Huyu dereva bodaboda na hii treni walikuwa wanarekodi sinema au ni tukio la kweli?

Huyu dereva bodaboda na hii treni walikuwa wanarekodi sinema au ni tukio la kweli?

TODAYS

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2014
Posts
14,747
Reaction score
24,250
Kuna kipande cha sinema kinasambaa sana kikimuonyesha afisa Usafirishaji a.k.a bodaboda akilazimisha kupita mbele ya treni iliyo kwenye mwendo.

Screenshot_2023_0405_223232.jpg


Ila naona hiyo treni ikasimama gafla kitu ambacho sikuwahi na sijawahi kuona wala kushuhidia breki za haraka za treni kuwa sawa na gari.

Nashangaa dereva toyo alishuka kama pikipiki imedondoka tu pembeni ya nyasi na wala hakushtuka alikuwa anajivuta kutoka kwenye toyo yake.

Screenshot_2023_0405_223344.jpg


Kama kuna mwenye hiyo sinema anaweza kuitupia hapa wadau waichakate.
 
Jambo la ajabu waliokuwa Wanarekodi ni kama walijiandaa na simu zao, sababu kuna angle mbili tofauti (mbele na nyingine nyuma) baada ya kuangalia hiyo clip.
 
Kuna kipande cha sinema kinasambaa sana kikimuonyesha afisa Usafirishaji a.k.a bodaboda akilazimisha kupita mbele ya treni iliyo kwenye mwendo.
View attachment 2577849
Ila naona gafla hiyo treni ikasimama gafla kitu ambacho sikuwahi na sijawahi kuona wala kushuhidia breki za haraka za treni kuwa sawa na gari.

Nashangaa dereva toyo alishuka kama pikipiki imedondoka tu pembeni ya nyasi na wala hakushtuka alikuwa anajivuta kutoka kwenye toyo yake.

View attachment 2577850
Kama kuna mwenye hiyo sinema anaweza kuituoia hapa wadau waichakate.
TREN Haina breki za hivyo mkuu
 
Ipo Video nyingine sikumbuki niliona wapi aidha humu jamvini au yutyub ambayo ilikuwa inaonyesha watu wa mitaani; wakihojiwa kuhusu Katiba na kwanini wanahitaji katiba mpya, Aiseee utaona kabisa watu wakitafuta script ilipo(wakipepesa kwa macho) wengine wanaangalia chini pembeni juu n.k na hata kuona kuna sehemu kana mtu amerudia kurekodi yaani kana imeunganishwa! Hii ilikuwa baada tu ya mikutano ya kwanza ya hadhara....

😄😂😂😅

Tutaona mengi
 
TREN Haina breki za hivyo mkuu
Ngoja nikuweke sawa kidogo kwanza unaposema treni maana yake ni locomotive na mabehewa yake. Sasa hiyo locomotive huwa na breki za aina 4.

1. Independent brake hii hutumika wakati locomotive ikiwa peke yake bila mabehewa na ni ya haraka zaidi.

2. Automatic brake hii hutumika locomotive ikiwa na mabehewa yake sasa hii kidogo huchukua muda kufanya application ndiyo hupelekea kupata long distance ili kusimama kwasababu mabehewa hayasimamishwi ghafla yanaweza kuanguka.

3. Dynamic brake hii ni brake ya kiumeme hutumika kupunguza mwendo wa treni siyo kusimama.

4. Parking brake hii hutumika locomotive ikiwa katika hali ya kusimama pasina matumizi tena au wakati wa matengenezo.

Sasa basi hilo tukio unaloliona hapo hiyo treni kwanza ilikuwa na behewa moja (passenger coach) pili haikuwa na speed kubwa kabisa ndiyo maana huyo locomotive driver aliweza kuidhibiti kwa urahisi sana ingekuwa na speed hata 20km/h huyo asingepona.
 
Back
Top Bottom