Huyu fundi wa hizi sarakasi ni nani?

Huyu fundi wa hizi sarakasi ni nani?

Sema nimegundua Mshana una hekima sana. Big up.

Sasa, naona baada ya kumchomoa baba askofu unataka kumchomoa aijipii [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
[emoji2][emoji2][emoji1545][emoji1545][emoji1545] Hao ni wamoja na lao ni moja! Lakini je wako pekeyao ama nyuma yao kuna iceberg?[emoji848][emoji2984][emoji2827]
 
Nidadavulie
Btn lines mwanzoni umedadavua barabara, lakini mwishoni kuhusisha unawake kuwa umedhauliwa kwa kuwa eti labda mwenye kutuhumiwa ni mwanaume na maagizo /amri ya kukamatwa amepewa mwanaume sioni mantiki yeyote.

Alichohitaji IGP ni official document inayoelezea tuhuma dhidi ya Bishop ili wao waweze kutekeleza maagizo. Na sio kwamba wao kama Jeshi la Polisi hwafahamu alichosema Bishop wanajua ndio maana wanataka maandishi ili walinganishe na walichonacho kama vinaendana waweze kumtia hatiani.

Tukumbuke pia Waziri naye anaweza kukosea kwa kutoa amri isiyokuwa na ushaidi hivyo kuliweka Jeshi la Polisi na Takukuru kwenye lawama nyingine mbaya zaidi kuliko issue yenyewe ya chanjo.

Lakini pia yawezekana Jeshi la Polisi limeona kuna nguvu kubwa inayotumika unayotumika kutoa elimu ya chanjo bila kutumia busara na kusababisha wenye Wizara kuparanganyika juu ya nini kifanyike.

Ndio maana IGP Siro akashauri apelekewe maandishi ili kama kuna chochote wajadiliane na wafikie hitimisho pasipo kuleta taaruki ya kusababisha Wananchi kugawanyika pande mbili au zoezi zima kupoteza maana.

Ni wazi kabisa Mh. Waziri alikuwa na jazba kiasi cha pengine kutoa maelekezo yaliyo nje ya kiapo chake.
 
Btn lines mwanzoni umedadavua barabara, lakini mwishoni kuhusisha unawake kuwa umedhauliwa kwa kuwa eti labda mwenye kutuhumiwa ni mwanaume na maagizo /amri ya kukamatwa amepewa mwanaume sioni mantiki yeyote....
Fursa Pesa hebu msome Malisa hapa

Nakumbuka Makonda amewahi kuwaagiza polisi kumkamata Mbowe baada ya kumtaja kwenye orodha ya madawa ya kulevya. Sirro hakusubiri maandishi. Makonda huyohuyo akaagiza Aabdul Nondo akamatwe kwa tuhuma za kujiteka. Sirro hakusubiri maandishi, licha ya kwamba yalikua maelekezo ya Mkuu wa mkoa tu. Leo Waziri katoa maelekezo anasema anasubiri maandishi?

Anyway ni barua gani Sirro alipewa kuwakamata vijana wa Chadema waliokua ibadani huko Mwanza juzi jumapili? Je Sirro alipewa barua na nani kumkamata Askofu Mwamakula na Prof.Azavel Lwaitama usiku wa manane hotelini kama majambazi na kuwaweka rumande bila hatia? Sirro alipewa barua na nani kuwakamata vijana wanaokwenda mahakamani kufuatilia kesi ya Mwenyekiti Mbowe? Why these double standards?

Credit: Malisa GJ
 
Fursa Pesa hebu msome Malisa hapa

Nakumbuka Makonda amewahi kuwaagiza polisi kumkamata Mbowe baada ya kumtaja kwenye orodha ya madawa ya kulevya. Sirro hakusubiri maandishi. Makonda huyohuyo akaagiza Aabdul Nondo akamatwe kwa tuhuma za kujiteka...
Anyway sina majibu ya maswali hayo ☝

Ila ninachoweza kusema labda pengine ukamataji wa Polisi unategemea iwapo kuna viashiria vya kijinai au kukamata kwa ajili ya kutawanya.

Issue ya chanjo yaweza kuwa ni tofauti kabisa na tuhuma nyingine ambazo pengine wao kama Jeshi la Polisi wameona linahitaji majadiliano zaidi, la sivyo linaweza kuingia kwenye lawama pasipo kujua.

Anyway ebu tusubili, yawezekana barua itapokelewa mapema leo.
 
Andiko zuri ila para yako ya mwisho ni uchochezi dhidi ya Sirro
Sirro mwambie kuna kongamano la Chadema, tena bila barua yaani aone tuu mtandaoni kwamba kesho Chadema wana kongamano utaona kama atasubiri barua...
 
