Leo asubuhi wakati nimepanda mwendokasi kuna mwamba mmoja nimekutana naye siyo mara ya kwanza mimi kumkuta kwenye gari, nadhani kama sijakosa itakuwa mara ya pili au tatu.
Sasa huyu mwamba alikuwa akipiga stori na mtu aliyekuwa amesimama naye karibu, nadhani wanafahamiana, sasa huyo jamaa ninayemzungumzia hapa akawa ndio msemaji mkuu, yule mshkaji mwingine akawa anaitikia tu au kuchombeza kidogo kidogo.
Kwa kuwa asubuhi kulikuwa na utulivu na asilimia kubwa ya abiria tukawa tunawaza mishe zetu tunazoenda kuzifanya kwenye purukusani zetu, jamaa akawa anazungumza kwa sauti kubwa, siyo kubwa kiasi cha kukera, Hapana ila ilikuwa kubwa kiasi ambacho wote waliomzunguka ni kama wanamsikiliza yeye.
Jamaa akaanza kuwa anazungumza kuhusu maisha yake binafsi, mara yeye na mkewe mara majirani zake, mara fulani kafanya hivi na ningekuwa mimi ningefanya hivi.
Yaani kwa ufupi ni kama alikuwa anawasimulia watu ambao hata hawamjui kuhusu mambo yake binafsi, kibaya zaidi stori nyingine zikawa unaona kabisa hii ni uwongo ila anaongeza chumvi ili aonekane mwamba, ni ushamba tu.
Hii michongo ya kuzungumza mambo yetu binafsi Watanzania sijui tumeitoa wapi, yaani likitokea tukio kidogo tu mtu anadakia na kuanza kuelezea “Mimi ni hivi…” mara utasikia “Achana na hiyo, mimi yalinikuta…”
Wabongo tuache ushamba, kwani mtu hauwezi kuzungumza kwa sauti ya chini tu na ukasikika na huyo uliyenaye karibu yako, unaongeza sauti ili watu wakusikilize wewe ili iweje, tena wengine wanaenda mbali na kuzungumza kuhusu maisha yao binafsi kabisa na kuhisi ni sifa.