Huyu fundi wa hizi sarakasi ni nani?

Huyu fundi wa hizi sarakasi ni nani?

Huyo siro kauli tu ya makonda alikuwa anatekeleza ka mjinga flani I wonder hii ya Waziri. Siro ajistaafie tu kwa heshima uu U Igp
Sirro hakubaliani na hayo machanjo! Hayuko upande wa support ukiona hivyo, angekuwa huko basi Gwajima angeamkia selo😂 kwa kifupi hii vita haina maslahi kwake!
 
Sirro gwajiboy wanadharau wanawake wamezoea huko kwao kutesa wanawake
Msijishushe, huyu mama kwanza hana adabu, haikuwa na sababu kumtemea mbovu Gwaji hadi kutaja mambo ya ngono na kukandia imani yake. Sngesema tunsmuhitaji athibitishe hiyo rushwa.
Msijifiche kwenye kivuli cha mwansmke...subirini spana j2[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Lazma ataliamsha dude yule msukuma hawez kumuacha mama ashinde kizembe[emoji23]
Atafunua hadi ya gizani tusiyoyajua...na atampa onyo kuwa akirudia atamalizia kupasua jipu.....Gwajiboy aka Rashid ni shida, Pengo anamjua, na Makonda skimkumbuka anahisi kuharisha[emoji28][emoji28][emoji28]
 
Baada ya rais mstaafu Jakaya Kikwete kurudi tena madarakani kwa mara ya pili alifanya jambo ambalo lilishutumiwa sana.. Alikusanya watendaji wa serikali karibia wote na kwenda kufanya semina elekezi kwenye hotel ya kifahari ya Ngurdoto mkoani Arusha.

Kiuhalisia maudhui ya semina naweza kusema kwamba hayakupewa kipaumbele zaidi ya watu kula bata kwa raha zao...Hakika usemi wa kazi na bata ulipata umaarufu sana kipindi kile.

Ukiachana na mapungufu ya ile semina lakini watendaji wale walitoka pale na kitu kikubwa sana! Kule kuwakutanisha nje ya taratibu zao za kawaida za majukumu ya kila siku kulisaidia sana kuwajenga na kuwaleta pamoja na kuwafanya kuwa kitu kimoja
Semina elekezi hizi ziliendelea kila wakati kwa kipindi chote cha utawala wa JK.. Hawa watendaji walipata nafasi ya ku relax, kupunguza uchovu,kutoa stress kufahamiana kwa karibu nje ya taratibu za kazi.

Baada ya Kikwete kumaliza muda wake alimkabidhi kijiti marehenu hayati Magufuli....Huyu alifuta kila kitu... Si senina elekezi wala makongamano makazini... Maono yake hayakuwa ya JK! Watendaji lile bata la JK likakoma na kuanza kutimiza majukumu yao kwa pressure kubwa..na hata kama kulikuwa na semina au kongamano kukawa tena hakuna bajeti za vyakula na kumbi za kukodi..mambo yaliishia idarani tena kwa maji na biskuti ikawa sasa sio KAZI NA BATA tena bali HAPA KAZI TUU.

Haya mambo ya sasa ya watendaji kupishana kauli ama kila mmoja kuongea lake ni matokeo ya kauli mbiu ya hapa kazi tuu.. Na wala hayakuanza sasa..huu ni mwendelezo tuu toka enzi za mwendazake.

Huu mgongano wa kauli na kulifungia gazeti la chama kwa siku saba ni matokeo yaleyale ya kukosekana mawasiliano, umoja na kujitambua kwamba nani anapaswa kufanya nini kusema nini na wapi! Nikikumbuka matamko ya watendaji wakati wa Magufuli nabaki tu kucheka.

Hakuna aliyekubali kuwa chini ya mwingine bali kila mmoja alijitahidi kutoa tamko kali kuliko mwenzake ili kumfurahisha bwana Mkubwa.