Sirro kadinda?! Sirro must go!
Ndugu mheshimika sana mkuu kabisa.na mtu muhimu sana sana kwa hofu kuu na heshima iliyopita viwango vyote na taazima hasa
Nachukua nafasi hii adimu na azimu kwanza kwa kukuomba lazi kutumia muda wako huu lakini pia kukuomba ukamshike yule bwana na kumficha kwenye ghala lako halafu tutalipa gharama zote pamoja na usumbufu na bakshish
 
Ndugu mheshimika sana mkuu kabisa.na mtu muhimu sana sana kwa hofu kuu na heshima iliyopita viwango vyote na taazima hasa
Nachukua nafasi hii adimu na azimu kwanza kwa kukuomba lazi kutumia muda wako huu lakini pia kukuomba ukamshike yule bwana na kumficha kwenye ghala lako halafu tutalipa gharama zote pamoja na usumbufu na bakshish
Duh, sidhani kama anaweza kubembelezwa namna hiyo maana waziri ni zaidi ya IGP. Na Sirro akiiona barua kama hiyo anaweza kupandisha mabega akasema waziri asubiri apate taarifa za kiintelejentsia!

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
Duh, sidhani kama anaweza kubembelezwa namna hiyo maana waziri ni zaidi ya IGP. Na Sirro akiiona barua kama hiyo anaweza kupandisha mabega akasema waziri asubiri apate taarifa za kiintelejentsia!

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
Inategemea maana kuna watu kama CDF, IGP, DG, Gavana wa Benki Kuu etc wakati mwingine wapo chini ya Katibu Mkuu na wala si Waziri ila kuna wakati wapo juu ya Waziri. Inategemea situation ni ipi.
 
Nahisi sirro amechoka kuwa kichaka kwa maovu ya wa2 wengne watakao mgeuka kutetea ugali wao.hii inajidhihrxha waz! Bcoz yeye katoa msimamo kama yeye na familia yake yaan kanisa.sasa wewe unatafuta nini? Na kipi kinakuwasha kufuatilia na kumkamata ni kumpa umaharufu.mwisho wa siku gwajma atakuwa rais.na rais kashashtukia hlo
Haswaaaa tena aanzee kula jaramba mapema..gwajima ndo rais ajae..hatutak mijitu isiyokuwa na misimamo na kusismamia wanachokiamn raia wake.
 
Baada ya rais mstaafu Jakaya Kikwete kurudi tena madarakani kwa mara ya pili alifanya jambo ambalo lilishutumiwa sana.. Alikusanya watendaji wa serikali karibia wote na kwenda kufanya semina elekezi kwenye hotel ya kifahari ya Ngurdoto mkoani Arusha
Kiuhalisia maudhui ya semina naweza kusema kwamba hayakupewa kipaumbele zaidi ya watu kula bata kwa raha zao...Hakika usemi wa kazi na bata ulipata umaarufu sana kipindi kile..
Ukiachana na mapungufu ya ile semina lakini watendaji wale walitoka pale na kitu kikubwa sana! Kule kuwakutanisha nje ya taratibu zao za kawaida za majukumu ya kila siku kulisaidia sana kuwajenga na kuwaleta pamoja na kuwafanya kuwa kitu kimoja
Semina elekezi hizi ziliendelea kila wakati kwa kipindi chote cha utawala wa JK.. Hawa watendaji walipata nafasi ya ku relax, kupunguza uchovu,kutoa stress kufahamiana kwa karibu nje ya taratibu za kazi nknk

Baada ya Kikwete kumaliza muda wake alimkabidhi kijiti marehenu hayati Magufuli....Huyu alifuta kila kitu... Si senina elekezi wala makongamano makazini... Maono yake hayakuwa ya JK! Watendaji lile bata la JK likakoma na kuanza kutimiza majukumu yao kwa pressure kubwa..na hata kama kulikuwa na semina au kongamano kukawa tena hakuna bajeti za vyakula na kumbi za kukodi..mambo yaliishia idarani tena kwa maji na biskuti ikawa sasa sio KAZI NA BATA tena bali HAPA KAZI TUU..!

