Huyu binti maisha yake hayatakuwa sawa tena

Usizichezee dini zinazomuabudu Mungu, naamini kwamba kufanya hivyo kunamfanya mtu akose baraka katika maisha yake ya hapa duniani.
 
Hiyo picha siyo yeye na maaskofu wa katoliki?
Awe mkatoliki au asiwe mkatoliki, Kwenda Kinyume na maagizo ya Padre, Achilia mbali Askofu, Askofu Mkuu au Kanisa kiujumla, Ni kukosa utii, Ni kinyume kabisa na mafundisho ya kiimani ya Katoliki, Achilia mbali kuthubutu kuitisha press kabisa! Tena kumsema Askofu! Kuna taratibu za ndani ya Kanisa kuhusu masuala ya kiimani, Sio kuitisha press! Kanisa limepewa mamlaka likifunga duniani, na mbinguni imefungwa! Ngoja tuone.
 
Kwa hiyo kuna udikteta na ukosefu wa haki katoliki?
 
Kwa hiyo kuna udikteta na ukosefu wa haki katoliki?
HAPANA, ila 'Utii' ni jambo la msingi sana, ndiyo maana watawa wote hula kiapo cha 'utii', Hata Mungu anapenda utii, Ndiyo maana dhambi ya Adam na Eva ilikuwa kukosa utii na ndiyo sababu wakafukuzwa Eden, Licha ya hivyo, sijamaanisha mawazo tofauti ni kukosa utii, bali kuna taratibu za ndani kufikisha mawazo yako kwa viongozi wa kiroho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…