Sakata la mchungaji Gwajima aliyeichokonoa serikali vilivyo limechukua sura mpya baada ya serikali kupitia waziri wa afya kutoa amri/agizo la kukamatwa Gwajima mchungaji na jeshi la polisi ambalo ni organ ya serikali

Mkuu wa jeshi la polisi bila fikra na tafakuri alipoulizwa kuhusu kukamatwa Gwajima alisema hajapata wito rasmi wa maandishi toka serikalini, lakini hata hivyo akaenda mbali na kutoa ushauri na maelekezo.

Kwamba hata akipokea oda ya kumkamata Gwajima mchungaji basi wataangalia kama kuna jinai na kama basi ipo jeshi la polisi litashauri wamalizane kwa njia ya mazungumzo!

Kwanza mzee Sirro ajue kwamba hili si suala la ndugu wawili mtu na shemeji yake hata atoe ushauri 'wamalizane wenyewe' hili ni la kiserikali.

Pili mzee Sirro alikuwa kwenye nafasi nzuri kabisa kujibu kuwa wanafanga mawasiliano na wizara au na waziri ..! Full stop! Mengine yote aliyoongea hayakuwa mahali pake! Je wakati wa kayafa angefanya hivi?

Mawasiliano ya watendaji yanafanyika mitandaoni na bila kuwasiliana kwanza..yaani ni kama kuna kuoneshana ubabe na ujuaji!
LAKINI ukiachana na hayo yote kuna tatizo kubwa huko ndani, waziri ni mdomo wa rais, akisema waziri ni agizo la serikali lenye ridhaa ya rais na organs za serikali zinachotakiwa kufanya ni KUTEKELEZA KWANZA!

Kuna dharau juu ya wanawake inajitanabaisha hapa na kuna kikundi ndani ya mamlaka hakikubali kuongozwa na wanawake! Je Gwajima na Sirro ni sehemu yao?
Uko right mkuu,inaonesha maisha ya SSH yataishia ingwe hii hii tu,masalia yaliyobaki ya mwendazake yanajaribu kurudisha kiti kwenye himaya yao...masalia ambayo hayana matumaini kwa mtanzania kama ilivyo Taliban kwa wa Afghanistan[emoji3525]
 
Atafunua hadi ya gizani tusiyoyajua...na atampa onyo kuwa akirudia atamalizia kupasua jipu.....Gwajiboy aka Rashid ni shida, Pengo anamjua, na Makonda skimkumbuka anahisi kuharisha[emoji28][emoji28][emoji28]
Gwajiboy ana mafolder yake lazma anayachambua ili Jpili amfanye kitu hakuna😂😂😂 mama kakanyaga waya wa speaker ya disco!
 
Fursa Pesa hebu msome Malisa hapa

Nakumbuka Makonda amewahi kuwaagiza polisi kumkamata Mbowe baada ya kumtaja kwenye orodha ya madawa ya kulevya. Sirro hakusubiri maandishi. Makonda huyohuyo akaagiza Aabdul Nondo akamatwe kwa tuhuma za kujiteka. Sirro hakusubiri maandishi, licha ya kwamba yalikua maelekezo ya Mkuu wa mkoa tu. Leo Waziri katoa maelekezo anasema anasubiri maandishi?

Anyway ni barua gani Sirro alipewa kuwakamata vijana wa Chadema waliokua ibadani huko Mwanza juzi jumapili? Je Sirro alipewa barua na nani kumkamata Askofu Mwamakula na Prof.Azavel Lwaitama usiku wa manane hotelini kama majambazi na kuwaweka rumande bila hatia? Sirro alipewa barua na nani kuwakamata vijana wanaokwenda mahakamani kufuatilia kesi ya Mwenyekiti Mbowe? Why these double standards?

