Huyu anayemfatilia Heche na ndiye aliyehusika October 29.

Haya mambo sio yakuchukulia kwa mzaha, hawa wahuni imeshaonekana wanafanya kazi ya kuua kwa kujiamini kwasababu wanafahamu watalindwa na mamlaka.

Heche awe makini sana, aongeze ulinzi wake binafsi, kuonesha kujiamini kwa kauli pekee bila matendo hakutoshi, hawachelewi kumuumiza au kumpoteza kabisa kisha tuanze kulia bila kusikilizwa.
 
Hahahaha....! Heche mwenyewe nasikia yuko upande uleeee!!
 
Hoja ya usalama wa viongozi wa kisiasa na watu wenye ushawishi katika jamii inapaswa kuchukuliwa kwa uzito. Ikiwa kuna viashiria au hofu za vitisho, ni muhimu wahusika kuchukua tahadhari zinazostahili na vyombo vya ulinzi na usalama kufanya kazi yake kwa weledi na bila upendeleo. Hata hivyo, ni vyema kuepuka hitimisho kuhusu nani anahusika bila ushahidi au uchunguzi rasmi. Kinachohitajika ni mazingira ambayo kila mtu anajisikia salama na sheria inalinda haki za wote kwa usawa.
 
Nimekusoma vzuri ila ulipogusia "vyombo vya ulinzi na usalama" ndio ukaharibu.

Vyombo vipi hivyo vya "ulinzi na usalama" ikiwa watanganyika tunaendelea kutekwa kwa zaidi ya miaka miwili sasa?

Hivyo vyombo vya "ulinzi na usalama" havitukindi sisi, naamini vibawalinda wanaoututeka na kutuua ndio maana bado wanaendelea na mateso yao kwetu bila hofu yoyote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…