Huyu dada simuelewi

Huyu dada simuelewi

niliwahi kukutana binti kariakoo kavaa baibui vizuri kabisaa, sheli flani hivi kuna ATM nilipita kuchota visenti kidogo mida ya saa1 usiku..

baada ya kutoka kwa ATM hatua kama 5hivi mbele yangu nikawa kama napishana nae hivi nae akawa kama ananiblock, nikasimama...

straight alinisalimia na akanambia kaka naomba kama una sh.elfu5, huku akinitazama na long smile 🐒
🤣🤣🤣Hujamalizia,Kwa hiyo ukafanyaje?ukampa au ukakemea pepo?
 
🤣🤣🤣Hujamalizia,Kwa hiyo ukafanyaje?ukampa au ukakemea pepo?
nilipata hofu kuu na lakini ghafla,
nikajawa na Roho mtakatifu na nikawa jasiri kupindukia, huku nikikemea kimoyomoyo nikamjibu kiungwana kabisa -Pole, Sina....

akalegeza shingo upande moja kwa smile lile lile, akimaanisha kukubali pole na sina yangu kwa shingo upande.....
akaendelea alikokua anaenda...

huku nami nikiendelea kukandamiza maombi ya nguvu na kukemea, nikitembea bila kugeuka nyuma kuelekea nilipokua nimepaki starlet yangu ilioyonitoa kimaisha 🐒
 
Dah,huu mji una mauzauza sana,zamani nilikuwa naamini katika kusaidia wahitaji ninaokutana nao,ila saa hivi nimekuwa na roho ngumu sana,yaani mpaka niguswe kwelikweli yaani maana mambo ni mengi
 
Dah,huu mji una mauzauza sana,zamani nilikuwa naamini katika kusaidia wahitaji ninaokutana nao,ila saa hivi nimekuwa na roho ngumu sana,yaani mpaka niguswe kwelikweli yaani maana mambo ni mengi
ni pagumu kidogo,
waombaji misaada wengi hawaaminiki, wanawatia hofu watoaji 🐒
 
Leo nilikua kwenye ktuo kimoja cha mabasi ya mikoani, nikiwa nikisubiri usafiri wa kunipeleka mkoa x; wakati nikisubiri gari, nilikaa kwenye kimeza kimoja karibu na mchoma mishikaki na chipsi, nikiwa napata pepsi huku tukibadilishana mawazo na baadhi ya abiria.

Ghafla akatokea dada mmoja ambaye simfahamu, amevaa baibui nyeusi huku amefunika hadi kichwa na kuachia sehemu ya uso tu ionekane; akaja kwenye ile meza yetu na kuvuta kiti, kisha akanijulia hali.

Baada ya kama dakika tatu hivi, yule dada akaniomba nimnunulie chipsi, kwa kuwa sikuwa nimejiandaa nikamwambia achukue chipsi kavu; mara ghafla akamwambia yule wa jikoni ampatie chipsi mayai na pepsi ya 'take away'.

Sisi tukabaki kumtazama tu, mara basi nililokuwa nalisubiri nalo likafika, nikamwambia yule dada mi naondoka; akaniuliza unaenda wapi? Nikamjibu naenda mkoa x, akamuita yule kijana ili nilipe bili; nami nikalipa nikaondoka.

Wakati naondoka, akanifuata kijana mmoja ambaye naye tulikuwa tumekaa naye pamoja; akaniuliza,mbona yule dada simuelewi elewi, inakuwaje mtu hamfahamiani afanye vile; mi nikamjibu hata mimi mwenyewe naona kama miujiza tu.

Yule kijana akaniambia, inawezekana labda ni majaribu tu, huwezi jua; inawezekana ikawa njia ya fursa huko mbeleni,mara mafursa ya maokoto yakafunguka.

Nikabaki nacheka tu. Ila kiukweli, mpaka sasa bado natafakari hiyo sinema.​
ni jini hilo, umelinunulia chipsi za kufuturu. mwezi huu majini mengi nayo yamesambaa, na yamefunga. wanaoyafuga wanajua hilo. jiandae usiku litakuja.
 
ni jini hilo, umelinunulia chipsi za kufuturu. mwezi huu majini mengi nayo yamesambaa, na yamefunga. wanaoyafuga wanajua hilo. jiandae usiku litakuja.
Alikula pale pale na ilikuwa saa kumi kasoro jioni; na je, nisingemnunulia kungetokea nini?
 
We bwana umejirahisisha sana dah umetufedhehesha wanaume we hata kukaza kidogo mambo gan haya mbavu
 
Kaka kaka kama humuelewi huyo mdada wewe chonga na mzizimkavu tuu inatosha 😂😂😂😂😂😂
 
We bwana umejirahisisha sana dah umetufedhehesha wanaume we hata kukaza kidogo mambo gan haya mbavu
Wanasema si vizuri kumuacha binadamu mwenzako afe kwa njaa, huku ukiwa na nafasi ya kuweza kumsaidia. Ni sawa na kuchangia mazishi kwa gharama kubwa, huku wakati wa kuuguza ulishindwa kuchangia ata panado.
 
Back
Top Bottom