Credit: Malisa GJ
Simple, vita hii haina maslahi wala haigusi maslahi yake kama IGP
 
Msijishushe, huyu mama kwanza hana adabu, haikuwa na sababu kumtemea mbovu Gwaji hadi kutaja mambo ya ngono na kukandia imani yake. Sngesema tunsmuhitaji athibitishe hiyo rushwa.
Msijifiche kwenye kivuli cha mwansmke...subirini spana j2[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Acheni kumtetea huyo gwajma mzinzi anayedaganya watu kuhusu coronavirus na anajifanya eti hagusiki Dorothy alikuwa sahihi aende kwa mkemia kudhibitisha kuhusu madai yake, no research no rights to speak, na hayo ya mkono wa baunsa ilikuwa utetezi wake, kufufua watu na kukataa ubunge lakini Leo yuko bungeni. Gwajima ni mhuni tu ka wahuni wengine nashangaa ccm inachekea ujinga wake wasipo mshughulikia mapema atawanyoosha nchi hii wajinga wengi
 
Sirro hakubaliani na hayo machanjo! Hayuko upande wa support ukiona hivyo, angekuwa huko basi Gwajima angeamkia selo[emoji23] kwa kifupi hii vita haina maslahi kwake!
Sirro ana mfumo dume flani hata mkoa anaotoka huwa Wana dharau wanawake pia hana cha kupoteza maana karibia astaafu. Mimi sijawahi ona insubordination ka ya wakati huu, Wana mwona Rais ni dhaifu na wana machungu ya mwendazake hao
 
Hahahhaha raisi ni dhaifu sio siri! 😂😂😂😂
 
Gwajiboy ana mafolder yake lazma anayachambua ili Jpili amfanye kitu hakuna[emoji23][emoji23][emoji23] mama kakanyaga waya wa speaker ya disco!
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23]
cariha
 
Hahahhaha raisi ni dhaifu sio siri! [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Ni mtu yuko fair akiamua kutumia madaraka yake kikatiba watu wataanza kulia na kusema ni dictator, hata gwajima askofu anajiropokea Ili akichukuliwa hatua ajifiche kwenye kichaka Cha udini kuwa anaonewa
 
Gwajiboy ana mafolder yake lazma anayachambua ili Jpili amfanye kitu hakuna[emoji23][emoji23][emoji23] mama kakanyaga waya wa speaker ya disco!
Kuwa na mafolder sio tija hata yeye watu Wana yake na isiwe excuse ya kudaganya umma apeleke ushahidi kwa mkemia na kudhibitisha kuwa Rais alipokea chanjo fake kweli.
 
Ni mtu yuko fair akiamua kutumia madaraka yake kikatiba watu wataanza kulia na kusema ni dictator, hata gwajima askofu anajiropokea Ili akichukuliwa hatua ajifiche kwenye kichaka Cha udini kuwa anaonewa
Tangu lini Gwajiboy huwa analialia?
 
Hana jipya huyo mnamkuza tu mbona yeye video yake iko kwenye porn site huko duniani yet anajifanya mchungaji
Kwa usomi wako wote hukung'amua kuwa hilo ni tukio la kutengeneza?
 
Ni mtu yuko fair akiamua kutumia madaraka yake kikatiba watu wataanza kulia na kusema ni dictator, hata gwajima askofu anajiropokea Ili akichukuliwa hatua ajifiche kwenye kichaka Cha udini kuwa anaonewa
Hakuna u fair wowote! Watoto hawawezi haribu mpangilio wa sebule we umejikalisha kimya wakati unajua kifuatacho watavunja vyombo halafu ujisemee eti wanangu nawapenda waache wacheze huo ni upunguani😂
 
Hakuna u fair wowote! Watoto hawawezi haribu mpangilio wa sebule we umejikalisha kimya wakati unajua kifuatacho watavunja vyombo halafu ujisemee eti wanangu nawapenda waache wacheze huo ni upunguani[emoji23]
Kila kitu timing even kikwete was fair watu wakamwita dhaifu na sio kila kelele uhangaike nazo na kuzipa uzito, sometimes ku avoid distractions za watu ka gwajima na ujinga wao maana wanataka wachukuliwe hatua wapate sababu, ningekuwa Mimi na Hilo kanisa nalifuta usajili wake kabisa
 
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂 Kwahio kanisa ukilifuta unapata relief
 
Back
Top Bottom