kafungwa mechi 70, hapa kwanini usiweke idadi ya magoli kama ulivyofanya kwa De Gea?

Binafsi namkubali sana Jan Oblak na nishabiki wake, uwezo wake hauachi mashaka kabisa.
Stats za Oblak ni kama zifuatazo
La liga kacheza mechi 135
Kafungwa magoli. 80
Clean sheets. 77

De gea
Premier league kacheza 259
Kafungwa goli. 256
Clean sheets. 97

Asilimia ya mechi alizocheza bila kufungwa
De Gea. 37%
Jan Oblak. 60%

Yaani katika kila mechi 100 Oblak hajafungwa mechi 60 ila De gea hajafungwa mechi 37!!!

Kuna hoja inasema defense ya Atletico ndio inamsaidia.... Basi tuone stats za mashuti yanayolenga Goli je huwa wanaokoa mangapi na mangapi yanapenya

Save per goal Ratio

Jan Oblak. 5
De Gea. 4

Yaani ikimaanisha katika kila mashuti 4 kwa De gea goli moja linaingia ila kwa Oblak itahitaji mashuti 5 on target ndio umfunge

Save percentage
Jan Oblak. 85%
De Gea. 81%

Hapo ningependa wenyewe muamue nani ni bora coz numbers don't lie

Source: Transfermarkt , premier league official website,

David De Gea Statistics | Premier League

Jan Oblak - Career Statistics
 
Ni kipa mzuri sana tokea akiwa Atletico madrid he was the best.... Ila sio best in the world yupo level moja na kina schmeichel,Ederson,Kepa n.k the best in the world ni Jan Oblak pekee na huo mjadala ulishafungwa tokea 2016 kma De Gea ni the best mnaweza nisaidia kwanini kila mechi anafungwa?? Yaani 259 games 256 conceded..... Alafu kma Jan Oblak sio the best nisaidia kwanini katika mechi 170 ana clean sheets 100!! Yaani ana clean sheets nyingi kuliko mechi alizofungwa?

Mpira ni takwimu sio mahaba
Quality ya walinzi waliopo mbele ya de gea na oblak ni sawa? Oblak namkubali sana by the way lakini he doesn't face many shots in a game compared to de gea kutokana na ukuta bora wa Diego godin alionao mbele yake

Sent from my SM-A720F using Tapatalk
 
wapumbavu hawa wamesababisha ubingwa tuusikie tu, kwa kuzira kucheza vizuri chini ya Mourinho
 
Quality ya walinzi waliopo mbele ya de gea na oblak ni sawa? Oblak namkubali sana by the way lakini he doesn't face many shots in a game compared to de gea kutokana na ukuta bora wa Diego godin alionao mbele yake

Sent from my SM-A720F using Tapatalk
Mkuu hapo juu nimeweka takwimu ya save peecentage ambayo iko fair kwamba kwa kila shuti unalopigiwa je mangapi huwa yanapita na mangapi yanakuokoa data za transfermarkt zinasema Oblak ana 85% na De gea ana 81%.... Pia katika kila mashuti 5 oblak anafungwa goli moja tu ila De Gea katika mashuti 4 pekee anafungwa goli moja.....

Save per goal ratio ndio kipimo maana haijalishi umepigiwa mashuti mangapi ila wao wanagawanya uliopigiwa na uliokoa mangapi so bado De Gea kazidiwa kwa mbali sana tu kwenye kila kitu.
 
Back
Top Bottom