Huyu fundi wa hizi sarakasi ni nani?

Sema nimegundua Mshana una hekima sana. Big up.

Sasa, naona baada ya kumchomoa baba askofu unataka kumchomoa aijipii [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
[emoji2][emoji2][emoji1545][emoji1545][emoji1545] Hao ni wamoja na lao ni moja! Lakini je wako pekeyao ama nyuma yao kuna iceberg?[emoji848][emoji2984][emoji2827]
 
Nidadavulie
Btn lines mwanzoni umedadavua barabara, lakini mwishoni kuhusisha unawake kuwa umedhauliwa kwa kuwa eti labda mwenye kutuhumiwa ni mwanaume na maagizo /amri ya kukamatwa amepewa mwanaume sioni mantiki yeyote.

Alichohitaji IGP ni official document inayoelezea tuhuma dhidi ya Bishop ili wao waweze kutekeleza maagizo. Na sio kwamba wao kama Jeshi la Polisi hwafahamu alichosema Bishop wanajua ndio maana wanataka maandishi ili walinganishe na walichonacho kama vinaendana waweze kumtia hatiani.

Tukumbuke pia Waziri naye anaweza kukosea kwa kutoa amri isiyokuwa na ushaidi hivyo kuliweka Jeshi la Polisi na Takukuru kwenye lawama nyingine mbaya zaidi kuliko issue yenyewe ya chanjo.

Lakini pia yawezekana Jeshi la Polisi limeona kuna nguvu kubwa inayotumika unayotumika kutoa elimu ya chanjo bila kutumia busara na kusababisha wenye Wizara kuparanganyika juu ya nini kifanyike.

Ndio maana IGP Siro akashauri apelekewe maandishi ili kama kuna chochote wajadiliane na wafikie hitimisho pasipo kuleta taaruki ya kusababisha Wananchi kugawanyika pande mbili au zoezi zima kupoteza maana.

Ni wazi kabisa Mh. Waziri alikuwa na jazba kiasi cha pengine kutoa maelekezo yaliyo nje ya kiapo chake.
 
Btn lines mwanzoni umedadavua barabara, lakini mwishoni kuhusisha unawake kuwa umedhauliwa kwa kuwa eti labda mwenye kutuhumiwa ni mwanaume na maagizo /amri ya kukamatwa amepewa mwanaume sioni mantiki yeyote....
Fursa Pesa hebu msome Malisa hapa

Nakumbuka Makonda amewahi kuwaagiza polisi kumkamata Mbowe baada ya kumtaja kwenye orodha ya madawa ya kulevya. Sirro hakusubiri maandishi. Makonda huyohuyo akaagiza Aabdul Nondo akamatwe kwa tuhuma za kujiteka. Sirro hakusubiri maandishi, licha ya kwamba yalikua maelekezo ya Mkuu wa mkoa tu. Leo Waziri katoa maelekezo anasema anasubiri maandishi?

Anyway ni barua gani Sirro alipewa kuwakamata vijana wa Chadema waliokua ibadani huko Mwanza juzi jumapili? Je Sirro alipewa barua na nani kumkamata Askofu Mwamakula na Prof.Azavel Lwaitama usiku wa manane hotelini kama majambazi na kuwaweka rumande bila hatia? Sirro alipewa barua na nani kuwakamata vijana wanaokwenda mahakamani kufuatilia kesi ya Mwenyekiti Mbowe? Why these double standards?

Credit: Malisa GJ
 
Fursa Pesa hebu msome Malisa hapa

Nakumbuka Makonda amewahi kuwaagiza polisi kumkamata Mbowe baada ya kumtaja kwenye orodha ya madawa ya kulevya. Sirro hakusubiri maandishi. Makonda huyohuyo akaagiza Aabdul Nondo akamatwe kwa tuhuma za kujiteka...
Anyway sina majibu ya maswali hayo ☝

Ila ninachoweza kusema labda pengine ukamataji wa Polisi unategemea iwapo kuna viashiria vya kijinai au kukamata kwa ajili ya kutawanya.

Issue ya chanjo yaweza kuwa ni tofauti kabisa na tuhuma nyingine ambazo pengine wao kama Jeshi la Polisi wameona linahitaji majadiliano zaidi, la sivyo linaweza kuingia kwenye lawama pasipo kujua.

Anyway ebu tusubili, yawezekana barua itapokelewa mapema leo.
 
Andiko zuri ila para yako ya mwisho ni uchochezi dhidi ya Sirro
Sirro mwambie kuna kongamano la Chadema, tena bila barua yaani aone tuu mtandaoni kwamba kesho Chadema wana kongamano utaona kama atasubiri barua...
 
Sirro kadinda?! Sirro must go!
Ndugu mheshimika sana mkuu kabisa.na mtu muhimu sana sana kwa hofu kuu na heshima iliyopita viwango vyote na taazima hasa
Nachukua nafasi hii adimu na azimu kwanza kwa kukuomba lazi kutumia muda wako huu lakini pia kukuomba ukamshike yule bwana na kumficha kwenye ghala lako halafu tutalipa gharama zote pamoja na usumbufu na bakshish
 
Duh, sidhani kama anaweza kubembelezwa namna hiyo maana waziri ni zaidi ya IGP. Na Sirro akiiona barua kama hiyo anaweza kupandisha mabega akasema waziri asubiri apate taarifa za kiintelejentsia!

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
Duh, sidhani kama anaweza kubembelezwa namna hiyo maana waziri ni zaidi ya IGP. Na Sirro akiiona barua kama hiyo anaweza kupandisha mabega akasema waziri asubiri apate taarifa za kiintelejentsia!

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
Inategemea maana kuna watu kama CDF, IGP, DG, Gavana wa Benki Kuu etc wakati mwingine wapo chini ya Katibu Mkuu na wala si Waziri ila kuna wakati wapo juu ya Waziri. Inategemea situation ni ipi.
 
Haswaaaa tena aanzee kula jaramba mapema..gwajima ndo rais ajae..hatutak mijitu isiyokuwa na misimamo na kusismamia wanachokiamn raia wake.
 
Kwa thread hii umeniangusha M/KITI.Alichosema IGP ni sahihi kabisa,taratibu zifuatwe wala hajamdharau huyo mama.
 
Hivi maidhui ya mwandishi ni hicho ulichokieleza wewe kweli?

Ni mara ngapi 'system' imelalamikiwa kubambikia watu kesi?

Je wabambikiwa makosa huwaga kuna ushahidi dhahiri wa kiuchunguzi wa kuwaswendema ndani?

Hili neno kubambikia lina tafsiri gani?

Mi namuunga mkono Mshana na wala asijishughulishe na kufuta futa uzi hapa.

Siro hakutakiwa kujadili ama kutoa maoni aliyoyatoa kwenye interview hiyo kwa sababu huko nyuma( awamu ya5)hakujadili hata dakika moja kuchukua hatua kwa yeyote popote na bila maelezo ya uchunguzi wa jinai kufanyika kwanza, uchunguzi ulifanyika watu wakiwa ndani.

Yaani kumekuwa na Siro wawili kwenye wadhifa mmoja katika serikali za awamu mbili?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…