Huyu abiria wa Mwendokasi kanikera sana, Wabongo tutaacha lini hizi tabia za kueleza mambo binafsi kwenye "public"?

Mwache mwamba atumie Uhuru wa kuzungumza
Tanzania wote ni ndugu naamini abiria wenzake walitamani jamaa aendelee kuongea tu, Tanzania nchi nzuri unaongea kwa uhuru ata kama mtu humjui
 
Ki saikolojia ni jambo zuri anatema nyongo
 
Mleta mada utakuwa mshamba na Dar

Dar unatakiwa ku mind your own business.
Usipende kutega tega misikio yako kama bwege kusikiliza wengine wanaongea nini.

Kifupi wewe una masikio ya umbeya na midomo ya umbeya. kaa mbali na umbeya uwe wa mwendokasi au popote.

Watu wa kuja washamba wa vijijini huko mnatia aibu
 
Mmh kwani ilikuwa lazima kumsikiliza sema na wewe ulitega sikio sanaaa ukanogewa na story za jamaa
 
Afya ya akili ni muhimu sanaa (punguza kubeba yasiyokuhusu na kupeleka kwingine)
 
Jf members wote tunamiliki magari yetu binafsi wewe ulitakiwa uwe mwanachama wa fb cause hauna gari
Te te te te nimesoma comments zote nimeona za kawaida tu kwa kuwa imenionesha levo zao za ufikiri, ila hii imenifanya nicheke, asante sana kwa kunipa tabasamu. Nami nitapambana ninunue gari langu.
 
Hadi muda huu mleta mada ashakimbia uzi wake maana sio kwa kashda hizi
😂😂😂😂😂
Nipo nasoma spana ninazopigwa, nasoma kwa umakini sana sana sana
 
Ndio nimeingia Dar wiki iliyopita bwana mkubwa.
 
Wacha kulalamika ,tafuta pesa ununue usafiri wako binafsi. Kama unaona mwendokasi jau ,ita uber ikupeleke unapokwenda uache kupangia watu maisha.
 
Kama unakereke nunua lako tu mbona kule kwenye madaladala wanagonga singeli kwa kwenda front tena full blast hamsemi? uhuru umerejea baada ya jiwe kufa, ukute alikua jela sasa ameamua kutumia uhuru wake vyema kabisa katika nchi ya mama yenu
 
Nipo nasoma spana ninazopigwa, nasoma kwa umakini sana sana sana
Achana na wahuni wa jamiiforums hawa wanaojifanya wote wanamiliki magari.

Wengine makapuku tu wanaoshindia mihogo.

Lakini ndio hivyo tena kwenye mitandao tunavumilia every tom and jerry.
 
Wacha kulalamika ,tafuta pesa ununue usafiri wako binafsi. Kama unaona mwendokasi jau ,ita uber ikupeleke unapokwenda uache kupangia watu maisha.
Uko sahihi mtu anakerwa kwenye basi badala ya kutoka kwenye basi na hasira za kutafuta pesa anunue gari yake binafsi anatoka na hasira ya kilichomkera kwenye basi

Mimi kuna siku basi limejaa tumesimama wima tumejazana kibao abiria mmoja akanikanyaga mguuni nikamwambia mbona unanikanyaga.Akanijibu kama hutaki kukanyagwa kwa mjazono huu shuka kakodi taxi .Nilinyamaza kimya nilishuka na hasira kuwa lazima nitafute gari yangu binafsi niepukane na hiyo adha.Na ndoto alitumia

Ukikerwa nyumba ya kupanga usiwe na hasira na wapangaji au wenye nyumba katafute yako.Hasira zipeleke kwenye kutafuta yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…