Haya mambo ya sasa ya watendaji kupishana kauli ama kila mmoja kuongea lake ni matokeo ya kauli mbiu ya hapa kazi tuu.. Na wala hayakuanza sasa..huu ni mwendelezo tuu toka enzi za mwendazake

Huu mgongano wa kauli na kulifungia gazeti la chama kwa siku saba ni matokeo yaleyale ya kukosekana mawasiliano, umoja na kujitambua kwamba nani anapaswa kufanya nini kusema nini na wapi! Nikikumbuka matamko ya watendaji wakati wa Magufuli nabaki tu kucheka...! Hakuna aliyekubali kuwa chini ya mwingine bali kila mmoja alijitahidi kutoa tamko kali kuliko mwenzake ili kumfurahisha bwana Mkubwa
Sakata la mchungaji Gwajima aliyeichokonoa serikali vilivyo limechukua sura mpya baada ya serikali kupitia waziri wa afya kutoa amri/agizo la kukamatwa Gwajima mchungaji na jeshi la polisi ambalo ni organ ya serikali

Mkuu wa jeshi la polisi bila fikra na tafakuri alipoulizwa kuhusu kukamatwa Gwajima alisema hajapata wito rasmi wa maandishi toka serikalini, lakini hata hivyo akaenda mbali na kutoa ushauri na maelekezo... Kwamba hata akipokea oda ya kumkamata Gwajima mchungaji basi wataangalia kama kuna jinai na kama basi ipo jeshi la polisi litashauri wamalizane kwa njia ya mazungumzo!
Kwanza mzee Sirro ajue kwamba hili si suala la ndugu wawili mtu na shemeji yake hata atoe ushauri 'wamalizane wenyewe' hili ni la kiserikali
Pili mzee Sirro alikuwa kwenye nafasi nzuri kabisa kujibu kuwa wanafanga mawasiliano na wizara au na waziri ..! Full stop! Mengine yote aliyoongea hayakuwa mahali pake! Je wakati wa kayafa angefanya hivi?

Mawasiliano ya watendaji yanafanyika mitandaoni na bila kuwasiliana kwanza..yaani ni kama kuna kuoneshana ubabe na ujuaji!
LAKINI ukiachana na hayo yote kuna tatizo kubwa huko ndani, waziri ni mdomo wa rais, akisema waziri ni agizo la serikali lenye ridhaa ya rais na organs za serikali zinachotakiwa kufanya ni KUTEKELEZA KWANZA!
Kuna dharau juu ya wanawake inajitanabaisha hapa na kuna kikundi ndani ya mamlaka hakikubali kuongozwa na wanawake! Je Gwajima na Sirro ni sehemu yao?
Kwa thread hii umeniangusha M/KITI.Alichosema IGP ni sahihi kabisa,taratibu zifuatwe wala hajamdharau huyo mama.
 
BROTHER KAKA! Huu uzi ebu angalia namna ya kuuboresha au kuufuta!

Jeshi la polisi linapomkamata mtu, LAZIMA Limfikishe mahakamani kwa mujibu wa sheria!
Hivyo LAZIMA LIPELEKE USHAHIDI MAHAKAMANI!
Sasa linapokamata watu bila jinai, huko MAHAKAMANI Polisi watatoa ushahidi gani?
HALAFU NDO NYIE NYIE POLISI WAKIBANWA MBAVU HUKO MAHAKANI MNASEMA HAWANA AKILI YA KUTOA UTETEZI!

SIRRO YUPO Sahihi 100% ; Jeshi la polisi pamoja jukumu la ukamataji, lakini hutazama jinai kwanza, kama hakuna jinai hushauri njia nyingine!

KUWA NA NYUNDO haimaanishi Uue kila kitu kwa Nyundo! Wadudu kama Inzi zipo njia zingine za kuwaondoa! Ukitumia Nyundo unaweza hata kuvunja na meza yenyewe!

UZI WAKO UNACHONGANISHA JINSIA NAOMBA UFUTE KWA HESHIMA YAKO MJOMBA WANGU brother kaka

Polisi wanasubili yule mlalamikaji wa video ya ngono! Kama unamjua toa ushirikiano
Hivi maidhui ya mwandishi ni hicho ulichokieleza wewe kweli?

Ni mara ngapi 'system' imelalamikiwa kubambikia watu kesi?

Je wabambikiwa makosa huwaga kuna ushahidi dhahiri wa kiuchunguzi wa kuwaswendema ndani?

Hili neno kubambikia lina tafsiri gani?

Mi namuunga mkono Mshana na wala asijishughulishe na kufuta futa uzi hapa.

Siro hakutakiwa kujadili ama kutoa maoni aliyoyatoa kwenye interview hiyo kwa sababu huko nyuma( awamu ya5)hakujadili hata dakika moja kuchukua hatua kwa yeyote popote na bila maelezo ya uchunguzi wa jinai kufanyika kwanza, uchunguzi ulifanyika watu wakiwa ndani.

Yaani kumekuwa na Siro wawili kwenye wadhifa mmoja katika serikali za awamu mbili?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom